Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 10/1 kur. 3-4
  • 1914—Ulibadili Maisha Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • 1914—Ulibadili Maisha Yako
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Matokeo Yake Yangali Yanaonekana
  • Makosa Yaliyoanzisha Vita vya Ulimwengu
    Amkeni!—2009
  • ‘Mabadiliko Makubwa Zaidi’
    Amkeni!—1999
  • Vita Ambayo Itavimaliza Vita
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Vita ya Ulimwengu ya Kwanza na Mwanzo wa Huzuni Mbalimbali
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 10/1 kur. 3-4

1914​—Ulibadili Maisha Yako

KARIBU miaka 70 iliyopita, siku ya Jumatatu asubuhi, Juni 29, 1914, magazeti yalikuwa na kichwa kikubwa chenye kushtua: “MRITHI WA KITI CHA UFALME CHA AUSTRIA ACHINJWA.” Labda kisehemu hicho cha habari kinaonekana kuwa cha kale sana kwako sasa​—kama kwamba ni jambo fulani la historia ya kale. Hata hivyo, kiligutua wale waliokuwa hai wakati huo. Na kilianzisha mfululizo wa matukio ambayo yangali yanakuhusu wewe.

Na zaidi, matukio hayo yalikuwa ushuhuda wa matukio mengine ya maana zaidi ambayo karibuni yatahusu maisha yako kwa njia kubwa sana hakika. Ebu tuone jinsi hayo yote yalivyo.

Matokeo Yake Yangali Yanaonekana

Kwanza, maisha yako leo, katika miaka hii ya 1980, yanapatwaje na matokeo ya uuaji huo wa wakati mrefu uliopita? Hilo ndilo tukio lililoanzisha vita ya ulimwengu ya kwanza. Vita hiyo, pamoja na mapatano ya amani yaliyofuata, yaliutokeza ulimwengu tunaojua sasa.

Kabla ya vita hiyo, ulimwengu ulikuwa umetawalwa na milki, nyingi za milki hizo zikiwa zimesimamishwa na mamlaka za Ulaya zenye nguvu. Vita hiyo ilitokeza kuvunjika-vunjika kwa milki hizo, na leo uimara wa ulimwengu hauko mikononi mwa nchi chache za Ulaya zenye nguvu nyingi. Badala yake tunaona jambo ambalo linahatirisha uhai wa wanadamu: shindano lenye kusonga mbele la kushindania utawala kati ya mamlaka kubwa sana mbili, Urusi ya kikomunisti na Amerika ya kibepari. Pia, chanzo cha hali hiyo ni vita ya ulimwengu ya kwanza.

Kabla ya vita hiyo, Urusi ilikuwa nchi kubwa, isiyo na maendeleo, yenye kusimamiwa na Kanisa la Orthodoksi la Urusi na kutawalwa na czar. Amerika, ingawa ilikuwa yenye nguvu, kwa vyo vyote haikuonwa kuwa yenye nguvu zenye kulingana na zile za mamlaka za Ulaya. Vita ya ulimwengu ya kwanza ilibadili hayo yote. Kulingana na mwanahistoria René Albrecht-Carrié, “vita [ya ulimwengu ya kwanza] ndipo Amerika ikakomaa kuweza kuingia katika jumuiya ya nchi zenye kujitawala.” Yeye anaongeza hivi: “Nguvu za United States mwishoni mwa vita hiyo kwa njia zote zilishinda zile za nyinginezo zote kabisa kabisa.” Utajiri mwingi wa Amerika, kwa kulinganisha na kuishiwa kiuchumi kwa mamlaka za Ulaya, ulitokeza mamlaka yake ya sasa juu ya ulimwengu.

Katika Urusi, mitetemeko ya maasi ilikuwa imesikiwa kabla ya vita. Wakati wa vita hiyo Urusi ilijitupa uwanjani kupigana na Ujeremani, kwa hiyo Ujeremani ikampeleka mwanamapinduzi Mrusi, Lenin, kutoka uhamisho wake katika Uswisi mpaka nchi ya kwao, wakitumaini kuongeza mchafuko uliokuwamo ndani ya nchi hiyo. Mbinu hiyo ilifaulu, na Urusi ikajiondoa vitani. Chama cha Lenin, Wabolsheviki, kikachukua usimamizi wa mapinduzi ya Urusi, na matokeo ya moja kwa moja ya tukio hilo ni Urusi tunayoiona leo.

Kujapokuwa kushindana kati ya mamlaka zenye nguvu zaidi, leo kuna mchafuko na ukosefu wa imara usiopata kuonekana tena kati na ndani ya mataifa. Hiyo pia ni sehemu ya ambacho mwanahistoria Charles L. Mee, Jr., anaita “urithi wenye mchanganyiko mbaya sana” wa vita ya ulimwengu ya kwanza na mkataba wa amani uliofuata. Ikiwa ni sehemu ya urithi huo, yeye anataja “kuinuka kwa Hitler, Vita ya Ulimwengu ya Pili, maasi na mapinduzi yanayoukumba ulimwengu usio na utaratibu wa kisiasa.” Ungali unasoma juu ya umwagaji wa damu na mateso katika magazeti yako ya asubuhi. Na kumbuka, vita ya ulimwengu ya pili ilichochea uundaji wa makombora ya nyukilia, ambayo yanahatirisha kuwapo kwenyewe kwa uhai duniani.

Lakini, mwandikaji Mee anaongeza hivi, “wakati uo huo, kuanguka kwa utaratibu wa kale kulikuwa utangulizi wa lazima ili kujitawala kuenee, kukombolewa kwa mataifa mapya na tabaka za kijamii, kutokezwa kwa uhuru na kujitegemea kwa njia mpya.” Kabla ya 1914, mataifa mengi yalikuwa yakitawalwa na jamii ya wakuu wa kurithi wenye pendeleo. Kulikuwa hakuna kuchangamana kwa tabaka mbalimbali za kijamii. Vita ya ulimwengu ya kwanza iliharakisha kuvunjika kwa mfumo huo. Ni kama mwanahistoria René Albrecht-Carrié anavyosema: “Vita ya Ulimwengu ya Kwanza ndiyo iliyovunja ukuta wa kutofautisha tabaka mbalimbali za kijamii wa karne ya kumi na tisa; madai ya Mtu wa Kawaida kutaka atambuliwe hayangeweza kukataliwa.” Leo, ni vigumu kuwazia uwezo ambao tabaka za jamii zenye kutawala za kale zilikuwa nao wakati mmoja.

Ndiyo, ulimwengu tunaojua sasa ulianza kufanyizwa wakati risasi ile ya muuaji ilipomchinja mrithi wa kiti cha ufalme wa Austria miaka 70 iliyopita. Maisha yako yangekuwa tofauti sana kama msiba huo, na vita ambayo ulitokeza, havingetokea kamwe. Lakini mambo mengine yalikuwa yakitokea wakati wa miaka ya mapema ya karne hii. Watu wengi hawakujua hata kidogo juu ya umaana wayo. Na mambo hayo yana matokeo makubwa sana juu ya maisha yako.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Mtawala mkuu Ferdinand na mkeye, dakika tano kabla ya kuchinjwa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki