Mahitaji Yetu—Je! Serikali Zinaweza Kuyajaza?
CHAKULA cha kutosha, maji safi ya kunywa, mavazi yanayofaa na nyumba ya kuishi ndani yake—hayo ni mambo ya lazima kabisa maishani. Ulimwenguni pote watu wanajitahidi kutafuta mahitaji hayo ya lazima, chini ya kila aina ya mfumo wa kiuchumi.
Je! wewe unatumia nyingi za saa zako za mchana ukijaribu kuyajaza? Je! serikali ya nchi unamoishi inatolea watu njia ya kuyapata mahitaji yao kwa njia ya kuyatosheleza? Ni kumbukumbu gani limewekwa ulimwenguni pote na serikali katika jambo hili?
Chakula
“Watu wasiopungua milioni karibu 450—labda kufikia bilioni moja—wana chakula kidogo sana kuliko kile wanachohitaji ili waendelee kuwa hai.”—Scientific American.
“Mabadiliko katika ulaji wa mtu wa wastani katika United States wakati wa karne hii yametokeza ukosefu wa chakula kinachoifaa miili kati ya watu wengi . . . unaoweza kuharibu afya kwa sababu unaleta ugonjwa wa mkazo wa mishipa ya damu na magonjwa mengine yaliyokolea mwilini.”—Ushuhuda wa matabibu, wachunguzi wa vyakula vyenye kufaa mwili na wanasayansi. Waliipa ushuhuda huo Halmashauri iliyoteuliwa na Bunge Kuu la United States.
Maji ya Kunywa
”Zaidi ya nusu ya watu wa nchi za ulimwengu ambazo ndiyo sasa tu zimeanza kuwa na maendeleo hazina maji yaliyo salama kwa kunywewa.”—Earthscan, ambalo maneno yake yalitumiwa na gazeti World Press Review.
“Mto huo [Rhine, ulio chanzo cha maji ya kunywewa na Wanaulaya milioni 18] unasafirisha takataka za watu milioni 60 . . . Mwaka wa 1973, karibu asilimia 55 za maji hayo yenye takataka hazikutiwa dawa za kuua vijidudu au zilitiwa kwa kiasi kidogo tu kabla hazijaingizwa katika mto huo.”—World Health (gazeti la Tengenezo la Afya Ulimwenguni).
“Maji ya nchini katika sehemu kubwa zaidi ya [United States] yanaelekea kuwa katika hatari ya kuharibiwa na uchafuzi wenye kuenea kote kutokana na kemikali zenye sumu.”—The New York Times.
Mavazi na Mahali pa Kukaa
Ulimwenguni pote “watu milioni 800 hawana makao.”—El Tiempo, Kolombia.
Katika nchi moja ya Amerika ya Kusini iliyo na uthabiti wa kiasi fulani “zaidi ya nusu [ya idadi ya watu wa nchi hiyo] . . . hawana mavazi mazuri, tena wanaishi katika nyumba mbaya-mbaya na wanakuwa na ukosefu wa maji ya kunywa.”—El Espectador, Kolombia.
Kwa Sababu Gani Upungufu Huo Unaendelea?
Serikali zinatoa sababu nyingi za upungufu huo. Wewe fikiri uone kama zinafaa.
1. Lawama la sehemu kubwa ya hali ya kukosa chakula kinachoufaa mwili linawekwa juu ya ujinga wa watu. Watu hata hawajui vyakula wanavyopaswa kula.
2. Wengine wanasema ulimwenguni mna chakula cha kutosha lakini, kama vile habari zinazotangaza zinavyoonyesha, “ukosefu wa usafirishaji, wala si ukosefu wa chakula, ndio moja ya sababu kubwa za kutokeza njaa na kupungukiwa kwa mwili na vyakula vinavyofaa katika zile nchi za ulimwengu ambazo ndiyo sasa tu zimeanza kufanya maendeleo.”
3. Tengenezo la Chakula cha Ukulima linadai kwamba mazungumzo ya polepole ya kujaribu kufikia mapatano na kanuni za ulinzi zinazuia nchi zinazozidi kupata maendeleo zisipate njia ya kuyaingia masoko ya nchi zilizokwisha kuendelea.
4. Mataifa mengi yanajikuta yakilazimika kuchagua kati ya kununua silaha na kuwapa maskini chakula wanachohitaji. Pesa zinazotumiwa kila mwaka kuhusu silaha za ulimwengu “zingetosha kujaza mahitaji yale ya msingi ya nchi zilizoanza kupata maendeleo hivi majuzi mpaka mwaka wa 2000 . . . Hata kupunguza kidogo tu gharama za mambo ya ulinzi kungefanya iwezekane kuwapa watu milioni 1,200 maji ya kunywa, na maji ni kimoja cha vitu vilivyo vya lazima maishani. Kama zile pesa zinazotumiwa kujenga na kuendesha meli moja ya kisasa yenye kupita chini ya bahari zingetumiwa katika ujenzi, nyumba nzuri 450,000 zingeweza kujengwa.”—El Tiempo.
Sababu Kubwa ya Msingi
Labda wewe utakubali kwamba matatizo yaliyotajwa yanashiriki kuleta magumu ya kuwapa wanadamu mahitaji yao ya lazima. Lakini kuna tatizo jingine lililo kubwa zaidi ya hayo: Huu mfumo wa mambo unatia kila mtu moyo ajitegemee na kujifikiria mwenyewe tu. Watu ‘wanataka kujipatia nafasi ya kwanza’ kwa kuwapita wenzao. Mazingira yanachafuliwa kwa sababu ya watu kutaka kujipatia faida kwa njia za kibiashara. Makundi ya kijamii yanatumia wivu kulinda mapendeleo yao na hayataki kujinyima ili yasaidie wale wasio na vitu vingi kama wao. Mataifa yanatetea vikali sana enzi zao na kuendeleza mapendezi yao wenyewe, bila kujali ni nani mwingine anayetaabika,
Ni wazi kwamba ushirikiano ulio bora kabisa kati ya mataifa unatakwa ndipo mahitaji yaliyo ya lazima kwa wanadamu wote yaweze kujazwa. Katika mfumo wa mambo ya sasa mtu mwenye kudhania-dhania mambo ndiye peke yake anayefikiri kwamba ushirikiano wa namna hiyo utakuwako. Ebu sema kweli. Je! wewe unafikiri utakuwako?
Je! Kuna Utatuzi?
Ndiyo, kuna utatuzi. Lakini unatokana na chanzo kisichotambuliwa na watu wengi. Huenda hata kikakushangaza wewe.