Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 3/15 kur. 3-4
  • Matetemeko ya Ardhi Je! Yanasababishwa na Mungu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matetemeko ya Ardhi Je! Yanasababishwa na Mungu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Matetemeko ya Ardhi Katika Nyakati za Biblia
  • Matetemeko Makubwa ya Ardhi—Biblia Ilitabiri Nini?
    Habari Zaidi
  • Matetemeko ya Ardhi Ni Ishara ya Ule Mwisho?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Matetemeko ya Ardhi, Unabii wa Biblia, na Wewe
    Amkeni!—2002
  • Matetemeko ya Dunia—Taabu Juu ya Taabu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 3/15 kur. 3-4

Matetemeko ya Ardhi Je! Yanasababishwa na Mungu?

‘Udongo ulio imara unakuwa kama uji mwororo wa kuganda chini ya miguu yako. Unachukua hatua tatu au nne kwenda mbele kisha unavutwa nyuma kwa ghafula kama kwamba unatembea katika mkeka wenye kuteleza. Unaanguka chini kisha inakuwa vigumu kuinuka kwa sababu unavutwa kuelekezwa kila upande. Miti inawaya-waya, na matawi ya juu ya miti hiyo yanagusa udongo—wa kwanza chini, halafu mwingine— mingine inakatika kuwa vipande viwili. Wewe unajaribu kuifikia barabara ukimbie; barabara inasonga-songa kama nyoka anayejipinda-pinda mbele yako. Kwenye udongo—kila mahali—unaona nyufa (miatuko) zikifunguka kisha zinajifunga upesi sana. Woga mwingi sana unakukamata. Hakuna mahali pa usalama. Wewe unafikiri kwamba: Ni mwisho wa ulimwengu! ’ ”—Sarah Burn Plunkett, mwokokaji wa tetemeko la ardhi lililotokea Alaska mwaka wa 1964.

WEWE umewahi kupatwa na mtikisiko wa tetemeko la ardhi? Hata kama hujapatwa, matetemeko ya ardhi yanakuwa na matokeo fulani juu ya maisha yako. Namna gani? Kwa njia zisizopungua mbili. Kwanza, yanaonyesha kwamba, hata uwe unaishi wapi, udongo ule ule ulio chini yako uko katika mwendo daima. Pili, tena jambo la maana zaidi, matetemeko ya ardhi ni kiishara cha “mwisho” wa “mfumo wa mambo” ya dunia. Kuhusiana na habari hiyo unabii unaojulikana sana unasema hivi: “Na kutakuwako matetemeko ya ardhi makubwa.” (Luka 21:9-11; Mathayo 24:3-8, NW ) Lakini Biblia ilitabiri kwamba matetemeko ya ardhi ya halisi yangekuwa sehemu ya “ishara” yenye kuonyesha wakati ambao Ufalme wa kimbingu wa Mungu ungemaliza uovu na kuanzisha Paradiso yenye amani duniani. (Zaburi 37:10, 11; Mathayo 6:10) Huenda jambo hilo likaharakisha wengine kuuliza: “Mungu ndiye mwenye kuleta hayo matetemeko ya ardhi? ”

Matetemeko ya Ardhi Katika Nyakati za Biblia

Je! Mungu ndiye anayesababisha matetemeko ya ardhi yote? Kwa ufupi—Hapana! Matetemeko ya ardhi ni kawaida iliyo asili ya dunia, sawasawa na vile upepo na matone ya mvua yalivyo mambo ya kawaida yaliyo asili ya dunia. Mitetemo midogo imekuwa ikifanya mipasuko kupitia duniani muda wa vizazi vingi sana. Kwa wastani, dunia inapatwa na mtetemo mmoja mdogo kila nukta 30.

Katika visa vichache vilivyo wazi matetemeko ya ardhi yameanzishwa na Yehova Mungu. Kwa sababu gani? Matetemeko hayo yalitimiza kusudi fulani la wazi nayo yalileta uharibifu wenye kuchagua—hayakutokea ovyo-ovyo. Fikiria mifano hii:

Karne 24 zilizopita, wakati wa kuanzishwa kwa moja la maagano ya Mungu, watu wa Israeli walikusanyika chini ya Mlima Sinai na “mlima wote ukatetemeka sana.” Kwa njia hiyo Yehova alitumia tetemeko la ardhi kukazia uzito wa agano hilo, huo ukiwa ni mmoja na mawonyesho ya uwezo wake usiolinganika na wa mwingine. Kutetema kwa mlima kulikuwa pia msaada wa kukumbuka kwa Waisraeli. Hawangesahau vyepesi kiapo walichofanya, kwa maana Yehova alikamatanisha mapatano hayo ya maana na matukio ya kutisha sana yaliyotia ndani tetemeko la ardhi.—Kutoka 19:7-19.

Tetemeko jingine lilitukia muda mfupi baadaye. Uasi ulisitawi kati ya jamaa za Dathani, Abiramu na Kora kupinga kiongozi aliyewekwa na Yehova. Mashauri ya kutosha yalipokwisha kutolewa na kupuzwa,Yehova alitumia tetemeko la ardhi kuwaondoa mbali waasi hao watoke kati ya watu wake. “Nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao, na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.”—Hesabu 16:31, 32.

Lakini, Mungu siye amekuwa msababishi wa matetemeko ya ardhi ya kisasa. Basi kwa sababu gani Biblia inayatia ndani kuwa sehemu ya ile ishara ya ule “mwisho”? Na je! kweli sisi tunaishi kwenye “umalizio wa mfumo wa mambo”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki