Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 3/1 uku. 3
  • Je! Wewe Unauacha Ukweli Ukuponyoke?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wewe Unauacha Ukweli Ukuponyoke?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Pontio Pilato Alikuwa Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Kutoka kwa Pilato Mpaka kwa Herode na Kurudi Tena
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutoka kwa Pilato Mpaka kwa Herode na Kurudi Tena
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Pilato na Herode Wakosa Kumpata na Hatia
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 3/1 uku. 3

Je! Wewe Unauacha Ukweli Ukuponyoke?

WALIPOKWISHA kuokoka baada ya kulazimika kutusha helikopta yao chini katika pori la Amazoni, abiria walio wengi hawakutaka sana kuyafikiria mazingira ya kipande hicho cha ardhi. Lakini mwanamume mmoja asiyepoteza utulivu wake na mwenye kuwa macho daima alikuwa tofauti! Yeye alikuwa mchunguzi wa ardhi na migodi (mjiolojia), na aliona kwamba kisehemu ambacho helikopta ilitulia kilikuwa na utupu usio wa kawaida. Badala ya kuacha nafasi hiyo ipite, aliitazama kwa makini zaidi sehemu hiyo isiyo na mmea. Baada ya muda mfupi akatambua kwamba kile kilichoelekea kwa wengine kuwa ni kipande cha kawaida tu cha ardhi kwa kweli kilikuwa moja la maeneo yanayoweza kutokeza madini za namna nyingi sana​—ghala kubwa sana la chuma, bokzaiti, manganisi, shaba, na dhahabu ambayo siku moja lingeshangiliwa kuwa mahali papya pa utajiri wa ajabu.

Ni watu wachache sana wanaozitumia kwa faida nzuri nafasi wanazopata, badala ya kuziacha ziwaponyoke. Kwa mfano, fikiria gavana Mroma Pontio Pilato wa huko nyuma katika karne ya kwanza ya Wakati wa Kawaida wetu. Nafasi bora ajabu iliwekwa mbele yake. Viongozi wa Kiyahudi walimletea mwalimu aliye mkuu zaidi wa ukweli aliyepata kuishi duniani, Yesu Kristo. Ebu wazia ni maulizo mengi kadiri gani ambayo Pilato angaliweza kuuliza! Ebu wazia kweli bora ambazo angaliweza kujifunza! Na jambo la kupendeza ni kwamba, wakati walipomleta Yesu mbele yake mara ya kwanza, wakimshtaki juu ya kudai kuwa ni “mfalme wa Wayahudi,” angalau Pilato alielekea kuwa mdadisi:

“Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Pilato akauliza.

Kwa kujibu, Yesu alisema: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu . . . Kwa hilo mimi nimezaliwa, na kwa hilo mimi nimekuja ndani ya ulimwengu, kwamba niutolee ukweli ushuhuda. Kila mtu aliye upande wa ukweli anasikiliza sauti yangu.” Hapo ikajitokeza nafasi iliyo nzuri kabisa ya Pilato. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamume ambaye maisha yake yalikuwa ushuhuda ulio hai kwa ukweli wa ahadi za Mungu, mtu mwenye nia na uwezo wa kumpa nuru ya ufahamu kuliko mtu mwingineye yote. Hata hivyo Pilato alijibuje? “Ukweli ni nini?” Kisha akafanya haraka nyingi ‘kwenda nje awarudie Wayahudi.’​—Yohana 18:33-38, NW.

Ndiyo, Pilato aliacha ukweli umponyoke. Na watu wengi leo wanafanya kosa ilo hilo. Jarida unalosoma sasa hivi, Mnara wa Mlinzi, linachapishwa ili kutolea watu nuru ya ukweli. Ingawa hivyo, watu wengi wanakataa hata kulisoma. Wengine wanazisoma na kuzifurahia makala, na mambo yanaishia hapo. Je, ingeweza kuwa kwamba watu hao wanauacha ukweli uwaponyoke kama Pilato?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki