Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 8/15 kur. 24-25
  • Kutimiza Unabii wa Isaya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutimiza Unabii wa Isaya
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Kutimiza Unabii wa Isaya
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Atimiza Unabii wa Isaya
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je, Ungeuzima Utambi Ufukao Moshi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • “Mteule Wangu, Ambaye Nafsi Yangu Imependezwa Naye”!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 8/15 kur. 24-25

Maisha na Huduma ya Yesu

Kutimiza Unabii wa Isaya

BAADA ya Yesu kupata habari kwamba Mafarisayo na wafuasi wa chama cha Herode wanapanga kumwua, yeye na wafuasi wake wanajitenga mbali kwa kwenda kwenye Bahari ya Galilayo. Wakiwa kule makutano makubwa ya watu kutoka sehemu zote za Palestina, na hata kutoka nje ya mipaka yake, wanammiminikia. Yeye anaponya wengi, na matokeo ni kwamba wote wenye magonjwa ya kuhuzunisha sana wanajisukuma mbele wamguze.

Kwa sababu makutano ya watu hao ni makubwa sana, Yesu anawaambia wanafunzi wake wamwekee mashua pale aendelee kuitumia. Kwa kuiendesha na kutoka ufuoni, anaweza kuyazuia makutano ya watu hao wasimsonge. Anaweza kuwafundisha akiwa mashuani au kusafiri kwenye eneo jingine kandokando ya ufuo wa bahari ili kuwasaidia watu kule.

Mwanafunzi Mathayo anaandika kwamba utendaji wa Yesu unatimiza “neno lililonenwa na nabii Isaya.” Halafu Mathayo anataja maneno ya unabii ambao Yesu anatimiza, yaani:

“Tazama, mtumishi wangu niliyemteua; mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye; nitatia roho yangu juu yake, naye atawatangazia Mataifa hukumu. Hatateta wala hatapaza sauti yake; wala mtu hatasikia sauti yake njiani. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima, hata ailetapo hukumu ikashinda. Na jina lake Mataifa watalitumainia.”

Bila shaka, Yesu ndiye mtumishi mpendwa ambaye Mungu anakubali. Na Yesu anafahamisha wazi ni nini haki ya kweli, ambayo mapokeo ya dini ya uwongo yanaifunika isionekane. Mafarisayo hawataki hata kwenda kusaidia mgonjwa siku ya Sabato kwa sababu wanatumia sheria ya Mungu visivyo haki! Kwa hiyo, kwa kufahamisha wazi haki ya Mungu ni nini, Yesu anawaondolea watu mzigo wa mapokeo yasiyo ya haki, na kwa sababu hiyo viongozi wa kidini wanajaribu kumwua.

Maana yake nini kwamba ‘hatateta wala hatapaza sauti yake’ katika njia pana? Ni kwamba, wakati anapoponya watu, Yesu ‘amewakataza sana wasimdhirishe.’ Yeye hataki kujitangaza kwa makelele mengi katika barabara wala hataki habari za msisimuko zipitizwe kutoka kinywa kimoja mpaka kinywa kingine na kupotoshwa.

Pia, Yesu anawapelekea ujumbe wenye faraja watu ambao kwa njia ya mfano ni kama mwanzi uliopondwa, uliokunjika na kugongwa katika sehemu ya chini. Wao ni kama utambi utokao moshi, ambao mwali wao wa mwisho karibu uzimwe. Yesu hauvunji mwanzi uliopondeka wala hauzimi utambi utokao moshi. Bali kwa wororo na upendo anawainua wapole kwa ustadi. Kwa kweli, Yesu ndiye ambaye mataifa wanaweza kutumainia! Mathayo 12:15-21; Marko 3:7-12; Isaya 42:1-4.

◆ Yesu anafahamishaje wazi maana ya haki, bila kuteta wala kupaza sauti katika njia pana?

◆ Ni nani walio kama mwanzi uliopondeka na utambi, na Yesu anawatendeaje?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki