Mchawi Mwenye Wake Wengi Apata Ukweli
MWANAMUME mmoja Mwafrika anayeitwa Isaka, pamoja na wanaume kadha wengine, alijiondoa katika Kanisa Apostoli la kijiji chao kwa sababu halikuzoea mambo liliyohubiri. Baadaye wenye kanisa hilo walihama kisha wote kutia ndani wake zao, wakawa Mashahidi wa Yehova isipokuwa Isaka. Wao waliamua kumtembelea kumwambia walikuwa wameupata ukweli. Kwa sasa, Isaka alikuwa amekuwa mchawi mwenye mafanikio na akawa ana wake kadha Baada ya kujifunza ile broshua Furahia Milele Maisha Duniani! yenye kushughulika na mtindo wake wa maisha, Isaka aliacha zoea lake la uchawi lililokuwa likimletea pesa nyingi. Aliwaacha wake zake pia isipokuwa yule mkubwa. Yeye alihalalisha ndoa yake pamoja na mke wake mkubwa, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 63 (naye miaka 68). Anasema anahisi akiwa “mwenye furaha sana na huru, bila kuwaogopa tena pepo.”