Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 1/15 uku. 7
  • Kujua Yaliyo Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kujua Yaliyo Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • lle Ishara Isiyofaa
  • Hakuna Maji—Hakuna Uhai
  • Kuzuru Tena Sayari Nyekundu
    Amkeni!—1999
  • Kuitazama Mihiri kwa Ukaribu
    Amkeni!—2009
  • Roboti Yachunguza Mihiri
    Amkeni!—1998
  • Mfumo Wetu wa Pekee wa Jua—Jinsi Ulivyotokea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 1/15 uku. 7

Kujua Yaliyo Katika Habari

lle Ishara Isiyofaa

“Ishara yako wewe ni nini?” Kwa mamilioni ya watu ambao wanatafuta maoni kwa kutazama orodha za “ishara za nyota” ambazo zinatayarishwa na wanajimu, swali hilo ni la umaana mkubwa. Wao wanaitikadi kwamba mahali zilipo nyota, sayari, jua, na mwezi kuhusiana na viungamano vya nyota za zodiaki wakati wa kuzaliwa panaongoza moja kwa moja maisha ya mtu. Hata hivyo, kulingana na Independent gazeti la kila siku la London, wanajimu wanawapa watu ishara isiyofaa. Orodha za “ishara za nyota” zinazotumiwa kwa kutabiri matukio ya maishani inategemea msingi wa “sheria” za uanajimu zilizochorwa yapata miaka 2,000 iliyopita.

Inasema Independent: “Mwanajimu ataambia wazazi wa kitoto kilichozaliwa karibuni cha siku hizi kwamba kitoto hicho kitalingana na kikundi cha nyota za Cancer [Kaa].” Hata hivyo, ripoti hiyo inasema: “Kama wao badala ya hivyo wangetazama mahali lilipo jua katika anga, wao wangepata kwamba jua kwa kweli limo katika Gemini.” Ni kitu gani kinachosababisha jambo hilo? Wastadi wa uchunguzi wa nyota wanakiita “badiliko la utangulizi wa zile siku-mlingano”—tukio la kiajabu ambalo katika hilo mhimili wa dunia unayumba-yumba kama vile pia ya kucharazwa kwa kamba inavyotikisika-tikisika inapopunguza mwendo. Hilo badiliko la utangulizi, au “myumbo-myumbo,” linamalizia mduara wa digrii 360 kila miaka 25,800, jambo ambalo linamaanisha kwamba zile siku-mlingano zinasonga mbele kwa dakika 50 za mduara huo kila mwaka, au digrii moja katika muda wa miaka 72. Hivyo, katika miaka 2,000 iliyopita, mahali ambapo jua linaonekana likiwa katika anga pamerudi nyuma kwa ishara moja kamili ya zodiaki. Kama tokeo, “ishara inayohusiana na utabiri wa siku ya mtu ya kuzaliwa haionyeshi kwa ukamili juu ya hali ya mbingu wakati ambao mtu yule alizaliwa,” anaeleza Richard F. Smith katika kitabu chake Prelude to Science. “Walio wengi kati ya watu wa ulimwengu huu wanaolinganishwa na mahali kilipo kile kikundi cha nyota za Scorpio [Nje],” yeye anaeleza, “kwa kweli walizaliwa wakati jua lilipokuwa katika kikundi cha nyota za Libra, na walio wengi kati ya wale wanaolinganishwa na mahali kilipo kikundi cha Leo [Simba] kwa kweli walizaliwa ilipokuwa ni Cancer, na wale wa Cancer ni wa Gemini, na vivyo hivyo.”

Kule kutotegemeka kwa orodha za nyota na ishara zinazofuatwa katika matabiri juu ya matukio ya maishani kunakazia tu hekima ya kutegemea Muumba kwa mwongozo wala si vitu ambavyo yeye aliviumba.” (Warumi 1:24, 25) Hata hivyo, sababu ambayo ni kubwa hata zaidi ya kuepuka utumizi wa ishara za kutabiri matukio ya maishani ni kwamba kufanya hivyo kungeweza kuongoza mtu atolee ibada “jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi ia mbinguni vyo vyote, [jambo ambalo Mungu hakuagiza].”—Kumbukumbu 17:2-5.

Hakuna Maji—Hakuna Uhai

Hivyo ndivyo alivyokata shauri Profesa Norman H. Horowitz, mwanasayansi mmoja mwenye ushirika na zile safari za Mariner na Viking za 1965-76 za kwenda Mars.

Katika kitabu chake To Utopia and Back: The Search for Life in the Solar System, Profesa Horowitz alisema kwamba mambo aliyopata kutokana na safari hizo yalimaliza waziwazi lile swali la kama kuna uhai juu ya Mars au juu ya sayari nyingine yo yote katika mfumo-jua wetu. “Mars,” yeye anasema, “haina ile sura nzuri ajabu ambayo inatawala mazingira ya sayari yetu yenyewe, bahari kuu za maji maowevu katika mahali pa kuweza kuona jua kabisa.” Utafiti ulithibitisha kwamba sayari hiyo ina ukosefu wa maji.

Baada ya majaribio ya uangalifu kuondolea mbali kila uwezekano wa kuwako uhai juu ya Mars, Horowitz alikiri hivi: “Ule mshindikano wa kupata uhai juu ya Mars ulikuwa mtamausho, lakini ulikuwa ufunuo pia. Kwa kuwa Mars ilitazamiwa sana kuwa ndipo mahali ambapo pangefaa zaidi kuwa makao ya uhai wa nje ya dunia katika zile sayari za mfumo-jua, sasa ni kama imehakikishwa kwamba dunia ndiyo sayari moja tu iliyo na uhai katika jimbo letu la ile galaksi.”

Ilifaa kama nini kwamba, wakati alipokuwa akiandika juu ya dunia, Isaya nabii wa kale akasema kwamba Mfanyi wayo “aliiumba ili ikaliwe.” (Isaya 45:18) Maji yametajwa mapema katika masimulizi ya uumbaji ya Biblia. Kwa uwazi, kuandaa maji kabla ya uumbaji wa umbo-uhai lo lote la kidunia lilikuwa jambo lililohitajiwa kabisa. Kama vile ambavyo safari za kwenda kwenye Mars zimeshuhudiza: Nje ya ulimwengu wa roho, mahali ambapo hapana maji, hapawezi kuwa na uhai.—Mwanzo 1:1-10.

[Picha katika ukurasa wa 7]

Sura ya Mars, sayari isiyo na uhai, kama ionekanavyo kutoka chombo cha anga za juu “Viking II”

[Credit Line]

NASA photo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki