Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w83 3/1 kur. 4-5
  • Hali ya Ujirani Imekwenda Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hali ya Ujirani Imekwenda Wapi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Habari Zinazolingana
  • Wewe Unaweza Kuwa Jirani Mwema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Majirani Wema Wanafaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Mbona Leo Hakuna Majirani Wanaojali?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Jirani Wema—Tunawahitaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
w83 3/1 kur. 4-5

Hali ya Ujirani Imekwenda Wapi?

KWA sababu gani watu wengi wanaoishi karibu nawe wameacha kutenda mambo kama majirani? Wachunguzi wanataja sababu kadha, na nyingi kati yazo zinahusu mitindo ya kisasa ya maisha.

Kuhama-hama ni sababu moja. Watu wengi wanahama-hama sana. Basi wanakuwa na wakati mchache wa kujua jirani zao na kusitawisha hali ya ujirani.

Miji yenye kuachwa upweke ni sababu nyingine pia inayotajwa. Hayo ni maeneo ya ujirani ambako jamaa nzima-nzima zinakwenda kazini au shuleni na kukosa kuwako nyumbani saa za mchana. Saa za jioni wanakwenda tena kutembea au wanaketi nyumbani kwa unyamavu wakiwa wamezunguka televisheni kuitazama. Katika nyumba ya namna hiyo, mara nyingi washiriki wa jamaa hawawi wageni kwa jirani zao tu. Wanakuwa sura ngeni kati yao kwa wao pia.

Ufundi wa uchoraji wa ramani za nyumba na upangaji wa mahali nyumba zitakapojengwa ni jambo jingine pia linaloharibu hali ya ujirani. Kuna orofa fulani zinazojengwa kila nyumba ikiwa na vifaa vyote vinavyohitajiwa, kama kwa mfano bafu na vyoo. Jamaa zinazoishi katika majengo ya namna hiyo hazionani sana na jirani zao.

Ile fahari ya kujitakia faragha (kujitenga na wengine wasikusumbue unapoendesha shughuli zako) inalaumiwa pia. Katika mikoa fulani hali ya kuwa na faragha inathaminiwa sana. “Huwezi kujipeleka bila mpango ukabishe hodi kwenye mlango wa nyumba yake ili kumtembelea,” akasema mkaaji wa eneo la kando ya mji mmoja. Mwanamke mmoja alitembelewa bila kutazamia na mwanamke mjane wa ujirani huo ambaye alilalamika kwamba alikuwa mpweke. Huyo mwenye kutembelewa alimwambia mjane huyo aende zake, akachukizwa kwamba alijaribu kumtembelea akiwa katika hali yake ya faragha. Usiku huo mjane huyo mpweke alijiua.

Uhalifu ni jambo jingine linalotajwa kuwa sababu. Kuogopa uhalifu kumefanya maeneo fulani ya ujirani yawe magereza ya nyakati za usiku kwa maana jamaa nyingi zinafunga milango kwa hofu jua likiisha kushuka, na ni watu wachache huko wanaothubutu kwenda nje.

Bila shaka mambo yote hayo yameshiriki kupunguza hali ya watu ya kujisikia wao ni jirani za wengine. Lakini lazima kuwe kuna sababu kubwa zaidi zinazofanya mengine ya mambo hayo yatukie. Katika eneo moja linalokaliwa na watu, mwanamke kijana alifuatwa-fuatwa na mwanamume mmoja muda wa nusu-saa. Alimshambulia mwanamke huyo mara tatu na mwishowe akamchoma kisu akafa. Jirani 38 walimsikia akipiga-piga mayowe au wakamwona akishambuliwa, lakini walilipuza jambo hilo. Mmoja tu ndiye aliyeita polisi mambo yakiwa yamekwisha kuharibika kabisa. Namna hiyo ya ubaridi wa kutokusaidia jirani za mtu ni hali iliyoenea sana.

Hali hiyo ya unyama inaonyesha makosa mazito katika nyutu za wale wanaohusika. Mtu anayejifunza Biblia anakumbushwa na matukio hayo ule unabii wa mtume Paulo unaohusu siku zetu: “Watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, . . . wasiowapenda wa kwao, . . . wasiotaka kufanya suluhu, . .. wasiojizuia, . . . wasiopenda mema, . . . wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu.”​—2 Timotheo 3:2-4.

Utimizo wa maneno hayo unamaanisha kwamba tunaishi katika nyakati za hatari sana, na huenda hali hizo zikawa zinaonekana sana katika ujirani unamoishi. Hata hivyo, hakuna sababu ya kutuzuia sisi mmoja tusiwatendee kijirani watu wanaoishi karibu nasi. Huenda kufanya hivyo kukaanza kuwachangamsha moyo. Ni gani ya hekima ya kuwa jirani mwema leo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki