Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 12/15 uku. 27
  • Unajimu Katika Masinagogi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unajimu Katika Masinagogi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Maisha Yako Yaongozwe na Unajimu?
    Amkeni!—2000
  • Je, Unajimu Unaweza Kukufunulia Wakati Ujao?
    Amkeni!—2005
  • Je, Maisha Yako Yanaongozwa na Nyota?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Je, Mungu Hukubali Kila Namna ya Ibada?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 12/15 uku. 27

Unajimu Katika Masinagogi?

Jarida Biblical Archaeology Review la Mei/Juni 1984 liliripoti uvumbuzi wa vigae vyenye rangi mbalimbali wakati wa uchimbuzi mahali pa sinagogi la kale. Liko mahali panapojulikana kama Hammath Tiberias, ukingoni mwa Bahari ya Galilaya. Kipimo cha uchimbuzi huo kimewekewa tarehe isiyo dhahiri kuwa kama kati ya karne ya pili na tano W. K. Kama makala hiyo inavyosema: “Wanachuo wana mawazo yanayotofautiana sana sana kuhusu tarehe za masinagogi hayo ya kale.”

Lakini ni jambo gani linalofanya vigae hivyo vyenye rangi mbalimbali visiwe vya kawaida? Vilikuwa na mungu wa Kigiriki Helios [mungu jua] akizungukwa na ukanda. . . . Ishara za miezi 12 zimeandikwa katika ukanda kuzunguka duara ya Helios.” Baada ya kuzungumzia ulizo la kama kazi hiyo ilitekelezwa na Myahudi au mtu asiye Myahudi, makala hiyo inasema: “Walakini, tatizo kubwa zaidi ni, Ukanda na mungu Mgiriki unafanya nini katika sinagogi? . . . Tatizo hilo linakuwa gumu kwa sababu ya kwamba ukanda huo na Helios vinakuwa kichwa kinachorudiwa-rudiwa katika masinagogi kadha ya kale, ambayo Hammath Tiberias pekee ndipo pa kale zaidi.”

Lakini je! huo ungekuwa ndio wakati wa kwanza ambao Wayahudi wa nyakati za kale walikuwa wamechanganya mifano ya kipagani na miungu pamoja na ibada yao? La, kwa kuwa Biblia inaonyesha kwamba kufikia wakati wa mfalme Manase (716-661 K.W.K.), unajimu ulikuwa tayari umeingia kisiri katika ibada ya Wayahudi. Masimulizi ya Biblia yanatuambia hivi: “Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera, kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Isaeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.”​—2 Wafalme 21:3.

Baadaye, Mfalme Yosia, mtengenezaji mwenye bidii, aliondoa mazoea hayo ya uwongo. “Kisha, mfalme akamwamuru Hilkia, kuhani mkuu, na makuhani wa daraja la pili, na walinzi wa mlango, kwamba watoe katika hekalu la [Yehova] vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali, na kwa ajili ya Ashera, na kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni; akavipiga moto nje ya Yerusalemu, katika mashamba ya Kidroni, akayachukua majivu yake mpaka Betheli. Akawaondosha wale makuhani walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.”​—2 Wafalme 23:4, 5.

Ni masomo gani yanayofundishwa na matukio hayo ya kihistoria? Jambo la kwanza ni kwamba, hakuna nafasi kwa unajimu, maaguzi kwa kutazama nyota, na mazoea mengine ya kuwasiliana na ulimwengu wa roho katika ibada ya Mungu wa kweli, Yehova. Jambo la pili ni kwamba, ni rahisi sana kujiingiza katika mazoea hayo ikiwa mtu anaacha uhusiano wake pamoja na Yehova na kusikiliza falsafa ya mwanadamu na inayoitwa hekima ati. Kisha inakuwa rahisi ‘kusujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba.’ Kizuizi cha mazoea ya namna hiyo ni ‘kumshika Mungu katika maarifa sahihi,’ kwa kweli ni kumjua Bwana Mwenye Enzi Kuu ya ulimwenguni pote, Yehova, na Mwanaye, Kristo Yesu.​—Warumi 1:20-25, 28; Yohana 17:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki