Ile Kanuni ya Kidhahabu Ni Nini?
“TAZAMA! mimi sisumbui jirani zangu. Kwa kadiri mimi nihusikavyo, wao waweza kufanya watakalo. Lakini, wakipatwa na ugumu, bila shaka mimi ningeweza kuwasaidia kwa vyovyote.” Je! hayo ndiyo maoni yako? Misiba itokeapo ghafula, huenda vitendo vya fadhili na vya kutokuwa na ubinafsi vikawa tele, mara nyingi jambo hilo likishangaza wengi. Lakini je! kufanya hivyo kwatosha?
Ikiwa wewe ni mzazi, pasipo shaka umewashauri watoto wako waepuke kuamsha kasirani ya watoto wenzao michezoni. Wengi wetu tuna makovu ya ujanani mwetu ambayo yaonyesha kwamba kupuuza mwongozo huo huleta kulipwa kisasi. Ndiyo, tumejifunza hekima ya ule msemo wa hekima uliofanyizwa wazi na Konfyushasi mwanafalsafa wa Mashariki: “Usilotaka ufanyiwe wewe, nawe usiwafanyie wengine.” Ingawa hivyo, je! wewe wang’amua kwamba hiyo ni fasiri hafifu tu ya kutochukua hatua hakika nayo imetokana na ile ijulikanayo kuwa Kanuni ya Kidhahabu?
Kanuni ya Kuchukua Hatua Hakika
Kulingana na Webster’s New Collegiate Dictionary, “kanuni ya kidhahabu” yafafanuliwa kuwa “kanuni ya mwenendo wa uungwana ambayo inarejezea [Mathayo] 7:12 na [Luka] 6:31 na ambayo inataarifu kwamba mtu apaswa kutendea wengine kama vile yeye angetaka wao wamtendee yeye.” Tupa jicho kwenye sanduku lililo chini ya ukurasa huu na ufikirie jinsi fasiri tofauti za Biblia kuhusu Mathayo sura ya 7, mstari wa 12 hutoa mwangaza mwingi wa kuelewesha wazi maana ya kanuni hii ya mwongozo.
Tafadhali angalia kwamba japo maneno hayo yatofautiana kutoka tafsiri moja na nyingine, kanuni yenyewe ni ya kuchukua hatua hakika. Ingawaje, kama vile Yesu alivyosababu mambo mapema kidogo katika Mahubiri ya Mlimani: “Endeleeni kuomba, nanyi mtapewa; endeleeni kutafuta, nanyi mtapata; endeleeni kubisha, nanyi mtafunguliwa. Kwa maana kila mmoja anayeomba hupokea, na kila mmoja anayetafuta hupata, na kila mmoja anayebisha atafunguliwa.” (Mathayo 7:7, 8, NW) Kuomba, kutafuta, kubisha, vyote hivyo ni vitendo vya kuchukua hatua hakika. “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo.”—Mathayo 7:12.
Biblia yaonyesha kwamba wanafunzi wa Yesu pia walitetea kuishi kulingana na kanuni hii hii. (Warumi 15:2; 1 Petro 3:11; 3 Yohana 11) Ingawa hivyo, jambo lisilo la furaha ni kwamba hali iliyopo ya mahusiano ya kibinadamu yashuhudia kwamba, kwa kadiri kubwa, watu, wawe au wasiwe ni Wakristo wa jina, hawaifuati. Je! hii yamaanisha kwamba kanuni hii ya mwenendo wa kiungwana si halali tena? Je! labda ni kuukuu?
[Sanduku katika ukurasa wa 3]
“Fanyieni wanadamu wengine yote ambayo nyinyi mngetaka wao wawafanyie nyinyi.”—The Holy Bible, iliyotafsiriwa na R. A. Knox.
“Tendeeni wengine sawasawa na vile nyinyi mngependa kutendewa nao.”—The New Testament in Modern English, na J. B Phillips.
“Lolote lile ambalo nyinyi mwatamani kwamba wengine wangetenda kwa ajili yenu na kwa niaba yenu, nyinyi pia tendeni hivyo hivyo kwa ajili yao na kwa niaba yao. “—The Amplified New Testament
“Fanyieni wengine kila jambo ambalo nyinyi mwataka wao wawafanyie nyinyi.”—The New Testament in the Language of Today, na W F Beck
“Katika mambo yote basi, tendeeni wanadamu wenzenu kama vile nyinyi mngetaka wao wawatendee nyinyi.”—The Four Gospels, ilipotafsiriwa na E. V Rieu
“Ni lazima nyinyi mzoee kushughulika pamoja na wengine kama vile nyinyi mngependa wao washughulike pamoja na nyinyi.”—The New Testament na C B Williams