Yesu Kristo Mwanadamu, au Mtu wa Hadithi Tu?
KIPINDI cha muziki wa roki kilichofunguliwa huko Broadway katika Jiji la New York katika 1971 kilithibitika kuwa chenye kutokeza ubishani, kwa kuwa kilishughulikia habari ya kidini. Lakini pengine habari hiyo haikuwa yenye kutokeza ubishani sana kama vile utambulishi wa mtu mwenyewe ulivyotokeza.
Mmojapo ya nyimbo zilizopendwa sana uliopigwa katika kipindi hicho uliuliza hivi: “Yesu Kristo, unayejulikana sana unafikiri wewe ni kile ambacho wanasema?” Watu katika karne ya kwanza walisema Yesu ni nani? Yesu mwenyewe aliuliza wanafunzi wake swali hilo naye alipata majibu mengi tofauti tofauti. (Mathayo 16:13, 14) Leo, takriban miaka 2,000 baadaye, utambulishi wa Yesu Kristo ungali wenye kubishaniwa.
Je! ni jambo la muhimu kujua Yesu alikuwa nani? Utambulishi wake unaweza kuwa na madhara gani kwetu? Watu mashuhuri wa siku zilizopita walifanyiza historia ya ulimwengu, hivyo wakaathiri sisi sote, ikiwa ni kwa njia isiyo ya moja kwa moja tu. Lakini leo wao ni wafu. Hivyo, ingawa wametuathiri kwa kile walichofanya, hawawezi kutuathiri kamwe kwa kile wanachofanya.
Hata hivyo, kwa habari ya Yesu Kristo mambo ni tofauti kabisa. Mamilioni wanaitikadi, na wana ithibati mkataa kwa itikadi hiyo, kwamba Yesu yu hai leo, si kama mwanadamu duniani, bali akiwa kiumbe roho mwenye nguvu katika mbingu. Jambo ambalo Yesu amekuwa akifanya, hasa katika karne hii ya 20, limekuwa na madhara makubwa kwa wanadamu wote. Waaidha, athiri ya Yesu juu ya maisha yetu haijawekewa hadi kwa yale ambayo ametenda wakati uliopita. Inatia ndani yale ambayo anafanya wakati huu na yale ambayo atafanya wakati ujao.
Tukirudia kichwa chetu: Yesu Kristo—Ni Mungu, mwanadamu, au mtu wa hadithi tu? Wewe unafikiri nini? Ikiwa Yesu ni mtu wa kihadithi tu ingemaanisha kwamba yeye hakuwa Mungu wala mwanadamu, hiyo ikifanya kufikiria zaidi jambo hili kukose maana. Kwa upande mwingine, tunapaswa kuwa na hamu nyingi ya kujifunza kuhusu Yesu aliye hai na ambaye amepewa uwezo na Mungu wa kuletea aina ya binadamu manufaa yenye kudumu.