Maisha na Huduma ya Yesu
Kristo Awasilipo Katika Mamlaka ya Ufalme
YESU angali pamoja na mitume wake juu ya Mlima wa Mizeituni. Katika kujibu ombi lao la ishara ya kuwapo kwake na umalizio wa mfumo wa mambo, sasa awaambia kielezi kilicho cha mwisho katika mfululizo wa vitatu. “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu [Mwana wa binadamu awasilipo, NW] katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye,” Yesu aanza, “ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.”
Wanadamu hawawezi kuona malaika katika utukufu wao wa kimbingu. Kwa hiyo kuwasili kwa Mwana wa binadamu, Yesu Kristo, pamoja nao malaika ni lazima kuwe kusikoonekana kwa macho ya kibinadamu. Kuwasili huko kwatukia katika mwaka 1914. Lakini kwa kusudi gani? Yesu aeleza hivi: “Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.”
Akisimulia litakalopata wale waliotengwa wawe upande wenye kupendelewa, Yesu asema hivi: “Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu [kuwekwa msingi wa ulimwengu, NW].” Kondoo hawatatawala pamoja na Kristo mbinguni bali watarithi Ufalme katika maana ya kuwa raia zao za kidunia. ‘Kuwekwa msingi wa ulimwengu’ kulitukia Adamu na Hawa walipozaa kwanza watoto ambao wangeweza kunufaika na uandalizi wa Mungu wa kufidia ainabinadamu.
Lakini kwa nini kondoo hutengwa wawe kwenye mkono wa kulia wenye upendeleo wa Mfalme? “Kwa maana nalikuwa na njaa,” mfalme ajibu, “mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.”
Kwa kuwa kondoo wapo duniani, wao wataka kujua ni jinsi gani wangeweza kuwa walifanya matendo mema jinsi hiyo kwa ajili ya Mfalme wao wa kimbingu. Wao wauliza, “Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?”
Mfalme ajibu, “Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.” Ndugu za Kristo ni waliosalia duniani kati ya wale 144,000 watakaotawala pamoja naye mbinguni. Na kuwafanyia mema, Yesu asema, ni sawa na kumfanyia yeye mema.
Mfalme awahutubia mbuzi, halafu. “Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.”
Hata hivyo, mbuzi walalamika hivi: “Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?” Mbuzi wahukumiwa vikali kwa msingi ule ule ambao kondoo wahukumiwa kwa njia yenye kupendeleka. “Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo [ndugu zangu],” Yesu ajibu, “hamkunitendea mimi.”
Kwa hiyo kuwapo kwa Kristo katika mamlaka ya Ufalme, kabla tu ya mwisho wa mfumo huu mbovu wa mambo katika dhiki kubwa, kutakuwa ni wakati wa hukumu. Mbuzi “watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele [kukatiliwa mbali kwa milele, NW]; bali wenye haki [kondoo] watakwenda katika uzima wa milele.” Mathayo 25:31-46; Ufunuo 14:1-3.
◆ Kwa nini ni lazima kuwapo kwa Kristo kuwe kusikoonekana, na ni kazi gani ambayo afanya wakati huo?
◆ Kondoo warithi Ufalme katika maana gani?
◆ ‘Kuwekwa msingi wa ulimwengu’ kulitukia wakati gani, na kwa nini wakati huo?
◆ Watu wahukumiwa kuwa kondoo au mbuzi kwa msingi gani?