Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w83 1/1 uku. 24
  • Ufahamu Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufahamu Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kusema “Hapana” kwa Ngono za Tineja
  • Ngono—Ni Shauri Gani Hasa Lihalofaa?
    Furaha​—Namna ya Kuipata
  • Ni Nini Huathiri Mtazamo Wako?
    Amkeni!—1997
  • Wafundishe Watoto Wako Maadili Mema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Ninaweza Kufanya Nini Ili Kupinga Shinikizo la Kufanya Ngono?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
w83 1/1 uku. 24

Ufahamu Katika Habari

Kusema “Hapana” kwa Ngono za Tineja

Ufanyaji ngono wenye kuongezeka kati ya vijana umesukuma serikali nyingi zifanye dawa za kuzuia mimba zipatikane kwa matineja. Hilo ni jambo la hekima jinsi gani? Jarida British Medical Journal lilitoa maoni haya hivi karibuni: “Kuwapa dawa za kuzuia mimba watu wenye umri wa chini sana bila shaka kunaonyesha kuendekeza maoni ya ufanyaji wa ngono.” Lakini je, nia hiyo kweli kweli inaleta faida bora sana kwa vijana?

“Ushuhuda unaonyesha uchukuaji mimba wa tineja unaleta umizo,” ndivyo jarida hilo linavyojibu. “Kwenda shule kunapungua, mataraja ya kazi ya kuajiriwa yanapungua na hesabu ya talaka inakuwa juu. Hakuna ushuhuda wo wote kwamba kufanya ngono kunawafaidi watoto na kwa kuwa ufanyaji ngono ni jambo la kisilika na pia ni tabia anayojifunza mtu, ni sawa na tatizo la matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Tabia ya kufanya ngono mapema haielekezi kwenye ufanyaji ngono mzuri katika maisha ya baadaye, hali ya kujifunza yenye maendeleo zaidi au ufanyaji kazi wenye maendeleo zaidi. Inaelekea unaongoza kwenye kutoweza kufanya ndoa inayofaa na ya kudumu. . . . Njia pekee yenye upatani ya kupunguza umizo hilo la ufanyaji ngono wa wenye umri wa chini sana ni kukaza jitihada zote katika kuzuia ufanyaji ngono.”

Vivyo hivyo, mwalimu wa ngono Mmarekani mwenye kujulikana ulimwenguni pote, Dakt. Sol Gordon, alisema majuzi hivi kwenye mkutano wa walimu wa ngono: “Siwezi kuwazia sababu yo yote nzuri ya matineja kufanya ngono. Ngono inahatirisha afya kwa wavulana na wasichana.” Akiitaja ngono ya matineja kuwa “msiba wa kijamii wa taifa,” alisema kwamba “bila maarifa na elimu, matineja wengi sana hawajatayarishwa kusema hapana.” Uongozi na elimu hiyo kwa kufaa zaidi inatoka kwa wazazi wanaoeleza wazi maoni ya Mungu juu ya ngono nje ya ndoa. Matineja wanahitaji kutii ambayo mtume Paulo alimwambia mwanamume kijana Timotheo: “Zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”​—2 Timotheo 2:22.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki