Wanafanya Kazi Ingawa Wamepigwa Marufuku
Ingawa katika nchi fulani za Afrika waganga wamepigwa marufuku, watu wengi wanawaendea wanapokuwa na magonjwa badala ya kwenda kutibiwa na madaktari wa kisasa. Inasemekana kwamba katika nchi moja ya Afrika ambako waganga wamepigwa marufuku, wao wana shughuli nyingi sana kufikia kiasi cha kwamba hata wachezaji-mpira wanakataa kucheza mpaka kwanza mganga alaani timu (kikoa) ile nyingine. Hivi majuzi madaktari wawili Wajeremani walitembelea nchi hiyo wakapiga picha ya sinema kuhusu upasuaji wa ubongo uliofanywa na mganga bila kumtia mgonjwa katika hali ya kutokuona maumivu.
Kivulana mdogo alikuwa na maumivu makali baada ya kupigwa kichwani, basi ubongo wake ukawa na mkazo. Alishikiliwa chini na wanaume watano huku mganga akitumia saa tano kutoboa shimo kichwani mwake kwa kitu chenye ncha kali. Baadaye, mafuta yalimiminwa juu ya jeraha lenyewe kisha akafungwa kichwa kwa vitambaa. Jambo la kustaajabisha ni kwamba kivulana aliinuka na kwenda zake nyumbani.
Lakini waganga na wachawi wanatoa wapi uwezo wao? Biblia inaonyesha waziwazi ni kutokana na mashetani, roho waovu, na kwa hiyo “mtu ye yote anayewaendea” watu wa namna hiyo anaonwa na Mungu kuwa ‘wa kuchukiza sana.’—Kumbukumbu la Torati 18:9-12, NW.