Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 2/15 kur. 3-4
  • Yule Farasi Mweusi wa Njaa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yule Farasi Mweusi wa Njaa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Habari Zinazolingana
  • Wapanda Farasi Wanne​—Jinsi Wanavyokuhusu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Njaa Ina Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 2/15 kur. 3-4

Yule Farasi Mweusi wa Njaa

“NA TAZAMA, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.”​—Ufunuo 6:5, 6.

Kwa maneno hayo ya kusikitisha, mtume Yohana anaeleza habari za yule wa tatu kati ya wapanda farasi wanne wa kitabu cha Ufunuo, yule mwenye kuendesha farasi mweusi wa njaa.a Je! wewe umetaka kujua ni wakati gani anapoanza kuendesha farasi wake? Inakupasa utake kujua. Uendeshaji wake unatangaza badiliko lililo kubwa kabisa ambalo ulimwengu huu haujapata kuona.

Wengine wana maoni ya kwamba sikuzote huyo mpanda farasi amekuwa akiendesha kati ya wanadamu. Na ni kweli kwamba historia imejawa na masimulizi ya njaa kurudi nyuma mpaka siku za Abrahamu na Yusufu na mpaka wakati wa njaa kubwa zaidi iliyopata kuandikwa katika historia, yaani, ile iliyoipiga China kati ya mwaka wa 1878 na 1879. (Mwanzo 12:10; 41:54) Makadirio ya hesabu ya Wachina waliouawa na njaa hiyo ni kati ya milioni 9 na milioni 13.

Lakini, yule farasi mweusi na mwendeshaji wake hawahusiani na upungufu wote wa chakula wa historia. Kwa sababu gani? Kwa sababu katika njozi yake, Yohana aliona huyo farasi mweusi akitanguliwa na yule farasi mwekundu wa vita, na pia akitanguliwa na mwendeshaji aliyevaa taji ya kifalme akiwa amepanda farasi mweupe. Mwendeshaji huyo ni Yesu Kristo, aliyewekwa karibuni kuwa Mfalme na anayeenda “akishinda na kumaliza ushindi wake.” (Ufunuo 6:1, 2, NW) Kwa hiyo, yule farasi mweusi mwenye kuruka-ruka na mpandaji wake wanafananisha upungufu wa chakula unaoumiza dunia wakatia Yesu anapowekwa kuwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu.

Njozi ya wapanda farasi wa kitabu cha Ufunuo inalingana na unabii ambao Yesu mwenyewe aliutamka. Wakati mmoja alitabiri kwa urefu hali ambazo zingekuwa duniani kuonyesha kuwapo kwake akiwa Mfalme asiyeonekana wa kimbingu. Sehemu moja ya unabii huo ilisema hivi: “Taifa litainuka juu ya taifa na ufalme juu ya ufalme, na kutakuwako upungufu wa chakula na matetemeko ya ardhi mahali hapa na mahali hapa.”​—Mathayo 24:3, 7, NW.

Ni wakati gani ishara hiyo inapotimizwa? Ni wakati gani hasa mpandaji wa farasi mwenye kuleta njaa anapoendesha farasi wake akiipitia dunia? Kwa miaka mingi Mashahidi wa Yehova wamejulisha watu kwamba kizazi kile kilichouona mwaka wa 1914 ndicho kimeshuhudia matokeo ya kupita kwa mpandaji farasi huyo. Je! ufahamu wao ni sahihi?

‘Bila shaka si sahihi,’ huenda wengine wakasema. ‘Dunia inazaa chakula kingi kuliko ilivyokuwa ikifanya zamani, shukrani kwa ukulima wa kisasa. Kuna mashirika yanayohusiana na Umoja wa Mataifa, kama Tengenezo la Chakula na Ukulima (FAO), yanayojaribu kuhakikisha kila mtu anapata chakula cha kumtosha. Zaidi ya hivyo, viwango vya maisha vimepanda juu kwa njia ya kustaajabisha katika maeneo fulani. Mataifa kama Uingereza, ambako njaa ilikuwako kwa wingi zamani, sasa hayaoni sana upungufu wa chakula. Leo nchi nyingi zinafurahia kiwango cha juu zaidi cha maisha ambacho hakijapata kuonekana siku za huko nyuma. Sasa basi tunawezaje kusema kwamba kizazi hiki ndicho kitakachoumizwa zaidi ya vizazi vyote na matokeo ya yule farasi mweusi wa njaa?’

Hilo ni ulizo la kupendeza. Ni kweli kwamba wanadamu wamevumilia upungufu wa chakula muda wote wa historia. Mtume Yohana na hata Yesu mwenyewe walijua hivyo. Hata hivyo walitabiri wakati ambao njaa ingeipiga dunia kwa njia kubwa inayostahili kufikiriwa. Ni kwa njia gani upungufu huo wa chakula ungestahili kufikiriwa? Na kwa kuwa sehemu kubwa ya ulimwengu wa kisasa ina ufanisi wa vitu vya kimwili, je! kuna sababu yo yote ya kuamini kwamba kizazi kilicho hai sasa kinashuhudia upungufu wa chakula?

[Maelezo ya Chini]

a Ili upate habari juu ya wapanda-farasi wote wanne na maana yao ya kiunabii, tafadhali ona toleo letu la Oktoba 15, 1983.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki