Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 7/15 uku. 3
  • Imani Inaweza Kuondosha Milima!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Imani Inaweza Kuondosha Milima!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Imani Ni Nini?
  • Imani Inaweza Kuondosha Milima!
  • Imani—Sifa Inayotuimarisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Onyesha Imani Yako Katika Ahadi za Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
  • Ubora Uliojaribiwa wa Imani Waleta Uvumilivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Imani ya Kweli—Ni Nini?
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 7/15 uku. 3

Imani Inaweza Kuondosha Milima!

UMATI huo ulikuwa katika hali ya kungojea kwa wasiwasi. Baba mmoja alikuwa ndipo tu amemleta mwanaye mwenye ugonjwa wa kifafa kwa wanaume waliofikiriwa kuwa na uwezo wa kumponya. Ponyo lilingojewa kwa shauku nyingi. Lakini hakuna kitu kilichotokea! Kwa kukatishwa tumaini, yule baba akageuka aende zake.

Wakati uo huo wanaume wengine wanne wakatokea, na miongoni mwao kiongozi wao, Yesu wa Nazareti. Akikimbia kumwelekea, yule baba akasihi: “Umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya.“

“Mleteni huku kwangu,“ akasema Yesu. Matokeo yakawaje? “Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.“ Ndiyo, muujiza mwingine! Lakini ni kwa sababu gani wanafunzi wa Yesu walikuwa wameshindwa?

Yesu alieleza sababu, akisema: “Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu.“ Kisha akaendelea: “Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.“—Mathayo 17:14-20.

Kutokana na jambo hili lililoonwa maishani, ni wazi kwamba imani ina nguvu nyingi. Lakini imani ni nini hasa? Je! inaweza kujengwa na kutiwa nguvu? Jel inaweza kweli kuondosha milima?

Imani Ni Nini?

Mtume Paulo alieleza imani kuwa “taraja lililohakikishwa la mambo yanayotumainiwa, wonyesho dhahiri [au, ushahidi wenye kusadikisha] wa mambo hakika ijapokuwa hayaonwi.“ (Waebrania 11:1, NW) Kwa maneno mengine, imani ni ushahidi wenye kusadikisha wa jambo lisiloonwa. Haitegemei mambo yaliyosikiwa tu bali ina msingi imara. Hivyo, imani inatofautiana na imani juu ya mambo bila msingi. Kamusi moja inafasili imani juu ya mambo bila msingi kuwa “itikadi au utayari wa itikadi, [hasa] juu ya ushahidi mdogo au usio na hakika.“ Tofauti kabisa, mtu aliye na imani ya kweli ana ushahidi thabiti kwa yale anayoamini. Basi, yeye anaweza kukuambia ni kwa sababu gani yeye anasadikishwa kwamba jambo fulani litakuja kutukia. Yule baba aliyetajwa mwanzoni alikuwa na ushahidi fulani uliomsadikisha kwamba Yesu angeweza kuponya mwanaye. Ushahidi gani? Basi, Yesu alikuwa amekuwa akifanya miujiza kwa zaidi ya miaka miwili, na sifa yake ilikuwa imeenea karibu sehemu zote za Palestina.​—Luka 7:17; Yohana 10:25..

Imani imeelezwa pia kuwa “hati ya umilikaji ya mambo yanayotumainiwa.“ Mtu anayenunua mali iliyo mbali na ana hati ya umilikaji mkononi mwake ana ushahidi wenye kusadikisha kwamba mali ile ipo na kwamba kwa kweli ni yake, hata ingawa huenda akawa hajapata kamwe kuiona. Ndivyo, pia, na mtu aliye na imani anaweza kutokeza ushahidi dhahiri kwa yale anayoamini. Kwa mfano, tuseme yeye ana imani kwamba Yehova Mungu ataleta amani ya kweli kwenye dunia hii kupitia Ufalme.​—1 Petro 3:15.

Imani Inaweza Kuondosha Milima!

Hata hivyo, huenda mtu fulani akauliza, ‵Je! Yesu alimaanisha kwamba imani kama hiyo ingeweza kihalisi kuhamisha milima?ʼ Huenda Yesu akawa alitia hilo ndani, lakini mara nyingi yeye alitumia mifano. (Mathayo 13:34) Kwa hiyo pengine yeye alifikiria vizuizi ambavyo vingeweza kuwa kama milima kwa mwamini. Kwa kweli, mara nyingi neno “mlima“ linatumiwa kumaanisha kiasi kikubwa, kama vile “mlima wa madeni.“ Uhakika wa kwamba imani ya kweli inaweza kuhamisha au kuondosha vizuizi mfano wa mlima unathibitishwa na mambo mengi yaliyoonwa na watu wa kisasa.

Kwa mfano, je! wewe hungekubali kwamba mtu kuwa amepooza kutoka shingoni kwenda chini ungekuwa mlima kweli kweli? Hata hivyo, mtu aliyepooza miguu na mikono yote anayeishi katika Vancouver, B.C., Kanada, si kwamba amejifunza kupaka rangi tu, kwa kutumia brashi au kisu cha kuchanganya rangi

akikishika mdomoni mwake, bali pia anajiruzuku mwenyewe kwa kuuza michoro yake. Tena, imani yake inamsukuma awaambie wengine juu ya yale ambayo amejifunza kutoka kwa Biblia, akifanya hivyo akiwa katika kiti chake cha magurudumu au kwa kuandika barua. Yeye anachapa barua zake kwa kupiga herufi za taipureta kwa kijiti anachokishika mdomoni mwake. Pia, yeye anahudhuria mikutano ya Kikristo kwa ukawaida na kutoa hotuba katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi inayoongozwa na Mashahidi wa Yehova. Mfano wa imani yake, pamoja na kazi yake ngumu na kupiga kwake moyo konde, ni chanzo cha kitiamoyo kwa wale walio karibu naye.

Imani katika Neno la Mungu na ahadi zake zimesaidia wengine jinsi iyo hiyo. Kwa mfano, zimesaidia wengi washinde mazoea na desturi zisizo za Kikristo, kama vile mazoea ya kibiashara yenye udanganyifu, kuiba, kuvuta sigareti, kucheza kamari, ulevi, kupashana habari na ulimwengu wa roho, ngono zisizo na adili, na mazoea ya kidini yasiyo ya kweli. Jambo moja linalofanana katika mambo yote hayo yaliyoonwa lilikuwa kupata ushahidi wenye kusadikisha kwamba Yehova Mungu yuko, kwamba Biblia ni Neno lake lililoandikwa, na kwamba ahadi zake zilizoandikwa katika Maandiko ni zenye kutegemeka na zitatimizwa, Imani kama hiyo inaweza kuondosha milima.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki