Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 3/1 uku. 3
  • Kuponya kwa Imani—Je! Kunaleta Matokeo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuponya kwa Imani—Je! Kunaleta Matokeo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • NI NINI?
  • JE! HAYO YANAFAULU?
  • Je! Uponyaji wa Imani Hukubaliwa na Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • ‘Uponyaji wa Kimuujiza’ Leo—Je, Unatoka kwa Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Kuponywa Kimuujiza kwa Wanadamu Kuko Karibu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Jinsi Imani Iwezavyo Kusaidia Wagonjwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 3/1 uku. 3

Kuponya kwa Imani​—Je! Kunaleta Matokeo?

“YULE msichana mwenye kitegemeza-shingo kile. Kiondolee mbali’ Umeponywa. Njoo hapa umsifu Yesu.” Msichana huyo anatembea kutoka kitini mwake na kwenda kwenye mimbari (jukwaa). Anasema amepasuliwa mara 12 na amekuwa hajiwezi kutokana na ugonjwa wa baridi yabisi tangu mwaka 1973. Akiwa amesimama mbele ya kuhani huyo, anasogeza shingo yake nyuma na mbele. Kuhani huyo anambariki, umati wa watu unapiga vigelegele na kuhani huyo anasema: “Ameponywa!”’

Ebu wazia furaha ya mtu aliyeponywa ugonjwa wa baridi yabisi! Je! mambo hayo yanatokea kikweli.

Ripoti kama hiyo iliyotokea katika gazeti Sunday Telegram ya Worcester yadokeza (yaonyesha) kwamba huenda ikawezekana. Si ajabu kwamba kuponya kwa imani kwa kisasa kunavutia watu wengi sana. Watu wagonjwa wanamiminika kwa wenye kuponya kwa imani, wakitumaini kupata maponyo. Je! matumaini yao yanatimizwa? Je! kuponya kwa imani kuna matokeo kikweli katika kutibu magonjwa? Kunafaulu?

NI NINI?

Kwa kweli, kuponya kwa imani ni kwa namna tofauti-tofauti. Katika nchi za Uzunguni, mara nyingi kunafanywa katika ibada zinazofanywa na waevanjeli (waeneza Injili) au na wahudumu wa dini kubwa-kubwa​—pengine madhehebu zinazodai zina karama ya kuponya magonjwa. Watu hao wenye kuponya kwa imani wanadai wanamwiga Yesu na mitume wake, na wanaona kwamba Mungu mwenyewe ndiye chanzo cha nguvu zao.

Kikundi kingine ni wale “waponyaji” wa dini zisizo za Kikristo​—wale makuhani wa uchawi, wachawi wanaotibu, wauguzi, na kadhalika. Hao wanaamini kwamba magonjwa yanaletwa na pepo wabaya, nao wanafanya sherehe za kufukuzia mbali pepo hao.

Halafu kuna wale “madaktari wenye uwezo wa roho” ambao wanafanya kile wanachoita “upasuaji wa roho.” Katika Filipino, kwa mfano, wanadai kuwa wanafikia kwa mikono mitupu ndani ya mwili wa mtu mgonjwa na kuondoa visehemu vya mwili vilivyoambukiwa na kuganda kwa damu. Inaripotiwa kwamba “wagonjwa” wao wanakuwa na fahamu kabisa na hakuna alama za vidonda zinazoonekana baadaye.

Mwishowe, kuna wale wanaosema kwamba “kuponya” kwao hakuhusiani na dini wala imani. Wanasema kuwa ni tendo la asili, njia moja ya kutumia nguvu ya siri ya kuponya inayotuzunguka, au iliyomo ndani ya mwili wenyewe. Wengine wa hawa wanapendelea kuitwa “waponyaji wa roho” mahali pa kuitwa “wenye kuponya kwa imani.”

JE! HAYO YANAFAULU?

Jibu la hilo litategemea unayemwuliza ni nani. Wenye kusadiki hivyo wanaeleza juu ya maponyo ambayo wamejionea wenyewe au wao wenyewe wakaponywa. Wenye kutia shaka wanaeleza juu ya wachunguzi ambao wamefuatia visa hivyo vya yaliyodaiwa kuwa maponyo ya kimwujiza na wamekata maneno kwamba jambo hilo halitokei. Kwa sababu gani kuna kupingana huko?

Nyakati nyingine kuna uwezekano wa kosa linalotokea kikweli. Mwanamke mmoja alisadiki kwa unyofu kwamba alikuwa ameponywa kansa (donda baya) ya sehemu ya kiungo cha uke. Alichunguzwa katika hospitali ikaonekana kwamba alikuwa na kansa. Kwa hiyo akamwendea mtu mwenye kuponya kwa imani. Pindi iliyofuata alipochunguzwa kansa haikuonekana. Mwanamke huyo anasadiki kwamba mtu huyo mwenye kuponya kwa imani alimponya. Walakini daktari wake alisema kwamba matokeo ya kwanza ya ule uchunguzi yalikuwa yenye kosa tu, kama inavyotokea nyakati fulani.

Nyakati nyingine, watu wanaotumaini sana mwujiza wanatamani mambo yawe vingine. Msichana mchanga aliyekuwa na maradhi makali sana ya kansa alimwendea mtu mwenye kuponya kwa imani. Baadaye alichunguzwa tena na daktari wake. “Wakati daktari aliponiona hakuweza kuamini,” msichana huyo akasema kwa furaha. “Nilipaswa kufa katika muda wa miezi miwili. Lakini hakuna jambo lililotokea . . . sipaswi kuwa hai lakini sijui kwa sababu gani Mungu aliniokoa mimi.” Kwa kusikitisha, muda usiozidi mwaka mmoja baadaye alikufa.

Wakati mmoja, daktari mmoja yasemekana alisema kwamba kupata nafuu kwa mgonjwa wake kulikuwa mwujiza. Hata hivyo, wakati ripota wa habari ya magazetini alipofuatia hadithi hiyo, daktari huyo alisema kwamba neno “mwujiza” lilikuwa namna ya usemi. Yeye alikuwa na hakika ponyo hilo lilikuwa “tukio la asili.” “Sidhani tunaweza kuthibitisha kwamba Mungu alihusika kibinafsi,” akasema, “Nimeona jambo lilo hilo likitokea wakati kuponya kwa imani hakukuhusika.”

Kuna mambo yanayofanya iwe vigumu kuamua ni nini hasa kilicholeta “maponyo” fulani. Matokeo ya akili juu ya afya ya mwili yangali yanafahamika kidogo tu. Maendeleo ya maradhi mengi hayaelezeki kimbele. Mengine yanakwisha bila sababu inayojulikana. Magonjwa mengi yanaponywa na mwili wenyewe, nyakati nyingine kwa msaada wa dawa. Dakt. William A. Nolan alipendekeza kwamba yaweza ikawa kwamba maono ya moyoni yenye nguvu sana ya ibada fulani za kuponya yanafanya magonjwa fulani yaishe haraka zaidi ya ilivyo kawaida. Yapasa kuangaliwa kwamba maponyo mengi yanayodaiwa ni kufanya hali ya mgonjwa iwe afadhali kidogo tu.

Watu wengine wenye kuponya kwa imani wanautambua uwezekano wa kwamba maponyo mengi si ya kimwujiza. Kuhani mmoja anayedai ana karama ya kuponya magonjwa, alisema: “[Maponyo] mengine ni uhusiano wa mwili na maono ya moyoni na mengine ni kuvurugika akili na mengine yanaweza kuelezwa kuwa ni ya asili.” Kisha akaongeza hivi: “Sitatizwi na hayo kwa sababu bado ni ya kweli.”

Bila shaka, si wote wanaokubali wazo la kwamba maponyo hayo ni ya asili. Kwa unyofu wengi wanasadiki kwamba miujiza hutokea na kwamba wagonjwa wanaponywa kwa nguvu fulani inayozidi nguvu za kibinadamu. Kwa hiyo, mtu anayetaka kujua huenda akawaza hivi: ‘Aaa, kuponya kwa imani kwaweza kufaulu, au kusifaulu. Walakini kujaribu jambo hilo kwaweza kuleta umizo gani?’ Hilo ni ulizo la maana.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki