Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 8/15 kur. 3-4
  • Ule Mfinyo wa Kupata Mafanikio

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ule Mfinyo wa Kupata Mafanikio
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mifinyo Ambayo Watu Wanakabiliana Nayo
  • Ni Jambo Gani Linaweza Kutokea?
  • Jinsi Unavyoweza Kupata Mafanikio ya Kweli Maishani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Kufanikiwa kwa Gharama Yoyote?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Jinsi ya Kupata Mafanikio ya Kweli
    Amkeni!—2014
  • Mafanikio ya Kweli Yanapatikana Jinsi Gani?
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 8/15 kur. 3-4

Ule Mfinyo wa Kupata Mafanikio

TANGAZO moja la kibiashara katika televisheni huhimiza Wanaijeria kwamba “Uwe mwenye mafanikio. Uwe mashuhuri” kwa kutumia aina fulani ya dawa ya meno. Ingawa sisi sote tunajua kwamba ni vigumu dawa ya meno kuwa ndiyo ufunguo wa mtu kuwa mashuhuri, watangazaji wale wanaonyesha wao wanatambua kwamba watu wanataka kutambulishwa na vitu vinavyosemwa kuwa vyenye kuleta “mafanikio.”

Tamaa ya kufaulu na kutambuliwa na wengine ni ya kiasili. Hata hivyo, wanaume na hata wanawake mara nyingi wanaweka mkazo mwingi sana juu ya kutimiza kwa binadamu mambo yaliyo bora hivi kwamba wanajitia wenyewe chini ya mfinyo wa kufanya yanayofanywa na wenzao ili wasiachwe nyuma. Je! jambo hili lingeweza kuwa hatari? Je! lingeweza kukuathiri wewe?

Mifinyo Ambayo Watu Wanakabiliana Nayo

Tamaa-makuu ya kibinafsi ya kutaka kuwa tajiri inaweza kutokeza mfinyo. Watu wengi wanataka waweze kufanya “wonyesho mshaufu wa mali [zao] za maisha,” ili wawe na fahari na umashuhuri katikati ya jamii ya watu.​—1 Yohana 2:16, NW.

Huenda jamaa ikatokeza mfinyo. Katika maskani nyingi ni lazima mume ajitahidi kwa kuzidi kufanya mwendelezo wa machumo yake na msimamo wake kazini ili ainue msimamo wa jamaa katikati ya jamii ya watu. Au huenda mke akajitahidi kuwa mwanamke mfanikiwa katika kufuatia kazi-maisha. Watoto wanaweza kusukumwa kuelekea kuwa na mafanikio makubwa ya kimasomo shuleni. Hili ni tatizo hasa katika mataifa yanayositawi ambako wengi wanaitikadi kwamba ufunguo wa mtu kufanya fungu lake maishani liwe bora umo katika elimu ya juu zaidi.

Huenda pia jumuiya ikatokeza mfinyo juu ya mtu ili alenge shabaha ya elimu ya juu zaidi, awe na utajiri, na vyeo vyenye fahari na uvutano mwingi. Kwa kawaida mafanikio, ambayo yanapimwa kulingana na pesa, huenda yakaongoza mtu kwenye umashuhuri, sifa, na staha. Tahariri moja ya Daily Times ya Naijeria ilisema hivi: “Hata kama mmoja ana sifa zenye wema na uvutio wa kadiri gani, [watu] walio wengi hawampi staha wala kumtambua yeye, ikiwa yeye hana pesa.”

Ni Jambo Gani Linaweza Kutokea?

Mafanikio hayo ya kilimwengu yanaweza kuleta mfurahio wa kadiri fulani, lakini fikiria ile bei kubwa ambayo yanaitoza pia. Mchangiaji wa safu za magazeti, Achike Okafo, aliandika hivi: “Jamaa zenye utulivu . . . zinavunjika-vunjika kila siku, sana-sana kwa sababu ya pesa na vitu vile ambavyo pesa zinaweza kununua. . . . Hata wenzi wa ndoa ambao bado wanamudu kukaa pamoja hawaongei sana juu ya wajibu wao mbalimbali wa kiuzazi... kwa sababu wote ni wenye shughuli nyingi mno katika ufuatiaji wa matakwa ya kimwili ya kuwa na hali njema.” Ongeza kwenye jambo hilo lile tatizo la watoto wasio na mtu wa kuwajali ambao wanageukia dawa za kulevya na uhalifu au wanaotoroka kwenye maskani yao, halafu bei yenyewe itakuwa ya gharama ya juu sana.

Ule mfinyo wa kupata mafanikio umesukuma watu fulani wenye kutaka makuu waingie katika kutofuata haki na kukosa adili. Wanawake vijana hata wamefanya biashara ya kubadilishana mapenzi ya kingono ili wapitishwe mitihani na kupewa kazi ya kuajiriwa. Hata wakati mafanikio yanapopatwa kwa njia ya kuheshimika, watu wenye ufanisi huenda wakakabiliana na uchungu au kijicho cha wasiofanikiwa sana na pia unafiki wa “marafiki” wanaovutiwa na utajiri na fahari. (Mhubiri 5:11) Je! kweli haya ni mafanikio?

Yule mwandikaji mwenye hekima wa Mhubiri katika Biblia anajibu hapana. Baada ya kuchunguza-chunguza utajiri wake mkubwa, nguvu zake za kimamlaka na fahari yake, pia mfurahio ambao mambo hayo yalileta, yeye alikata shauri kwamba hayo yalikuwa ni “ubatili na kujilisha upepo.”​—Mhubiri 2:3-11.

Je! hiyo inamaanisha kwamba kila ufuatiaji ulio maishani ni wa kazi-bure tu? Au kuna usawaziko fulani unaofaa ambao watu wanaweza kuwa nao wanapojenga kazi-maisha yenye matokeo? Mambo yaliyoonekana maishani yanaonyesha ni jambo gani litaelekea kuthibitika kuwa ndilo mradi wao unaofaa zaidi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki