Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 12/1 kur. 8-9
  • Ile Mikate na Ile Chachu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ile Mikate na Ile Chachu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Habari Zinazolingana
  • Ile Mikate na Ile Chachu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Afanya Mikate Iongezeke Kimuujiza na Kuonya Kuhusu Chachu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Alisha Maelfu kwa Mwujiza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Yesu Alisha Maelfu kwa Muujiza
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 12/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Ile Mikate na Ile Chachu

MAKUTANO makubwa wamemiminikia Yesu katika Dekapoli. Wengi wamekuja umbali mkubwa kwenye jimbo hilo ambalo sana-sana linakaliwa na Wamataifa ili wamsikilize yeye na kuponywa hali zao za kutoweza. Wao wameleta makapu makubwa, au makanda, ambayo kwa desturi wao wanatumia kuchukulia vyakula vya matumizi wakati wanaposafiri kupita katika maeneo ya Wamataifa.

Hata hivyo, hatimaye, Yesu anaita wanafunzi wake na kusema: “Mimi nahisi sikitikio kwa lile kutano, kwa sababu tayari ni siku tatu ambazo wao wamebaki karibu na mimi na wao hawana kitu cha kula; na mimi nikiwaambia waende zao kwenye makao yao wakiwa wanafunga, wao wataishiwa nguvu katika barabara. Kwa kweli, watu fulani kati yao ni wa kutoka mbali sana.”

“Ni kutoka wapi ambapo mtu ye yote hapa katika mahali palipo peke yapo ataweza kuridhisha watu hawa kwa mikate?” wanafunzi wanauliza.

Yesu anaulizia hivi: “Ni mikate mingapi ambayo ninyi mnayo?”

“Saba,” wao wanajibu, “na samaki wadogo wachache.”

Akiwaagiza watu waegemee chini, Yesu anachukua mikate na samaki wale, anapelekea Mungu sala, anaimega-mega, na kuanza kuwapa wanafunzi wake. Wao, nao, wanawatolea watu wale, nao wote wanakula mpaka kuridhika. Baada ya hapo, wakati masalio yanapookotwa, kuna makapu saba ya kuchukulia maandalizi ambayo yamejaa, hata ingawa karibu wanaume 4,000, pia wanawake na watoto, wamekula!

Yesu anaambia makutano hao waende zao, anapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, na kuvuka kwenda kwenye ufuo wa magharibi wa Bahari ya Galilaya. Hapa Mafarisayo, wakati huu wakiwa wameandamana na washiriki wa lile farakano la Masadukayo, wanajaribu kushawishi Yesu kwa kumuuliza aonyeshe ishara kutoka mbinguni.

Kwa kujua jitihada zao za kumshawishi, Yesu anajibu: “Wakati jioni inapoingia ninyi mna desturi ya kusema, ‘Itakuwa hali ya hewa iliyo nzuri kiasi, kwa maana anga lina wekundu-moto’; na asubuhi, ‘Itakuwa hali ya hewa iliyo ya kipupwe-kipupwe na mvua-mvua leo, kwa maana anga lina wekundu-moto, lakini lenye kuonekana la utusi-utusi.’

Ninyi mnajua kufasiri sura ya anga, lakini zile ishara za nyakati ninyi hamwezi kufasiri.” Kufuata hilo, Yesu anawaita wao kuwa waovu na wazinifu na kuwaonya kwamba, kama vile alivyokuwa ametangulia kuambia Mafarisayo, hakuna ishara watakayopewa isipokuwa ile ishara ya Yona. Kwa kuondoka, yeye na wanafunzi wake wanaingia katika mashua na kuelekea Bethsaida katika ufuo wa kaskazini mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Wakiwa njiani wanafunzi wanagundua kwamba wao wamesahau kuleta mkate, kwa kuwa miongoni mwao mna mkate mmoja tu.

Akifikiria akilini mkabiliano wake pamoja na Mafarisayo na Masadukayo wenye kuunga mkono Herode, Yesu anaonya kwa upole hivi: “Endeleeni kuweka macho yenu yakiwa wazi, tazameni kwa kujihadhari na ile chachu ya Mafarisayo na ile chachu ya Herode.” Kwa kuwa wanafunzi wanaitikadi ya kwamba Yesu anarejeza kwenye lile jambo la kusahau kwao kuleta mkate, huku chachu kwa wazi ikidokeza kwenye akili zao wazo la mkate, wao wanaanza kutoleana hoja juu ya jambo hilo. Kwa kuona kutofahamu kwao, Yesu anasema: “Kwa sababu gani ninyi mnatoleana hoja juu ya kutokuwa na mikate?”

Hivi majuzi, Yesu alikuwa ameandaa kimuujiza mkate kwa ajili ya maelfu ya watu, akifanya muujiza huo wa mwisho labda siku moja au mbili tu kabla ya hapo. Inawapasa wao kujua kwamba yeye hahangaikii ukosefu wa mikate halisi. “Je! ninyi hamkumbuki,” yeye anawakumbusha, “wakati mimi nilipoivunja-vunja ile mikate mitano kwa ajili ya wale wanaume elfu tano, ni makapu mangapi yenye kujaa vipande-vipande ambayo ninyi mlichukua?”

“Kumi na mawili,” wao wanajibu.

“Wakati mimi nilipoivunja-vunja ile saba kwa ajili ya wale wanaume elfu nne, ni makapu mangapi ya kuchukulia maandalizi yenye kujawa na vipande-vipande ambaye ninyi mlichukua?”

“Saba,” wao wanajibu.

“Je! ninyi hamwipati maana?” Yesu anauliza. “Ni jinsi gani ninyi hamng’amui kwamba mimi sikusema kwenu ninyi juu ya mikate? Bali chungulieni ile chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”

Mwishowe wanafunzi wanaipata maana. Chachu, kitu ambacho kinasababisha uchachishaji na kufanya mkate uumuke, lilikuwa neno ambalo mara nyingi lilitumiwa kuonyesha ufisadi. Kwa hiyo sasa wanafunzi wanafahamu kwamba Yesu anatumia neno la ufananishi, kwamba yeye anawaonya wao wawe macho dhidi ya “lile fundisho la Mafarisayo na Masadukayo,” fundisho ambalo lina matokeo yenye kufisidi. Marko 8:1-21; Mathayo 15:32–16:12, NW.

◆ Kwa sababu gani watu wanatembea wakiwa na makapu makubwa ya maandalizi?

◆ Baada ya kuondoka Dekapoli, ni safari gani za mashua ambazo Yesu anafunga?

◆ Ni kutofahamu gani ambako wanafunzi wanako kwa habari ya elezo la Yesu juu ya chachu?

◆ Yesu alimaanisha nini kwa kusema “ile chachu ya Mafarisayo na Masadukayo”?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki