Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 11/1 uku. 24
  • Guinea Yakaribisha Wakusanyikaji wa “Amani ya Kimungu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Guinea Yakaribisha Wakusanyikaji wa “Amani ya Kimungu”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Habari Zinazolingana
  • Sanduku la Swali
    Huduma Yetu ya Ufalme—2000
  • Kazi ya Kufanya Wanafunzi Imefinyanga Maisha Yangu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Mtu wa Mnara wa Mlinzi
    2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Nilipata Usalama wa Kweli kwa Kumtumaini Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 11/1 uku. 24

Watangazaji wa Ufalme Waripoti

Guinea Yakaribisha Wakusanyikaji wa “Amani ya Kimungu”

SIKU nne za kwanza za 1987 ziliona mkusanyiko wa wilaya wa kwanza wa Mashahidi wa Yehova uliopata kufanyiwa katika Jamhuri ya Guinea, Afrika ya Magharibi. Ijapokuwa Guinea sana sana ni nchi ya Kiislamu ambako kazi ya Mashahidi wa Yehova haijatambuliwa bado kisheria, Mashahidi huko wamejipatia sifa ya kuwa watu wema, wenye fadhili, wenye kuamanika. Ilikuwa kwa sababu ya sifa hiyo kwamba serikali ilifungua milango wazi kupokea wakusanyikaji wa “Amani ya Kimungu.”

Miongoni mwa wajumbe walikuwamo wamisionari tisa waliosafiri kutoka Freetown, Sierra Leone, kwa vani na pikipiki mbili. Kwenye mpaka, ilikuwa sharti wavuke mtu kwa feri iliyofanyizwa kwa mitumbwi mitatu hivi na mbao zilizolazwa mkingamo juu yayo. Mara walipokuwa wamevuka kwa usalama pamoja na magari yao, wamisionari hao wakauliza: ‘Itatugharimu nini?’ “Ninyi watu ni Mashahidi wa Yehova,” likawa jibu. “Hakuna malipo.”

Namna gani kwa habari ya ushuru wa forodhani na kuingia nchini? “Msihangaikie hilo,” wakaambiwa. “Kila kitu kimekwisha shughulikiwa. Vaeni tu kadi zenu za kunjo la kifuani.” Mamia ya wajumbe wengine walikuwa wakipata maono yanayofanana na hilo. Serikali ya Guinea si kwamba tu ilikuwa imeruhusu nafasi ya kuvuka bila kizuizi mto unaotenganisha Guinea na Sierra Leone na Liberia, ilikuwa pia imeondoa kawaida za forodha na kuingia nchini kwa ye yote aliyekuwa na baji ya kunjo la kifuani ya “Amani ya Kimungu”! Mwangalizi wa mzunguko mmoja, aliyekuja kutoka Liberia, alisema: “Hiyo baji ya kunjo la kifuani ilikuwa bora zaidi sana kuliko pasipoti.”

Serikali ya Guinea ilikuwa saidifu katika njia nyinginezo Waliandaa gari la kusafarisha Mashahidi kutoka Conakry mji mkuu kwenda Guéckédou ule mji wa kusanyiko, umbali wa kilometa zaidi ya 640. Walitoa ruhusa ya kununua petroli kwa ajili ya magari yaliyokuja kutoka Freetown. Waliagiza hoteli iliyokuwa karibu zaidi na mahali pa kusanyiko waweke vyumba vyao vyote kwa ajili ya Mashahidi. Pia walitumia mamlaka yao kupata ruhusa ili jumba la mji litumiwe kwa ajili ya mkusanyiko huo, wakilitoa bure bila malipo.

Gavana wa wilaya, ambaye ndiye afisa mwenye cheo cha juu zaidi sana katika sehemu hiyo ya nchi, aliwapa mahali pa kulala wajumbe 11 kwenye makao yake mwenyewe. Pia, yeye alikuwa miongoni mwa 1,132 ambao walisikiliza hotuba ya watu wote Jumapili.

Yehova Mungu hatasahau fadhili kama hizo wanazoonyeshwa watumishi wake.—Mathayo 10:42; 25:40.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki