Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 9/1 kur. 3-4
  • Utawala wa Makasisi Je! Ndilo Jibu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Utawala wa Makasisi Je! Ndilo Jibu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Makasisi Walipotawala Ulaya
  • Hukumu ya Mungu Dhidi ya “Mtu wa Kuasi [Sheria]”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Dini ya Calvin Imetimiza Nini Tangu Ianzishwe Miaka 500 Iliyopita?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke Yake
    Amkeni!—2006
  • “Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 9/1 kur. 3-4

Utawala wa Makasisi Je! Ndilo Jibu

WATU wamechoshwa na ukosefu wa haki, uonevu, na ufisadi wa kisiasa ulimwenguni pote. Wanataka kitu fulani kilicho bora kama inavyotolewa ushuhuda na jitihada zao za kubadili viongozi wa kisiasa. Lakini ni mara chache sana viongozi wapya wanapowaletea watu uradhi.

Watu fulani wanafikiri kwamba utawala wa makasisi utatokeza serikali iliyo bora. Wao wanaamini kwamba makasisi wangeingiza sifa za kimungu katika shughuli za kisiasa. Labda kasisi Marion (Pat) Robertson, aliyetumaini kuwa rais wa U.S. katika 1988, alifikiria jambo hili aliposali kwamba “watu wanaomcha Mungu” washinde na kupata cheo cha kisiasa. Lakini je! hilo kweli lingetokeza jibu kwa uhitaji wa watawala walio bora?

Makasisi Walipotawala Ulaya

Wakati wa zile Enzi za Katikati, makasisi walikuwa na uwezo mwingi ajabu wa kiserikali. Kwani, mapapa waliweza kuwatawaza na kuwaondoa wafalme! Katika 800 W.K., Papa Leo wa 3 alimtawaza mfalme Mjeremani Charlemagne awe mtawala wa Milki ya Roma Takatifu. Kwa miaka elfu, milki hii iliwakilisha muungano uliokuwako kati ya Kanisa na Serikali, na wakati huo makasisi walionea shangwe uwezo wa viwango mbalimbali waliokuwa nao juu ya mamlaka ya kiserikali.

Kuanzia karne ya 11, upapa ukachukua daraka la kuongoza Ulaya. Kwa habari hii, The Columbia History of the World, kilichohaririwa na John Garraty na Peter Gay, kinasema: “Kanisa lilikuwa ndilo serikali kubwa zaidi ya Ulaya.” Kitabu hiki pia kinaonelea kwamba kanisa liliweza “kutumia uwezo mwingi wa kisiasa kuliko serikali nyingine yoyote ya Magharibi.” Hali ya watu ilikuwaje wakiwa chini ya utawala wa makasisi?

Hakuna mtu aliyekuwa huru kuabudu alivyotaka au kutoa maoni yenye kuhitilafiana na yale ya makasisi. Kutovumilia kwa makasisi kulifanyiza hali ya hofu kote kote katika Ulaya. Kanisa lilianzisha Baraza la Kuhukumu Wazushi wa Kidini ili liondolee mbali watu mmoja mmoja ambao walijaribu kushikilia maoni tofauti. Wakionwa kuwa wazushi, waliletwa mbele ya mahakimu, ambao waliwatesa-tesa ili waungame. Mara nyingi wale waliopatikana wakiwa na hatia walichomwa kwenye mti wa mateso.

Kuhusu utawala wa makasisi katika Hispania, The Columbia History of the World kinataarifu: “Vita na maoni ya ukrusedi vikawa vimeunganisha utawala wa kawaida rasmi ya makabaila wachache wenye vyeo bora wenye kupenda makuu na makasisi ambao walishikilia uongozi wote wa mamlaka katika serikali. Akili za watu zilikuwa zimelemazwa na ukaguzi na Baraza la Kuhukumu Wazushi wa Kidini, ambalo lilikuwa limetumiwa dhidi ya yeyote aliyeteta dhidi ya theolojia rasmi au maongozi ya serikali.”

Katika kitabu chake The Age of Faith, Will Durant alisema: “Tukiruhusu hali zote zinazohitajiwa na mwanahistoria na zinazoruhusiwa kwa Mkristo, lazima tudai kwamba Baraza la Kuhukumu Wazushi wa Kidini, pamoja na vita na minyanyaso ya wakati wetu, ni miongoni mwa mawaa maovu sana katika maandishi ya aina ya binadamu, yenye kufunua ukatili ambao haujapata kujulikana kuwa katika hayawani yeyote.” Katika Enzi za Katikati, utawala wa makasisi ulimaanisha kuharibu uhuru wa kibinafsi.

Je! mrekebisha-kanisa Mprotestanti John Calvin alitofautiana na makasisi Wakatoliki? Basi, fikiria jambo lililotukia wakati Michael Servetus alipotoroka mnyanyaso wa makasisi Wahispania na akashikwa katika Geneva, Switzerland. Akiwa huko, Calvin alikuwa ameanzisha jamii ambayo yeye na wahudumu wake walitawala kwa uwezo kamili. Kwa sababu Servetus alikataa Utatu, Calvin alipata kile ambacho Baraza la Kuhukumu Wazushi wa Kidini halikuweza kukipata. Servetus alihukumiwa kifo kwa sababu ya uzushi naye alichomwa kwenye mti wa mateso. Hivyo Calvin akaonyesha kutovumilia kule kule kulikoonyeshwa na makasisi Wakatoliki.

Je! uongozi wa makasisi wa serikali za ulimwengu ulimaanisha amani kwa watu wa Ulaya? Sivyo hata kidogo. Badala ya kushangilia amani, walilazimika kuvumilia miaka mingi ya vita vilivyovuviwa na makasisi. Papa Urban 2 alianzisha Krusedi ya Kwanza na hivyo akaanza mfululizo wa vita ambavyo viliendelea kwa miaka 200. Zaidi ya hilo, vita vilivyochochewa na makasisi dhidi ya watu walioonwa kuwa wazushi vilitokeza kifo kwa maelfu ya wanaume, wanawake, na watoto.

Je! utawala wa makasisi ulikomesha ufisadi? Hata kidogo. Kitabu A History of the Modern World cha R. R. Palmer na Joel Colton, kinataarifu hivi: “Mwendo wa kanisa ulizidi kufisidiwa na pesa. Hakuna mtu aliyeamini katika hongo; lakini kila mtu alijua kwamba watu wengi wa kanisa walio na vyeo (kama vile maofisa wengi leo wenye vyeo katika serikali) wangeweza kuhongwa.” Ufisadi uliokuwako miongoni mwa makasisi ulilalamikiwa kwa ukawaida.

Je! utawala wa makasisi ulitokeza kuwahurumia watu wa kawaida? Hata. Kwa kielelezo, fikiria lililotokea wakati Kardinali Richelieu wa Ufaransa alipopata uongozi wa mambo ya kiserikali wakati wa utawala wa Louis wa 13. Kitabu The History of the Nations, kilichopigwa chapa na Henry Cabot Lodge, kinasema kwamba “maongozi [ya Richelieu] yalitegemea kuangamiza uhuru wa Wafaransa.”

Katika Meksiko wakati wa karne ya 17, mara nyingi miji ya Wahindi ilitawalwa na makasisi. Kulingana na kitabu Many Mexicos, cha Lesley Simpson, makasisi waliuona mti ambapo watu walichapiwa kuwa ni chombo cha ufundisha na kudumisha maadili ya Kikristo, na pia wa kutumiwa kuadhibu wenye kukosea serikali.”

Hivyo basi vitabu vya Kihistoria vinatuwezesha tuchunguze kumbukumbu la utawala wa makasisi kwa muda wa karne nyingi. Kumbukumbu hilo linafunua nini? Kutojali furaha, hali njema na uhuru wa watu wa kawaida kwa njia yenye kugutusha. Kweli kweli, utawala wa makasisi umekuwa udhalimu usiovumilika. Kama alivyoandika Daniel Defoe katika kitabu chake The True-Born Englishman: “Na kati ya tauni zote ambazo aina ya binadamu imeteseka, udhalimu wa kidini ndio mbaya zaidi.”

Kwa wazi basi, utawala wa makasisi sio jibu kwa uhitaji wa mwanadamu kwa serikali bora. Kwa hiyo, tunaweza kugeukia nani? Jibu linaweza kupatikana na kila mmoja, kama tutakavyoona.

[Picture on page 4]

Mprotestanti Calvin alionyesha kutovumilia kule kule kulikoonyeshwa na makasisi Wakatoliki

[Hisani]

Kwa hisani ya Wadhamini wa Jumba la Makumbusho la Uingereza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki