Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 1/1 kur. 16-17
  • Bonde la Ela—Mahali Ambapo Daudi Aliua Jitu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Bonde la Ela—Mahali Ambapo Daudi Aliua Jitu!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • “Vita Ni vya Yehova”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Daudi na Goliathi​—Je, Pigano Lao Lilikuwa Halisi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • “Vita Ni vya Yehova”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Kaa Katika “Bonde la Milima”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 1/1 kur. 16-17

Tamasha za Kutoka Lile Bara la Ahadi

Bonde la Ela​—Mahali Ambapo Daudi Aliua Jitu!

NI MASIMULIZI machache ya Biblia yaliyo ya kusisimua zaidi ya yale yenye kusimulia jinsi ‘Daudi kwa kombeo na jiwe alimshinda yule Mfilisti,’ Goliathi aliyekuwa jitu. (1 Samweli 17:50) Hiyo ilitukia katika Bonde la Ela.

Lakini bonde hilo liko wapi, nalo liko namna gani? Kujua hivi kutakuwezesha wewe ujaribu kuuona akilini ushindi huu wenye sifa alioupata kijulanga aliyepakwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli wa wakati ujao. Baadaye Mungu alifanya na Daudi agano la ufalme ambalo laweza kutuletea manufaa za milele, na jambo hili lapasa kutupa sisi sababu zaidi ya kujifunza yaliyotukia katika Bonde la Ela.

Wafilisti waliishi kandokando ya pwani ya Kanaani. Waisraeli walidhibiti milima ya Yudea (kusini ya Yerusalemu). Basi mambo yako hivyo​—adui wakiwa katika uwanda wa chini kuelekea magharibi, na watumishi wa Mungu wakiwa katika ile nchi iliyoinuka zaidi kuelekea mashariki. Kati yao lilikuwako jimbo lisilo la mtu lenye kufanyiwa ubishi, vile vilima vya chini vyenye kuitwa Shefela. Wafilisti wangeweza kushambuliaje Israeli? Njia ifaayo kufuatwa ilipanda juu kwenye wadi, au pitio, lililotoka mashariki kwenda magharibi, njia ile kuu ikiwa ndilo Bonde la Ela. Bonde hili lilienea kutoka nyanda za karibu na majiji ya Gathi na Ekroni, na kupanda juu kupitia Shefela, hadi kwenye milima iliyoko kilometa karibu 24 kusini-magharibi ya Yerusalemu na Bethlehemu. Ile picha (yenye kuonwa kwa kuelekea kusini-mashariki) yaonyesha mwisho wa upande wa juu wa bonde hili. Kwenye upeo wa macho waiona milima ya Yudea.a

Kwa kutazama foto hii, wazia Wafilisti wakiisha kuja huku kwenye bonde hili tambarare kuelekea ile milima. Ili kuwazuia, Waisraeli walikuja kusini-magharibi kutoka Yudea. Hapa pande zote mbili zikakaa katika hali ya kutokaribiana. Kwa nini? ‘Wafilisti walisimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli walisimama juu ya mlima upande huu, napo palikuwa na hilo bonde katikati.’​—1 Samweli 17:3.

Wewe jaribu kuona katika akili yako Wafilisti wakiwa juu ya kilima kilicho sehemu ya chini kulia, ingawa hatujui kikamili ni wapi hasa walipokuwa kandokando ya bonde hilo. Jeshi la Sauli lingaliweza kuwa lilikuwa ng’ambo ile ya kilima kule mbele ya shamba lile lenye rangi-rangi ya kahawia. Hakuna lolote la majeshi mawili hayo lililotaka kushuka, lipite katikati ya bonde, na kushambulia jeshi la upinzani likiwa katika mahali palo palipoinuka penye kinga salama. Tokeo hilo la kutokaribiana liliendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja. Kimya hicho kingemalizwa na nini?

Kila asubuhi na jioni Goliathi, bingwa Mfilisti aliyekuwa na urefu wa meta zaidi ya 2.7, alisimama katika bonde hilo akidhihaki vikali kambi ya Sauli ili waamue jambo hilo kwa pambano la mmoja kwa mmoja. Lakini hakuna Mwisraeli yeyote aliyethubutu kumjibu. Mwishowe, mchungaji kijana jina lake Daudi alikuja kutoka Bethlehemu akiwa na chakula kwa ajili ya ndugu zake walio kambini. Itikio lake likawa nini kwa dai lile lenye matukano? “Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?” (1 Samweli 17:4-30) Kwa uwazi Daudi alikuwa na maoni yenye kutokezwa katika andiko la kichwa ambacho Mashahidi wa Yehova wanacho kwa 1990: “Mwe wenye moyo mkuu na kusema: ‘Yehova ndiye msaidiaji wangu.’”​—Waebrania 13:6; Zaburi 56:11; 118:6, NW.

Mfalme Sauli aliposikia kwamba kijulanga huyu, ingawa hakuwa na silaha na hakuwa shujaa aliyezoezwa vita, angekabiliana na Goliathi mwenye kutia hofu, alifanya toleo ili deraya yake itumiwe. Daudi akakataa, akiwa na nia ya kwenda dhidi ya lile jitu akiwa na fimbo yake ya mchungaji, kombeo ya ngozi, na mawe matano aliyopata katika lile bonde. Mawe hayo yalikuwa kama nini? Haielekei yalikuwa vijiwe vya kikawaida tu vyenye ukubwa wa zabibu au zeituni. Yamepatikana mawe ya kombeo ambayo urefu wa mviringo wayo ni sentimeta 5 hadi 8, huo ukiwa ni ukubwa wa chungwa dogo. Mtumia-kombeo angeweza kurusha jiwe hilo kwa kasi za kuanzia kilometa 160 hadi 240 kwa saa moja.

Bila shaka wewe umesoma lililotukia humo chini katika bonde hilo, huku likionwa wazi kabisa na majeshi yote mawili. Daudi alijulisha wazi hivi: “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi nakujia wewe kwa jina la BWANA [Yehova, NW] wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.” Ndipo Yehova akatoa ushindi. Kijulanga huyo alilirusha kwa kani nyingi sana jiwe hilo la kombeoni hata likazama ndani ya kipaji cha uso wa Goliathi, likamuua. Ndipo mchungaji huyo akapiga mbio akipanda juu na kutumia upanga wa jitu hilo lenyewe kukata kichwa chalo.​—1 Samweli 17:31-51.

Kwa kutiwa moyo na imani na tegemeo la Daudi katika Mungu, Waisraeli walifukuza adui zao waliolegea roho, wakiwafuatia kwa kuteremka wakipita katika Shefela na mpaka mle ndani Filistia walikokuwa wametoka.​—1 Samweli 17:52, 53.

Fikiria ushangilio ambao ni lazima uwe ulisikiwa katika Yuda! Watu wa Mungu katika milima wangeweza kutazama magharibi chini ndani ya Bonde la Ela na Shefela, kama vile katika mwono ule wa ki-siku-hizi wa kutazama chini kutoka eneo lililo karibu na Hebroni. Yale maua meupe ya mti wa lozi yana uzuri wa kupendeza macho, lakini kupata ushindi juu ya adui za Mungu kulikuwa na uzuri mwingi zaidi. Wanawake Waisraeli wangeweza sana kusema: “Sauli amewaua elfu zake, na Daudi makumi elfu yake,” kutia na jitu lile ambalo yeye aliliangusha chini katika Bonde la Ela.​—1 Samweli 18:7.

[Maelezo ya Chini]

a Picha iyo hiyo imo katika 1990 Calendar of Jehovah’s Witnesses ikiwa kwa saizi kubwa, ambayo pia yapaonyesha mahali hapo katika ramani ya jalada.

[Picha katika ukurasa wa 17]

[Picha Hisani katika ukurasa wa 16]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki