Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 1/15 kur. 3-4
  • Kwa Nini Uwe na Akili Iliyofunguka Kupokea Mawazo Mapya?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Uwe na Akili Iliyofunguka Kupokea Mawazo Mapya?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Kilichofanya Japani Ijitenge Mbali na Wengine?
  • Mwisho wa Kujitenga Mbali na Wengine
  • Je! Wewe Una Akili Iliyofunguka Kupokea Mawazo Mapya?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Je! Kazi Ngumu Huleta Furaha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Jinsi Kijiji cha Wavuvi Kilivyokuja Kuwa Jiji Kubwa
    Amkeni!—2008
  • Wajapani Wapokea Zawadi Ambayo Hawakutarajia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 1/15 kur. 3-4

Kwa Nini Uwe na Akili Iliyofunguka Kupokea Mawazo Mapya?

PAZIA la ukungu lilipokuwa likiinuka polepole, Matthew C. Perry amiri Mwamerika wa kikosi cha meli aliona Mlima Fuji akiwa katika sakafu ya meli yake ya uongozi, ile Susquehanna. Alikuwa amekuwa akitamani sana kuiona Japani na mwishowe akaifikia siku ya Julai 8, 1853, baada ya kusafiri baharini kwa zaidi ya miezi saba. Amri huyo alikuwa amechunguza kila ripoti iliyopatikana kuhusu nchi ile. Kwa nini? Kwa sababu alitumainia kufungua huo “ufalme uliojikalia peke yao” uwe wazi kwa ulimwengu.

Nao ulikuwa umejikalia peke yao kweli kweli! Zaidi ya miaka 200 mapema, Japani ilikuwa imekata mahusiano ya kibiashara na kitamaduni na nchi zote isipokuwa China, Korea, na Uholanzi. Halafu taifa hilo likajikalia kitako kwa ustarehe usio na masumbufu. Katika hali hiyo, lililanda watu wengi mmoja mmoja ambao hukinza mawazo mapya na kukataa kusikiliza kauli zinazotofautiana na zao wenyewe. Kwa njia fulani-fulani, kufanya hivyo kunaweza kufariji, kwa maana mawazo mapya yanaweza kukosesha utulivu, hata kuogopesha sana. Lakini je! ni hekima kuwa na msimamo kama huo? Basi, fikiria matokeo ya sera ya Japani ya kujitenga mbali na wengine.

Ni Nini Kilichofanya Japani Ijitenge Mbali na Wengine?

Japani haikujitenga mbali na wengine bila sababu. Katika 1549, Francis Xavier misionari Myeswiti aliwasili Japani kueneza dini yake. Katika kipindi kifupi, imani ya Katoliki ya Kiroma ikawa mashuhuri katika bara hilo. Watawala wa wakati huo walikuwa wamefanyiwa uasi wa kidini na farakano moja la Kibuddha na waliona uwezekano wa jambo hilo hilo miongoni mwa Wakatoliki. Kwa sababu hiyo, Ukatoliki ulipigwa marufuku, ingawa marufuku hiyo haikufikilizwa kwa kufuatiliwa sana.

Kwa kudai kwamba Japani lilikuwa “taifa lililo la kimungu,” watawala hawakuwa na madhumuni ya kuruhusu dini “ya Kikristo” itishe mfumo wao. Basi, kwa nini hawakufikiliza marufuku juu ya Ukatoliki kwa uthabiti zaidi? Kwa sababu wamisionari Wakatoliki walikuja wakiwa katika meli za biashara za Kireno, na serikali ilitamani faida zenye kuletwa na vyombo hivyo vya bahari. Hata hivyo, pole kwa pole tamaa ya watawala ya kutaka biashara ikalemewa na hofu ya kwamba Wakatoliki wangetia uvutano wao katika Wajapani. Hivyo, wao wakatoa maamrisho ya udhibiti wenye mkazo zaidi ili kuzuia biashara ya kigeni, kuzuia wananchi wao wenyewe wasitoke nchini, na kuzuia “Wakristo.”

Wakati “Wakristo” wenye kunyanyaswa na kubanwa sana walipoasi dhidi ya bwana-shamba mwenye kusimamia ardhi yao, hapo ndipo mambo yalipochacha. Kwa kuwa na rai ya kwamba maasi hayo yalitokana moja kwa moja na propaganda za Kikatoliki, serikali kuu ya Gavana wa kijeshi iliwafukuza Wareno na kufanya iwe haramu Wajapani kwenda ng’ambo. Amrisho hilo lilipotolewa katika 1639, Japani ilijitenga kihalisi na nchi nyinginezo.

Wanamagharibi wa pekee kuruhusiwa waendeleze biashara pamoja na Japani walikuwa Waholanzi, waliojazanishwa katika Dejima, ambacho wakati huo kilikuwa ni kisiwa kidogo katika bandari ya Nagasaki. Kwa miaka 200, utamaduni wa Magharibi ulipenya-penya katika Japani kupitia tu Dejima ambacho sasa kilikuwa kimetiishwa. Kila mwaka, mkurugenzi wa kituo cha ubiashara kisiwani alitoa “Ripoti ya Waholanzi,” iliyojulisha serikali yaliyokuwa yakiendelea katika ulimwengu wa nje. Lakini utawala wa Gavana wa kijeshi ulihakikisha kwamba hakuna mtu mwingine yeyote aliyeona ripoti hizo. Kwa hiyo Wajapani wakaishi wakiwa peke yao mpaka Amiri Perry alipowapigia hodi kali katika 1853.

Mwisho wa Kujitenga Mbali na Wengine

Meli kubwa nyeusi za Perry zilipokuwa mwendoni kuingia Hori ya Edo, zikiduwaza wavuvi wa huko, waliofikiri hizi zilikuwa milima inayoenda yenye kulipusha moto. Raia za Edo (ambayo sasa ni Tokyo) walibabaika, na wengi wakakimbia jiji hilo wakiwa na fanicha yao. Mhamo huo ulikuwa mkubwa sana hata serikali ikalazimika kutoa ilani rasmi ili kutuliza watu.

Kilichowashangaza sana watu hao wenye ku- kaa peke yao hakikuwa meli za stimu tu zenye kuamrishwa na Amiri Perry bali pia zawadi alizoleta. Wao walistaajabishwa na wonyesho wa kupeleka jumbe kutoka jengo moja hadi jingine kwa njia ya telegrafu. Usimulizi Narrative of the Expedition of an American Squadron to the China Seas and Japan, uliokusanywa chini ya usimamizi wa Perry, unaeleza juu ya maofisa Wajapani ambao waligusika sana hisia hata wakadandia kigari kidogo sana chenye umbo la gari-moshi la kawaida ambacho “hakingeweza hata kumbeba mtoto wa miaka sita. Hatajnandarini (ofisa) mwenye fahari” alijishikiza kwenye paa ya kigari hicho “huku majoho yake legelege yakipeperushwa-peperushwa na upepo.”

Mwishowe mlango wa kuingia Japani ulilazimishwa kufunguka wazi kabisa na ziara ya pili ya Perry mwaka uliofuata. Kwa kulemewa na mbano, serikali ikafungua wazi nchi hiyo. Waliojitahidi kufa na kupona ili wahifadhi hali ya kujitenga kwa Japani waligeukia uvamizi-haramu, wakaua waziri mkuu wa serikali, na kushambulia watu wa kigeni. Mabwana fulani wenye kutetea hali hiyo walifyatua risasi kuelekea vikosi vya meli za kigeni. Hata hivyo, hatimaye mashambulizi yao yalififia, na mmaliki akatwaa serikali kutoka kwa Gavana wa kijeshi wa Tokugawa.

Kufikia wakati ambapo Perry alifungua mlango wa kuingia Japani, mataifa ya Magharibi yalikuwa yamekwisha kupita katika ule Muda wa Mageuzo Makubwa ya Shughuli za Viwandani. Kwa sababu ya Japani kuwa imejitenga mbali na wengine, nchi hiyo ilikuwa imeachwa nyuma sana. Nchi zenye viwanda zilikuwa zimechota nguvu za stimu. Kufikia miaka ya 1830, injini na mashine za kutumia stimu zilikuwa zikitumiwa kwa wingi. Sera ya Japani ya kujitenga mbali na wengine ilikuwa imesababisha nchi hiyo ibaki nyuma sana katika maendeleo ya viwanda. Jambo hilo lilihisiwa sana na ujumbe wa kwanza wa Japani uliopelekwa Ulaya. Kwenye wonyesho mmoja mkubwa uliofanywa katika London katika 1862, vionyesho vya Wajapani vilikuwa vya karatasi na mbao vikiwa vya hali ile “ambayo ingewekwa katika wonyesho wa duka la vitu vya kale,” kulingana na mjumbe mmoja aliyeona haya.

Wajumbe Wajapani katika Ulaya na United States walihisi uhitaji mkubwa sana wa kufanya nchi yao iwe na maendeleo ya viwandani na wakaanzisha kwa hamu nyingi mavumbuzi na mawazo ya ki-siku-hizi. Miaka 64 baada ya ziara ya kwanza ya Perry, mshiriki wa mwisho kubaki hai kati ya kikosi chake alizuru Japani na kusema: “Mimi nilistaajabishwa sana na maendeleo ya Japani katika muda unaozidi kidogo tu miaka sitini.”

Kwa sababu hiyo, sera ya Japani ya kujitenga na wengine ilifanya uwe haba sana ukuzi wa nchi hiyo. Kufungua milango ili iingiwe na mawazo mapya kulithibitika kuwa na manufaa kwa taifa hilo kwa njia nyingi. Hata hivyo, leo watu fulani katika Japani wanaonyesha “hali ya kujitenga na wengine kiakili” miongoni mwa watu mmoja mmoja, nao wanatokeza hilo kuwa tatizo moja la kutatuliwa. Kweli kweli, ni tatizo kushinda elekeo la kukinza mawazo mapya, si kwa Wajapani wa ki-siku-hizi tu bali kwa wanadamu wote. Namna gani wewe na ile “hali ya kujitenga na wengine kiakili”? Je! wewe ungenufaika kwa kuwa na akili iliyofunguka ipokee mawazo mapya, kama vile Japani ilivyonufaika kule nyuma katika miaka ya 1850?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki