Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 3/15 kur. 4-7
  • Matetemeko ya Ardhi Ni Ishara ya Ule Mwisho?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matetemeko ya Ardhi Ni Ishara ya Ule Mwisho?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Matetemeko ya Ardhi—Yesu Alikuwa na Maana Gani?
  • Matetemeko ya Ardhi ya Kisasa
  • Ni Wazi Kwamba Ni Sehemu ya Ile “Ishara”
  • Mengine ya Matetemeko Yaliyotokea Kati ya 33-70 W.K.
  • Mengine ya Matetemeko ya Ardhi Yaliyotokea Kati ya 1914 na 1982
  • Matetemeko Makubwa ya Ardhi—Biblia Ilitabiri Nini?
    Habari Zaidi
  • Matetemeko ya Dunia—Taabu Juu ya Taabu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Matetemeko ya Ardhi, Unabii wa Biblia, na Wewe
    Amkeni!—2002
  • Matetemeko ya Ardhi Je! Yanasababishwa na Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 3/15 kur. 4-7

Matetemeko ya Ardhi Ni Ishara ya Ule Mwisho?

WANAUME wanne walikuwa wameshangaa wakiwa na Yesu peke yao katika kilima kirefu, chenye kuzungukwa na mizeituni yenye kupindika-pindika, mji wa Yerusalemu ukiwa kule chini yao. Mapema siku hiyo walikuwa wamemsikia Kiongozi wao, Yesu Kristo, akitabiri kwamba Yerusalemu na hekalu lao ungeharibiwa na ‘jiwe lisibaki juu ya jiwe jingine.’ Kwa kustaajabu, wao wakauliza hivi: “Mambo hayo yatakuwa wakati gani? ” Wao walipendezwa kulisikia jibu la Yesu kwa makini. Lakini jibu lake linapasa kutupendeza zaidi leo.—Mathayo 24:1-3, NW.

Jambo ambalo mitume walitaka kujua wakati huo ni uharibifu wa Yerusalemu. Lakini hamu yao ya kutaka kujua haikumalizika baada ya ulizo hilo moja, kwa maana wao walitaka pia kujua wakati wa kuwapo kwa Yesu wakati ujao akiwa katika utukufu wa Ufalme na wakataka wajue ni wakati gani wangetazamia mwisho wa taratibu yenye uovu. Waliuliza hivi: “Ni nini itakayokuwa ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo? ” Jibu alilotoa Yesu liliwaridhisha wafuasi wake wa karne ya kwanza. Jibu lake lilikuwa juu ya “Ishara” inayoweza kuridhisha wafuasi wake wa kisasa pia ambao wanatamani sana kuuona uovu ukimalizika, kwa maana utimizo wa ishara yenyewe unatokea siku zetu.

Ishara aliyoitoa Yesu ina sehemu fulani za waziwazi, zinazofahamiwa vyepesi kila mahali. Hazitendeki kwa njia isiyo wazi wala hazikosi kuonekana. Angalia sehemu moja ya jibu la Yesu kwenye Mathayo 24:7 (NW ): “Kwa maana taifa litainuka juu ya taifa na ufalme juu ya ufalme, na kutakuwako upungufu wa chakula na matetemeko ya ardhi mahali hapa na mahali hapa.” Wakati vita vinapotokea, mataifa yanajua vimetokea. Wakati watu wanapokuwa na njaa—kufa njaa—mataifa yanajua. Na wakati tetemeko la ardhi linapoutikisha udongo ulio chini ya miguu yako, wewe unajua imekuwa hivyo, kwa sababu tetemeko la ardhi ni moja la matukio ya asili yaliyo ya kutisha zaidi ambayo yanaweza kupata watu. Mambo hayo na mengine yanayoonekana kwa njia kubwa ndiyo yanayokuwa ile “ishara” nayo yote yanataabisha wanadamu muda wa kizazi kimoja. (Mathayo 24:3, 34, NW ) Acha tuchunguze sehemu moja ya “ishara” hiyo, yaani, matetemeko ya ardhi.

Matetemeko ya Ardhi—Yesu Alikuwa na Maana Gani?

Yesu hakuwa mtaalamu wa kuchunguza mambo ya matetemeko ya ardhi. Alikuwa mhubiri na mwalimu, na nabii pia. Akiwa ‘amejaa roho takatifu’ na akiwa chini ya mwelekezo wa hiyo kani (nguvu) ya utendaji isiyoonekana ya kutoka kwa Yehova, Yesu alitoa unabii juu ya matetemeko ya ardhi na mambo mengine ya ile “ishara.”—Luka 4:1; 8:28.

Je! kulikuwa na utimizo wa karne ya kwanza wa maneno ya Yesu? Ndivyo. Historia ya Kibiblia na ya kilimwengu ina kumbukumbu za hesabu kubwa ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea kati ya mwaka wa unabii wake, mwaka wa 33 W.K., na kuharibiwa kabisa kwa Yerusalemu mwaka wa 70 W.K. Mitikisiko miwili ya ardhi ilitikisa Yerusalemu katika muda wa siku ambazo Yesu alitoa unabii wake. Mathayo 27:51; 28:2) Miaka kumi na saba baadaye tetemeko la ardhi lilitukia katika mji wa Filipi, kama Luka mwandikaji wa Biblia alivyoandika. (Matendo 16:26) Tena, wanahistoria wasio wa Kibiblia wanaonyesha matetemeko ya ardhi makubwa-makubwa yasiyopungua sita yaliyotokea katika sehemu hiyo ya dunia wakati wa kipindi hicho. (Ona Orodha ya Kwanza.)

Ni nini kilichofanya matetemeko ya ardhi yawe mambo ya pekee katika karne ya kwanza? Na je! ripoti ya kutokea kwa tetemeko la ardhi ilikuwa habari zisizo za kawaida kwa Wakristo wa karne ya kwanza? Kujibu maulizo hayo kunaweza kutusaidia tufahamu maana ya matetemeko ya ardhi ya siku zetu.

Kwa kuwa ile sehemu ngumu ya ardhi iliyo chini ya uso wa dunia katika maeneo ya kando-kando ya Bahari ya Kati, kutia ndani Yerusalemu, iko katika eneo ambalo lina maelekeo ya kiasi ya kupatwa na matetemeko ya ardhi, na hivyo ingeweza kuwa na mtikisiko, mitetemo ya ardhi haingekuwa jambo lisilo la kawaida kwa wakaaji wa karne ya kwanza wa eneo hilo. Kwa mfano, lile Bonde Kuu la Mto Yordani na Bahari ya Chumvi na maeneo ya ng’ambo yenye mielekeo ya kutetema ambayo ndiyo yanakuwa Uwanda wa Esdraeloni (Yezreeli) kati ya Galilaya na Samaria yalisemwa kuwa yenye matetemeko ya ardhi hata kabla ya karne ya kwanza.—Amosi 1:1; Zekaria 14:5.

Matetemeko ya ardhi yakiwa pekee hayangeleta umaana wa pekee kuhusu “ishara” ya kiunabii ya Yesu juu ya mwisho uliokuwa ukikaribia kuupata Yerusalemu, kama vile homa kali isisvyoweza kujulisha wazi ni ugonjwa gani hasa ulio katika mtu ikiwa hakuna dalili nyingine za kuutambulisha. Basi, jambo lililoongeza maana kwenye utabiri wa Yesu juu ya matetemeko ya ardhi ni kwamba yalitukia kwa mwungano pamoja na sehemu zile nyingine zote za ile “ishara.” Na “ishara” hiyo yenye matukio mengi yaliyotabiriwa ndiyo iliyoshuhudiwa na Wakristo wa karne ya kwanza nao wakaiitikia.

Matetemeko ya Ardhi ya Kisasa

Je! utabiri wa Yesu juu ya matetemeko ya ardhi unatimia katika karne ya 20? Yaani, kumekuwako matetemeko ya ardhi makubwa yanayoonyesha kwamba tunaishi kwenye “umalizio wa mfumo wa mambo”? Mambo ya uhakika yanathibitisha kwamba karne hii inatikiswa sana na matetemeko ya ardhi. Dunia inapatwa na mitetemo zaidi ya 1,000,000 kwa mwaka, na 1,000 kati ya hiyo inakuwa matukio yenye kushtua na kuleta madhara.

Wataalamu fulani wa mambo ya matetemeko ya ardhi wanaamini kwamba sasa dunia iko katika kipindi cha kuelekea sana kusababisha matetemeko ya ardhi. Kwa mfano, Profesa Keiiti Aki wa Idara ya Dunia na Sayansi za Mambo ya Sayari wa huko kwenye Taasisi ya Ufundi ya Massachusetts anataja “mwelekeo wa kuongezeka kwa uzito na visa vya matetemeko ya ardhi yaliyo makubwa-makubwa wakati wa miaka mia moja iliyopita,” ingawa anataja kwamba kipindi cha kuanzia mwaka wa 1500 mpaka wa 1700 kilikuwa chenye matetemeko ya kadiri iyo hiyo.

Katika jarida la Kiitalia linaloitwa Il Piccolo, la Oktoba 8, 1978, Geo Malagoli alitoa maoni haya:

“Kizazi chetu kinaishi katika kipindi chenye hatari ya kutokea mara nyingi kwa matetemeko ya ardhi, kama inavyoonyeshwa na takwimu. Kwa kweli, wakati wa kipindi cha miaka 1,059 (kuanzia mwaka wa 856 mpaka 1914) vyanzo vyenye kutegemeka vinapanga katika orodha matetemeko ya ardhi yaliyokuwa makubwa 24, nayo yalisababisha vifo 1,973,000. Lakini [katika] misiba ya majuzi, tunakuta kwamba watu 1,600,,000 wamekufa katika muda wa miaka 63 tu kutokana na matetemeko ya ardhi 43 yaliyotukia kuanzia mwaka wa 1915 mpaka wa 1978. Ongezeko hilo la kutazamisha linakazia uhakika mwingine unaokubaliwa—kizazi chetu ni chenye kupatwa na maafa kwa njia nyingi.”

Yesu alitabiri kwamba “umalizio wa mfumo wa mambo” ungeonyeshwa na “matetemeko ya ardhi mahali hapa na mahali hapa”, na kulingana na masimulizi ya Luka, yangekuwa “matetemeko ya ardhi makubwa.” (Mathayo 24:3, 7; Luka 21:11, NW) Je! kizazi ambacho kilikuwa kikiishi mwaka wa 1914, ambacho kingali na wengi walio hai sasa, kiliyashuhudia mambo hayo? Mambo ya uhakika yanajibu, Ndivyo! (Ona Orodha ya Pili.) Na bado matetemeko ya ardhi yanashuhudiwa, si na waliosalia tu wa kizazi hicho, bali pia na hesabu ya watu iliyo kubwa kupita zote katika historia. (Mathayo 24:34) Wanadamu leo wanajua zaidi habari zinazohusu utendaji wa vile matetemeko ya ardhi yanavyotokea duniani pamoja na matokeo ya matetemeko yenyewe. Wanajua zaidi ya watu waliokuwa katika karne yo yote iliyopita.

Ni jambo gani lingefanya tetemeko la ardhi lihesabiwe kuwa ‘kubwa’? Je! ni uzito walo, au eneo kubwa linalopatwa, kama ilivyopima mizani ya Mercalli au ya Richter? Au, badala ya kuhesabiwa hivyo kile ambacho kingehesabiwa ni sifa mbaya ya tetemeko la ardhi na kiasi cha uharibifu ambao limeleta? Kama inavyoonyeshwa na Orodha ya Tatu iliyo hapa, hesabu ya wanadamu waliouawa na matetemeko ya ardhi imeongezeka ajabu tangu mwaka wa 1914. Ni kweli kwamba matetemeko mengine yaliyo makubwa kabisa yametokea ndani sana ya bahari zilizo kuu, bila kujulikana na watu wengi na bila kuleta madhara kwenye mali au uhai wa kibinadamu. Lakini, katika kuamua utimizo wa kisasa wa unabii wa Yesu, haitupasi kuelekeza fikira kwenye ukubwa tu wa matetemeko kulingana na mizani ya Richter wala kwenye mizani nyingine kama hiyo, bali inatupasa tuamue kwa kuangalia kiasi cha madhara ambayo yamepata mali za watu na hesabu ya wanadamu ambao wameuawa.

Ni Wazi Kwamba Ni Sehemu ya Ile “Ishara”

Gazeti Europe (Ulaya) la Julai—Agosti 1980 linasema hivi: “Katika karne hii, matetemeko ya ardhi yameua watu wapatao 1,600,000, na ni watu 120,000 ambao wamekufa katika Ulaya pekee.” Kwa hiyo tunapoiona hali ya ulimwengu na kuilinganisha na maneno ya Yesu tunaweza kukubali kwamba “matetemeko ya ardhi mahali hapa na mahali hapa” na hata “matetemeko ya ardhi makubwa”yamekuwa yakitukia. Je! kuna kizazi cho chote kimoja cha nyakati zilizopita ambacho kimepatwa na uharibifu mbaya sana wa matetemeko ya ardhi kama ule unaotaabisha wanadamu tangu mwaka wa 1914? Takwimu zinaonyesha hakuna.

Lakini, wengine watasema hivi: “Hiyo ni kwa sababu sasa watu ni wengi zaidi duniani.” Ni kweli kwamba hesabu ya wanadamu imeongezeka, lakini jambo hilo halifanyi unabii wa Yesu ukose matokeo. Bali, linauongezea mkazo, na kutupa sisi sababu kubwa zaidi ya kutii maneno yake. Kwa sababu gani? Kwa sababu watu 2,000,000,000, karibu nusu ya hesabu ya watu walio katika ulimwengu, wanaishi katika maeneo yanayoelekea kupatwa na matetemeko ya ardhi. Tena njia za kufanya mawasiliano ya haraka na uchunguzi wa kisasa wa hali ya juu wa kujua maelekeo ya kutokea kwa matetemeko ya ardhi zimekuwa zikifahamisha watu habari za kuweza kutokea kwa matetemeko ya ardhi kupita nyakati zote zilizotangulia, kufahamisha hata wale ambao hawajajionea wenyewe mtetemo hata mmoja. Kwa sababu hiyo, matetemeko ya ardhi yanakuwa na matokeo juu ya watu wengi zaidi na yanajulikana wazi zaidi na watu wengi zaidi leo kuliko yalivyokuwa zamani. Na wakati watu wanapoona mambo mengine ya ile “ishara” yakitimizwa kati ya kizazi kile kile kimoja, jambo hilo linapasa kuwasukuma wachukue hatua. Kwa njia hiyo, ni nani anayeweza kuwa na kisababu cha kutokutii “ishara ya kuwapo [kwa Yesu] na ya umalizio wa mfumo wa mambo”?

Je! wewe umeona kwamba maafa ya matetemeko ya ardhi juu ya maisha ya kibinadamu yameongezeka tangu mwaka wa 1914? Halafu kujumlisha na jambo hilo, je! wewe umeyaona yale mambo mengine ya ile “ishara,” kama vita, njaa na ukosefu wa kutii sheria ambao umeongezeka? Ikiwa umeyaona, bila shaka wewe unataka kujua habari zaidi juu ya matabiri ambayo Yesu alitoa kuhusu wakati ujao ulio karibu. Mashahidi wa Yehova wanafurahia kukusaidia uyachunguze mambo hayo ya maana.

[Chati katika ukyrasa wa 6]

Orodha ya Kwanza

Mengine ya Matetemeko Yaliyotokea Kati ya 33-70 W.K.

MWAKA MAHALI

33 Yerusalemu

33 Yerusalemu

karibu na 46 Krete

karibu na 50 Filipi

51 Roma

53 Apam æa

60 Laodikia

63 Pompeii

karibu na 67 Yerusalemu

[Chati katika ukurasa wa 7]

Orodha ya Pili

Mengine ya Matetemeko ya Ardhi Yaliyotokea Kati ya 1914 na 1982

(Orodha isiyo kamili)

MWAKA MAHALI VIFO

1915 Avezzano, Italia 29,970

1920 Kansu, China 200,000

1923 Kanto, Japani 142,800

1932 Kansu, China 70,000

1934 Bihar-Nepal, India 10,700

1935 Quetta, Pakistan 60,000

1939 Chillan, Chile 30,000

1939 Erzincan, Uturuki 30,000

1950 Assam, India 20,000

1960 Agadir, Morocco 12,000

1962 Iran ya Kaskazini-magharibi 12,230

1968 Iran ya Kaskazini-mashariki 11,500

1970 Peru ya Kaskazini 66,700

1972 Managua, Nicaragua 10,000

1976 Mji wa Guatemala, Guatemala 23,000

1976 Tangshan, China 800,000

1978 Iran ya Kaskazini-mashariki 25,000

Matetemeko ya ardhi mengine makubwa-makubwa yaliandikwa kuwa yalitokea mahali pengine-pengine 33

[Chati katika ukurasa wa 7]

Orodha ya Tatu

Vifo Kutokana na Matetemeko ya Ardhi

(Kadirio limefanywa kwa kutegemea miaka 1,122)

Kufikia mwaka wa 1914—vifo 1,800 kwa mwaka

Tangu mwaka wa 1914—vifo 25,300 kwa mwaka

[Ramani katika ukurasa wa 5]

(Kwa mpangilio kamili, ona kichapo)

Maeneo ya ulimwengu yenye maelekeo ya kupatwa na matetemeko

AFRIKA

ULAYA

ESIA

MAREKANI KASKAZINI

MAREKANI KUSINI

AUSTRALIA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki