Uendeshaji wa Wale Wapanda-Farasi Wanne Ni Ishara
Nami nikaona, na, tazama! farasi mweupe, farasi mwenye rangi ya moto, farasi mweusi, farasi wa kijivujivu; na yule aliyemkalia alikuwa na jina Kifo. Na Hadesi alikuwa akimfuata kwa ukaribu.’—UFUNUO 6:2-8, NW.
1. Kabla hajakalia kiti chake kwenye meza ya kiamsha-kinywa tarehe ya Oktoba 2, 1914, msimamizi wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi na Biblia na Trakti alifanya nini kwenye makao makuu huko Brooklyn?
SIKU yenyewe ilikuwa Ijumaa, siku ya pili ya mwezi wa Oktoba wa mwaka wa 1914. Ndipo msimamizi wa Sosaiti alipopiga hatua akaingia katika chumba cha kulia cha wafanya kazi wa makao makuu wa hiyo Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi na Biblia na Trakti, huko 124 Columbia Heights, Brooklyn, New York, U.S.A. Zilibaki dakika chache sana saa moja ya asubuhi ifike. Kabla ya yeye kwenda akaketi kwenye kikao cha kuongozea mazungumzo ya mezani katika chumba cha kulia, alitua. Alipiga makofi ili washiriki wa jamaa ya Betheli walioketi kwenye meza za kulia wamkazie fikira. Halafu, akitumia sauti yenye furaha, akayataja maneno ya utangulizi ya mstari wa 3 wa wimbo unaoitwa “Mfalme Wetu Anapiga Miguu Kusonga Mbele!” yenye kupatikana katika kurasa 162, 163 za kitabu cha nyimbo cha Kiingereza kinachoitwa Hymns of Millennial Dawn. Maneno yenyewe yalisema, “Majira ya Mataifa yamekwisha, kwa maana wafalme wao wamekwisha kuwa na siku yao nayo ikaisha.” Halafu kwanza akakalia kiti chake cha kawaida, ili asimamie kipindi cha kidini cha kila siku kinachohusiana na kiamsha-kinywa cha jamaa ya Betheli.
2. Msimamizi huyo alikuwa ameelekeza fikira za watu kwenye mwaka huo wa maana mapema gani, naye aliruhusiwa aendelee kuishi kwa muda gani katika kipindi hicho cha pigano la ulimwengu?
2 Huko nyuma sana mwaka wa 1876 msimamizi huyo alikuwa amekwisha kuonyesha kwamba mwaka wa 1914 ndio ungekuwa tarehe ya kumalizika kwa “majira ya Mataifa” katika makala aliyotoa ichapishwe katika The Bible Examiner. Alionyesha kwamba mambo mazito yangeupata ulimwengu wote wa wanadamu. (Luka 21:24) Jambo la kushangaza sana ni kwamba, wakati msimamizi alipoitangazia jamaa ya Betheli ya Brooklyn kwamba Majira ya Mataifa yalikuwa yamemalizika, vita ya ulimwengu iliyokuwa ya kwanza katika historia yote ya kibinadamu ilikuwa imefikia siku ya 66 tangu ilipoanza. Kufikia wakati huo maazimio 14 ya vita yalikuwa yamekwisha kufanywa na washiriki wa pigano hilo lililokuwa baya sana. Kabla ya kumalizika kwa tendo hilo la kung’ang’ania utawala wa ulimwengu na masoko ya kibiashara ya ulimwengu, mataifa na falme 29 yalikuwa yamehusika katika pigano hilo la kuogopesha sana. Msimamizi huyo wa Sosaiti, aliyeyasema maneno hayo yenye kufaa, alikufa kabla nchi yake mwenyewe, United States ya Amerika ya Kaskazini, haijahusika katika Vita ya Ulimwengu ya Kwanza katika tarehe ya Aprili 6, 1917 ili iwe mwenzi wa Milki ya Uingereza kwa kusudi la kupambana na zile Serikali Kubwa-Kubwa za Ulaya.
3. Msimamizi alikuwa ameukaziaje umaana wa mwaka wa 1914, naye aliweza kujisikiaje aliposema, “Majira ya Mataifa yamekwisha”?
3 Msimamizi wa Sosaiti alikuwa amerudia kukazia umaana mkubwa sana wa mwaka wa 1914 katika gazeti Mnara wa Mlinzi (Kiingereza) tangu mwaka wa 1879, na hasa katika kitabu The Time Is at Hand, kilichochapishwa mwaka wa 1889. Lakini kufikia Oktoba 2, 1914, yeye alikuwa ameona mambo ya kutosha yaliyotukia katika ulimwengu wa siku hizo katika mwaka huo unaostahili kukumbukwa, akawa na uhakikisho zaidi kwamba maneno aliyoyasema hadharani yalikuwa ya kweli. Aliweza kujisikia akiwa na uwezo wa kutetea maneno yake, angaa katika upande huo, kuonyesha kwamba alikuwa mwanafunzi mwenye makini ya kuchunguza orodha ya tarehe za Biblia inayotabiri nyakati na majira ya Mungu.
4. Msimamizi wa Sosaiti alikuwa ameona mwanzo wa uendeshaji wa nani kabla hajafa, na hiyo ingeweza kuitwa kwa kufaa “ishara” ya nini?
4 Hivyo, kabla ya kifo chake kisichotazamiwa kilichotokea usiku wa Jumanne, Oktoba 31, 1916, msimamizi wa Sosaiti alikuwa ameona mwanzo wa uendeshaji wa wale wapanda-farasi wanne wa kitabu cha Ufunuo tangu mwaka huo ambao Majira ya Mataifa yalikuwa karibu kumalizika kulingana na orodha ya tarehe za Biblia. Ufunuo ndicho kitabu cha mwisho cha Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, ambayo kwa kawaida yanaitwa Agano Jipya. Uendeshaji wa wale wapanda-farasi wanne ni wa maana ulimwenguni pote kwa sababu ni sehemu ya “ishara” fulani inayoonyesha kipindi ambamo jamaa ya kibinadamu imo sasa. Unaonyesha kwamba sisi tumo katika ule ulioitwa na wanafunzi wa Yesu “umalizio wa mfumo wa mambo.” (Mathayo 24:3, NW) Tunaonyeshwa kwamba uendeshaji huo ni “ishara” katika mstari wa kwanza wa Ufunuo, tunaposoma hivi: “Ufunuo kupitia kwa Yesu Kristo, ambao Mungu alimpa, awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo ni lazima yatukie upesi. Naye alimtuma malaika wake akautoa katika ishara kupitia kwake kwa mtumwa wake Yohana.”—Ufunuo 1:1, NW.
5. Tafsiri mbalimbali za Biblia zinatofautianaje katika kuonyesha maneno yaliyotumiwa kutoa maelezo ya vifananishi vya Ufunuo, na kulingana kikweli na utangulizi wa kitabu cha Ufunuo, kitabu chenyewe kimejawa na nini?
5 Uendeshaji wa wale wapanda-farasi wanne umeelezwa katika Ufunuo 6:1-8. Jambo la kupendeza ni kwamba, ijapokuwa Biblia ya New World Translation inasema “akautoa katika ishara” na kwa njia hiyo inalingana na The Emphasised New Testament ya Rotherham, maneno “akautolea maana” ndiyo yanayotumiwa na Biblia ya King James Version, au Authorized Version ya mwaka wa 1611, pia na The Emphatic Diaglott ya B. Wilson na Literal Translation of the Holy Bible ya Young: Kupatana na maneno hayo ya utangulizi, ni kweli kitabu cha mwisho cha Biblia, yaani Ufunuo, kimejawa sana na ishara, vifananishi vyenye maana ya mambo yenye ubora mkubwa zaidi katika historia ya kibinadamu. Mambo hayo yangetukia wakati ujao, “upesi.”
Wale Farasi Wanne na Waendeshaji Wao
6. Ni nani wamewekewa nafasi ya kuingia katika furaha iliyotabiriwa katika Ufunuo 1:3, na namna gani?
6 Hakuna matukio yaliyotokea kuhakikisha kwamba mambo hayo yalitimia wakati wa karne 18 zilizofuata kifo cha mtume Yohana, karibu na mwaka wa 98 W. K., na kwa hiyo, sasa, tunakaza fikira zetu juu ya karne hii ya 20 W.K. Tunapofanya hivyo, tunakuta kwamba jambo lililobaki kwa ajili ya sisi tulio wa karne hii yenye mahangaisho ni kuingia katika furaha ambayo huyo mtume mwenye kuongozwa na Mungu alionyesha ingekuwako, alipoandika hivi: “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” (Ufunuo 1:3) Ili tupate furaha, acheni tuichunguze “ishara” ya wale farasi wanne na waendeshaji wao. Acheni tusome Ufunuo 6:1-8:
7. Ni kitu gani kilichotokea wakati Mwana-Kondoo wa Mungu alipofungua muhuri ya kwanza ya kitabu cha kukunjwa kilichokuwa mkononi mwake?
7 “Kisha nikaona hapo Mwana-Kondoo [Yesu Kristo] alipofungua moja ya zile muhuri saba [za kitabu cha kukunjwa kilichokuwa mkononi mwake], nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate [kumaliza, NW] kushinda.
8. Mtume Yohana aliona nini ilipofunguliwa muhuri ya pili ya kitabu cha kukunjwa?
8 “Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana [mwenye rangi ya moto, NW], na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
9. Yohana aliona na kusikia nini ilipofunguliwa muhuri ya tatu?
9 “Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.
10. Ilipofunguliwa muhuri ya nne, Yohana aliona na kusikia nini katika njozi?
10 “Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu [Hadesi, NW] akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.”
YULE FARASI MWEUPE NA MWENDESHAJI WAKE
11-13. (a) Yule farasi mweupe anafananisha nini, naye mwendeshaji wake anafananisha mtu wa namna gani? (b) Mwendeshaji anayetajwa hapo analingana na mwendeshaji gani anayesemeshwa na mtunga zaburi, na kwenye Waebrania 1:8, 9 Paulo anayatumia maneno hayo ya kiunabii kumhusu nani?
11 Yule farasi mweupe alimaanisha uendeshaji wa kifalme, uchukuaji wa sifa za kifalme, kazi ya maisha yenye uadilifu iliyo na weupe pe, kuwa na wepesi mwingi wa kukimbia kama farasi halisi. Mwendeshaji wa kifaa hicho chenye mwendo wa upesi alifananisha mfalme aliyetawazwa hivi karibuni, kwa maana alipewa taji ya kifalme. Alikuwa mfalme shujaa wa vita, kwa maana alikuwa na silaha ya uta. Tena, alisonga mbele na uendeshaji wake akishinda, mpaka mwishowe mpinzani aliye wa mwisho wa Ufalme wake awekwe chini yake akiwa ameshindwa. Ushindi wake ungekuwa kamili! Kupatana na hilo, yeye alipewa upanga mrefu, chombo cha kifalme cha vita. Basi, je! ni nani amekuwa akitimiza fungu hilo katika karne yetu wenyewe ya 20? Ni wazi kwamba ni yule yule Mfalme anayetimiza Zaburi 45 (NW), tunaposoma hivi:
12 “Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema. Mimi ninasema: ‘Kazi zangu ni kuhusu mfalme fulani.’ . . . Jivike upanga wako juu ya paja lako, Ewe uliye hodari wa nguvu, kwa adhama yako na fahari yako. Na katika fahari yako songa ukapate fanikio; endesha katika kusudi la kweli na unyenyekevu na uadilifu, na mkono wa kuume wako utakufunza wewe katika mambo ya kutia hofu. Mishale yako ni yenye ncha kali—chini yako makundi ya mataifa yanaendelea kuanguka—katika moyo wa maadui wa mfalme. Mungu ndiye kiti chako cha enzi kwa wakati usiojulikana, hata milele; fimbo ya uufalme wako ni fimbo ya unyofu. Wewe umependa uadilifu nawe wachukia uovu. Hiyo ndiyo sababu Mungu, Mungu wako, amekupaka kwa mafuta ya shangwe zaidi ya wenzi wako.”—Mistari 1-7.
13 Katika Waebrania 1:8,9 mtume Paulo anataja maneno ya Zaburi 45:6, 7 na kuyatumia yamhusu Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Basi, ni jambo lisiloepukika kusema kwamba mwendeshaji wa yule farasi mweupe anayeendesha kwa ushindi ni Yesu Kristo wakati wa kutawazwa kwake kwa sherehe katika mbingu, mwishoni mwa Majira ya Mataifa mwaka wa 1914.
14. (a) Ni wakati gani na namna gani Yesu aliendesha akaingia Yerusalemu kama kwamba akatawazwe kwa sherehe, na hilo lilitukia kutimiza unabii gani? (b) Ni babu gani mtukufu ambaye Yesu alimwiga katika uendeshaji wa namna hiyo katika pindi hiyo?
14 Tunaukumbuka wakati ambao Yesu Kristo aliendesha akiwa mfalme-mchaguliwa kama kwamba alikuwa akielekea akatawazwe kwa sherehe kwenye hekalu la Yerusalemu. Wakati huo hakuendesha farasi mweupe mwenye kukimbia sana. Alimwendesha punda, miguu ikiwa upande kwa upande. Tendo hilo lilitimiza unabii wa Zekaria 9:9, unaosema hivi: “Furahi sana, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee binti Yerusalemu; tazama, mfalme wako anakuja kwako; ni mwenye haki, naye ana wokovu; ni mnyenyekevu, amepanda punda, naam, mwana-punda, mtoto wa [punda-mke].” Kupatana na unabii huo, Yesu aliendesha mnyama mwenye amani wakati alipopanda kwa njia ya kutazamisha sana akaingia Yerusalemu siku ya 9 ya mwezi wa Kiyahudi wa Nisani, mwaka wa 33 W.K., ili jambo hilo lilingane na yule mwana-kondoo wa Kupitwa aliyeingizwa ndani ya nyumba za Kiyahudi siku ya Nisani 10 na kuwekwa humo mpaka wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Kupitwa Nisani 14. Kwa kuendesha hivyo Yesu alimwiga Sulemani, babu yake mwenye utukufu, mwana wa Daudi. Wakati Daudi alipojiuzulu katika uufalme wake baada ya kukalia kiti cha enzi cha ufalme wa Israeli muda wa miaka 40, aliagiza Sulemani aendeshe nyumbu-mke ili aelekea kwenye sherehe za kutawazwa. Halafu, Sadoki Kuhani Mkuu alipokwisha kumpaka mafuta awe mrithi wa baba yake, kundi la Waisraeli waliohudhuria lilianza kupiga kelele likisema, “Mfalme Sulemani na aishi!”—1 Wafalme 1:33-40.
15. (a) Yesu aliitikiwaje na watu walio wengi alipoendesha punda kuingia Yerusalemu? (b) Mji wa Yerusalemu ulimpa ukaribishaji wa namna gani, na kwa sababu gani?
15 Sasa, Yesu angepewa ukaribishaji wa namna gani wakati alipoendesha punda siku nne kabla ya sikukuu ya Kupitwa, akautelemka Mlima wa Mizeituni na kuja kwenye mji wa sherehe za kumtawaza? Makundi ya watu yaliyoanza kufuatana naye yaliingiwa na roho ya kipindi hicho wakawa na maoni ya kwamba alikuwa ndiye mfalme wa Israeli wa Kimasihi aliyeahidiwa. Walipunga-punga matawi ya mitende. Walitandika mavazi yao ya nje ili ayapite juu wakati wa uendeshaji wake. “Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la [Yehova]; Hosana juu mbinguni”! (Mathayo 21:1-9) Hivyo ndivyo watu wengi waliitikia. Lakini mji wenyewe wa Yerusalemu ulikuwa chini ya mavutano ya viongozi wa kidini Wayahudi wasioongozwa na utimizo wa unabii huo waliouona ukitimia peupe. Kwa hiyo mji wa Yerusalemu haukumpa yeye ukaribishaji wa kifalme.
16. Wakuu wa hekalu walimtendea Yesu kwa njia gani iliyo tofauti na vile walivyowatendea wafanya biashara?
16 Wakati Yesu alipokwenda hekaluni, Kayafa Kuhani Mkuu hakumpaka mafuta awe mfalme wa Kimasihi asiyetegemea Milki ya Kiroma. Makuhani walikuwa wakiruhusu wafanya biashara watumie maeneo ya hekalu kuendesha biashara yao ya kujipatia faida, lakini Yesu akaonyesha zile sifa zinazomfaa kuhani mkuu kwa kuwaondosha, tena akawakemea wale waliopinga kwa kuwaambia: “Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.” Wayahudi vipofu na viwete walimjia katika hekalu, naye akawaponya. Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walilaumu kitendo hicho, nao wakakataa kumkubali kuwa ndiye “Mwana wa Daudi” na kumtangaza kuwa ndiye mtawala mwenye haki ya kuupata ufalme wa Israeli. Yesu alipowaacha huko hekaluni akaenda zake Bethania, Hakuondoka akiwa amekwisha kutawazwa kuwa mfalme wakati huo.—Mathayo 21:1-17.
17. Pontio Pilato alionyeshaje alitaka kujua habari za dai la Yesu la uufalme, naye aliyatupilia mbali namna gani matakwa ambayo wakuu wa makuhani walidai kuhusu uufalme wa Yesu?
17 Siku nne baadaye, wakati Yesu aliposimama mbele ya Pontio Pilato gavana Mroma, Mtaifa huyo alimwuliza kama yeye alikuwa ni mfalme. Yesu alijibu kwamba Ufalme wake si sehemu ya ulimwengu huu ambao Pilato alikuwa sehemu yao. Kwa kusihiwa na wakuu wa makuhani waliosema, “Sisi hatuna mfalme ila Kaisari,” Pilato alimtoa Yesu akatundikwe Kalvari. Hata hivyo Pilato alishika sana msimamo wake kwa kuweka juu ya kichwa cha Yesu kwenye mti wa kutundikwa kwake ishara yenye kusema: ‘Yesu, Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi.’—Yohana 19:15, 19-22.
18. Ni katika siku gani ya maana Yehova alimwinua Mwanaye kutoka kwa wafu, naye Yesu mfufuliwa aliwaambia wanafunzi wake maneno gani ya kuwaaga kabla hajapaa mbinguni?
18 Lililobaki ni Mungu Mweza Yote, Yehova, kumfufua Mwanaye aliyefia imani awe “mzaliwa wa kwanza wa waliokufa” katika siku ya Nisani 16. Siku iyo hiyo ndiyo Wayahudi walimtolea Yehova mazao ya kwanza ya mavuno ya ngano huko hekaluni. (Ufunuo 1:5) Kwa njia hiyo yeye ambaye angekuwa Mfalme baadaye aliweza kujionyesha wazi kwa wanafunzi wake waaminifu siku hiyo hiyo. Siku 40 baadaye, kabla hajapaa kurudia mbingu, yeye aliwaambia hivi: “Mimi nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote, kuwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu.”—Mathayo 28:18, 19, NW; Mambo ya Walawi 23:10-12; 1 Wakorintho 15:20.
Kumaliza Kushinda Kwake
19. Kwa njia hiyo Yesu aliwezeshwa kutimiza mfano gani wa kiunabii katika wakati uliofaa, naye amekuwa mfalme wa namna gani tangu wakati huo?
19 Hivyo Yesu Kristo aliwezeshwa kutimiza ule mfano wa kiunabii wa kuendesha yule farasi mweupe, kumwendesha akiwa mfalme aliyevikwa taji ili akamalize kushinda maadui wake wote mbinguni na duniani. (Ufunuo 6:1, 2) Tangu mwisho wa “majira ya Mataifa” mwaka wa 1914 W.K. yeye ni Mfalme aliye shujaa wa vita, mwenye silaha ya uta ili awachome maadui zake wakiwa mbali. Kwa uhakika, maneno ya kiunabii yanayofuata ya Zaburi 45:3-8 (NW) yalisemwa kumhusu huyu Mfalme aliye shujaa wa vita:
20. Maneno anayoambiwa na mtunga zaburi yanasema afanye nini?
20 “Jivike upanga wako juu ya paja lako, Ewe uliye hodari wa nguvu, kwa adhama yako na fahari yako. Na katika fahari yako songa ukapate fanikio; endesha katika kusudi la kweli na unyenyekevu na uadilifu, na mkono wa kuume wako utakufunza wewe katika mambo ya kutia hofu. Mishale yako ni yenye ncha kali—chini yako makundi ya mataifa yanaendelea kuanguka—katika moyo wa maadui wa mfalme. Mungu ndiye kiti chako cha enzi kwa wakati usiojulikana, hata milele; fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya unyofu. Wewe umependa uadilifu nawe wachukia uovu. Hiyo ndiyo sababu Mungu, Mungu wako, amekupaka kwa mafuta ya shangwe zaidi ya wenzi wako. Mavazi yako yote ni manemane na uudi na mdalasini; vyombo vya muziki vyenye nyuzi vimesikika kutoka lile jumba la kifalme lililo bora sana lenye vifaa vya pembe, vikakufanya uwe na shangwe.”
21. (a) Tunaweza kuwaje na uhakika kwamba maneno ya mtunga zaburi yanamhusu Yesu Kristo aliyetukuzwa? (b) Usahihi wa kulenga shabaha ya maadui wake unakaziwaje kwenye Zaburi 45:5?
21 Kwenye Waebrania 1:8, 9 mtume Paulo anataja maneno ya Zaburi 45:3-8 na kuyatumia kumhusu Yesu Kristo, ili kuonyesha kwamba sasa yeye ana cheo cha kutukuzwa sana. Hiyo inahakikisha kwamba “mfalme” ambaye “wana wa Kora” waliongozwa na Mungu wamtolee maelezo yao ni yule Mfalme Yesu Kristo aliyetawazwa kwa haki. (Ona maelezo ya juu yaliyo utangulizi wa Zaburi 45, NW.) Mishale inayotoka kwenye “upinde” wake itaelekezwa kwenye moyo wa wapinzani wa Ufalme wake. Mishale hiyo itailenga shabaha kwa usahihi mkubwa kuliko ule waliokuwa nao Waparthia wa kale, waliokuwa wapiga upinde wastadi hata wakiwa wamepanda farasi.
22. (a) Ni katika sehemu gani nyingine ya Ufunuo mwendeshaji huyu wa farasi mweupe anapoonyeshwa, na hapo anaitwa nani? (b) Macho yetu yamebarikiwaje kwa kuweza kuona njozi? Hiyo ni njozi gani, nasi tunatendaje tunapoiona?
22 Mwendeshaji wa farasi mweupe anayeelezwa kwenye Ufunuo 6:2 ni yule yule mwendeshaji wa farasi mweupe anayeonyeshwa kwenye Ufunuo 19:11-16. Katika mtajo huu wa pili jina lake ni “Neno la Mungu,” na katika paja lake amejivika mtajo unaomwita ‘Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.’ Hapo anaonyeshwa akiwa kwenye upeo wa kufuatia wapinzani wake, wakati anapofikisha uendeshaji wake kwenye ushindi wa mwisho katika “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” katika uwanja wa Har–Magedoni, au Mlima wa Megido. (Ufunuo 16:14-16; 19:17-21) Ndipo Shetani Ibilisi na mashetani wake wanapofungwa kwa miaka elfu moja ya kuzuiwa katika shimo lisilo na mwisho. Jambo hilo linatukia bila kuonwa na macho ya kibinadamu. (Ufunuo 20:1-3) Yenye baraka ni macho yetu kwa kuweza kuuona kupitia imani ule uendeshaji wa Mfalme aliyevikwa taji ambaye amempanda “farasi mweupe” tangu mwisho wa Majira ya Mataifa mwaka wa 1914. Kwa sababu ya kusisimuliwa sana ndani ya nafsi zetu na ushindi mbalimbali alioupata kufikia sasa, sisi tunapa-a-za sauti tukisema, ‘Ewe mwendeshaji wa kifalme uliye juu ya farasi mweupe, zidi kuendesha ukajipatie ushindi unaopita wa wengine wote huko Har–Magedoni. Fanya hivyo uondolee malawama enzi kuu ya ulimwengu wote ya Yehova Mungu, Mpaji wa “ishara” hii ya kiunabii.’
Wewe Ungejibuje Maulizo Yanayofuata:
□ Wapanda-farasi walianza uendeshaji wao wakati gani?
□ Ni tazamio gani lililotimizwa wakati huo?
□ Mwendeshaji wa kwanza alifanya uendeshaji gani wa utangulizi, naye alipokewaje?
□ Maandiko ya Ufunuo 6:1, 2; 19:11-16 na Zaburi 45:3-8 yanaonyeshaje kusudi la uendeshaji wa baadaye wa mwendeshaji huyo?