Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 2/15 kur. 8-9
  • Katika Sinagogi la Mji wa Kwao

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Katika Sinagogi la Mji wa Kwao
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Akiwa Katika Sinagogi la Mji wa Kwao
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Katika Sinagogi Huko Nazareti
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Miujiza Ambayo Yesu Alifanya Katika Mji Alimokaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Nazareti—Makao ya Nabii
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 2/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Katika Sinagogi la Mji wa Kwao

WAKATI Yesu anaporudi nyumbani, tunaweza kuwazia msisimuko unaotokea Nazareti. Kabla hajaondoka kwenda kubatizwa na Yohana muda unaozidi kidogo mwaka mmoja, Yesu alijulikana kuwa seremala. Lakini sasa amejulikana sana kuwa mfanya miujiza. Wakaaji wa Nazareti wanataka sana kumwona akifanya baadhi ya maajabu hayo kati yao.

Matazamio yao yanaongezeka wakati Yesu anapoenda kwenye sinagogi la huko kwao kulingana na desturi yake. Wakati wa ibada zinazoendelea humo, yeye anasimama asome, naye anapewa kitabu cha kukunjwa cha nabii Isaya. Anakunjua mahali panaposema juu ya Yule aliyepakwa mafuta kwa roho ya Yehova, ambapo katika Biblia zetu leo ni sura ya 61.

Akiisha kusoma juu ya jinsi Huyu angehubiria mateka kufunguliwa kwao, vipofu kufumbuliwa macho, na juu ya mwaka uliokubalika wa Yehova, Yesu anamrudishia mtumishi kitabu cha kukunja kisha anaketi. Wote wamemkazia macho. Halafu anasema nao, labda kwa muda mrefu kidogo, akieleza hivi: “Leo andiko hili ambalo mmesikia sasa hivi limetimizwa.”

Watu wanastaajabia maneno yake ya kuvutia na kusemezana hivi: “Huyu ni mmoja wa wana wa Yusufu, sivyo?” Lakini yeye akijua kwamba wanataka kumwona akifanya miujiza, Yesu anaendelea kusema: “Hakuna shaka mtautumia mfano huu kunihusu mimi, ‘Tabibu, jiponye mwenyewe; mambo tuliyosikia kuwa yalitukia katika Kapernaumu yafanye hapa pia katika eneo la nyumbani kwenu.’” Kwa wazi, watu hawa waliokuwa jirani za Yesu hapo kwanza, wanaona kwamba mtu anapaswa kuanzia nyumbani maponyo anayofanya, kwa faida ya watu wake mwenyewe kwanza. Kwa hiyo wanaona wamepuuzwa na Yesu.

Kwa kutambua kuwaza kwao, Yesu anasimulia historia fulani yenye matumizi yanayofaa. Anasema walikuwako wajane wengi katika Israeli siku za Eliya lakini Eliya hakutumwa kwa ye yote kati yao. Bali, alienda kwa mjane asiye Mwisraeli katika Sidoni, ambako alifanya muujiza wenye kuokoa uhai. Na katika siku za Elisha, walikuwako wenye ukoma wengi, lakini Elisha alisafisha Naamani wa Shamu (Siria) peke yake.

Kwa kukasirishwa na ulinganisho huo wa kihistoria wenye sifa mbaya unaofunua uchoyo wao na ukosefu wa imani, wale walio katika sinagogi wanainuka na kumsukumiza Yesu nje ya mji. Huko, kwenye ukingo wa mlima ambao mji wa Nazareti umejengwa juu yao, wanajaribu kumtupa akaanguke chini. Lakini Yesu anawaponyoka na kwenda zake akiwa salama. Luka 4:16-30, NW; 1 Wafalme 17:8-16; 2 Wafalme 5:8-14.

◆ Kwa sababu gani kuna msisimuko mwingi Nazareti?

◆ Watu wanafikiri nini juu ya hotuba ya Yesu, lakini ni jambo gani linalowakasirisha sana?

◆ Watu wanajaribu kumtendaje Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki