Maisha na Huduma ya Yesu
Hadithi ya Mwana Mpotevu
MAFARISAYO wamechambua Yesu kwa kufanya uandamani pamoja na watu wanaojulikana kuwa watenda dhambi, na katika kujibu yeye amemaliza sasa tu kusimulia vielezi kuhusu kondoo mpotevu na sarafu-drakma iliyopotea. Sasa yeye anaendelea na kielezi kingine, hiki kikihusu baba mmoja mwenye upendo na jinsi anavyotendea wanaye wawili, kila mmoja wao akiwa na dosari kubwa-kubwa.
Kwanza, kuna yule mwana mchanga zaidi, aliye mhusika mkuu wa kielezi hiki. Yeye anakusanya urithi wake, ambao baba yake amempa bila kusita-sita. Halafu yeye anaondoka kwenye maskani yao na kuhusika katika njia ya maisha ya kukosa sana adili. Lakini sikiliza wakati Yesu anaposimulia hadithi hii, na uone kama unaweza kupambanua wahusika hao wamekusudiwa kuwakilisha nani.
“Mtu mmoja,” Yesu anaanza, “alikuwa na wana wawili; yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. [Baba huyoj akawagawia vitu vyake.” Huyu aliye mchanga zaidi anafanya nini na kile anachopokea?
Yesu anaeleza, “Baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.” Uhakika ni kwamba, yeye anatumia pesa zake akiishi pamoja na malaya. Baadaye nyakati zenye magumu zinakuja, kama vile Yesu anavyoendelea kusimulia:
“Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu”
Lo, ni kushushwa cheo kama nini kulazimika kuanza kuchunga nguruwe, kwa maana wanyama hao walikuwa si safi kulingana na Sheria! Lakini kilichoumiza zaidi hisia za mwana huyo kilikuwa ile njaa yenye kumtafuna-tafuna ambayo hata ilisababisha atamani chakula walicholishwa nguruwe. Kwa sababu ya afa hilo baya sana, Yesu alisema, ‘akazingatia moyoni mwake [‘akili zake zikamrudia,’ NW].’
Akiendelea na hadithi yake, Yesu anaeleza hivi: “Alisema [akijiambia mwenyewej, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. Akaondoka, akaenda kwa babaye.”
Hapa pana jambo la kufikiria: Kama baba yake angalikuwa amemgombeza-gombeza na kumpigia makelele ya hasira wakati alipoondoka kwenye maskani yao, haielekei kwamba mwana huyo angalikuwa na nia moja tu juu ya limpasalo kufanya. Huenda ikawa angaliamua kurudi na kutafuta kazi mahali pengine katika nchi ya kwao ili asilazimike kukabiliana uso kwa uso na baba yake. Hata hivyo, hakuna fikira ya jinsi hiyo iliyoingia akilini mwake. Yeye alitaka kuwa kuko huko kwenye maskani yao!
Ni wazi kwamba, yule baba katika kielezi cha Yesu anawakilisha Baba yetu wa kimbingu mwenye upendo na rehema, Yehova Mungu. Na pia labda wewe unatambua kwamba yule mwana mpotevu anawakilisha watu wenye kujulikana kuwa watenda dhambi. Mafarisayo, ambao Yesu ananena nao, hapo kwanza wamekuwa wakimchambua Yesu kwa kula pamoja na watu hao hao.
Lakini mwana yule mwenye umri mkubwa zaidi anawakilisha nani? Na kielezi cha Yesu kina utumizi gani katika karne yetu ya 20? Toleo letu linalofuata la gazeti hili litajibu maswali hayo linapozungumzia sehemu iliyobaki ya hadithi ya Yesu juu ya mwana mpotevu aliyepatikana. Luka 15:11-20, 30; Walawi 11:7, 8.
◆ Yesu anasimulia kielezi, au hadithi hii kwa nani, na kwa nini?
◆ Ni nani mhusika mkuu katika hadithi hii, na ni jambo gani linalompata?
◆ Baba na mwana yule mchanga zaidi wanawakilisha nani?
◆ Ni habari gani tunazoweza kutazamia katika toleo linalokuja la gazeti hili?