Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 7/1 kur. 16-17
  • Yordani Ambayo Huenda Ikawa Huijui

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yordani Ambayo Huenda Ikawa Huijui
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Hula—Ile Dansi ya Hawaii
    Amkeni!—1995
  • Funzo Namba 1—Ziara Kwenye Bara Lililoahidiwa
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Njoo Uzuru Bahari ya Galilaya!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Kuvuka Mto Yordani
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 7/1 kur. 16-17

Mandhari za Kutoka Bara Lililoahidiwa

Yordani Ambayo Huenda Ikawa Huijui

MTAJO wenyewe wa Mto Yordani huenda ukakukumbusha mandhari ambazo wewe wazifahamu sana: Waisraeli chini ya Yoshua wakivuka sakafu yao iliyokaushwa maji karibu na Yeriko; Naamani akioga mara saba katika maji yao ili aponywe ukoma; Wayahudi wengi, halafu Yesu, wakija kubatizwa huko na Yohana.—Yoshua 3:5-17; 2 Wafalme 5:10-14; Mathayo 3:3-5, 13.

Kwa wazi, matukio yote haya maarufu yalitukia katika sehemu ile ndefu na yenye kujulikana vizuri zaidi ya Yordani, ile sehemu ya kusini ya Bahari ya Galilaya na kuteremka chini kwenye Bahari ya Ufu (ya Chumvi). Lakini wanafunzi wenye bidii nyendelevu wa Neno la Mungu huenda wakakosa kutazama sehemu nyingine ya Yordani—ile sehemu ya kaskazini ya mto na eneo layo lenye kuzunguka. Angalia ramani.a Lile jimbo la chini katikati ni sehemu ya lile Bonde Kuu la Ufa, ule mwatuko wa ardhi unaotandaa kutoka Siria (Shamu) hadi Afrika.

Vyanzo vikubwa vitatu vya Mto Yordani ni vijito ambavyo hutoka kwenye theluji inayoyeyuka kutoka Mlima Hermoni wenye kimo kirefu. Kile kijito cha mashariki kabisa (kilichoonyeshwa hapa) huibuka kutoka genge la mawe-chokaa karibu na sehemu ya chini ya mlima huo. Hapo ndipo Filipi Kaisaria ilipokuwa; kumbuka kwamba Yesu alizuru huko muda mfupi kabla hajageuzwa sura juu ya “mlima mrefu.” (Mathayo 16:13—17:2) Kijito kingine huibuka kutoka kwenye chungu ambapo jiji la Dani lilijengwa, ambamo Waisraeli wa ufalme wa kaskazini walisimamisha ndama wa dhahabu. (Waamuzi 18:27-31; 1 Wafalme 12:25-30) Kijito cha tatu huungana na hivyo viwili kuwa Mto Yordani, ambao huteremka chini meta zaidi ya 300 kwa mwendo wa karibu kilometa 11.

Halafu bonde hilo huwa tambarare na kuwa Bonde la Hula, likisababisha maji ya Yordani yaenee, yakifanyiza eneo pana lenye majimaji. Katika nyakati za kale mengi ya maji hayo yalikusanyika kuwa maji ya kina kidogo yajulikanayo kuwa Ziwa Hula (au Huleh). Lakini Ziwa Hula haliko tena kwa sababu katika nyakati za majuzi sehemu ya juu ya Yordani ilinyooshwa, mifereji iliongezwa kukausha eneo lile lenye majimaji, na kilango cha kutokea maji ya ziwa kiliongezewa kina. Hivyo, ukitazama ramani fulani ya eneo hilo na, kaskazini ya Bahari ya Galilaya, uone ziwa moja (Hula), utajua kwamba ramani hiyo ni ya jimbo hilo katika nyakati za kale, wala si ya vile utakavyolikuta leo.

Ingawa hivyo, ukizuru utakuta mbuga ya hifadhi ya kiasili ambayo yaweza kukupa wazo juu ya jinsi eneo hilo lilivyoonekana katika siku za Kibiblia, lilipokuwa makao ya namna maalumu za mimea, kama vile misitu yenye kuyumba-yumba ya mafunjo na matete.—Ayubu 8:11.

Eneo hilo lilikuwa makao yenye kukaliwa na ndege ambao walikuwa wa namna zenye kutofautiana daima. Kulasitara, korongo, miari, njiwa-turturi, na ndege wengine walikuwa tele, sababu kwa sehemu ikiwa kwamba lile bwawa lenye utopetope na lile ziwa lilikuwa eneo zuri kabisa la mapumziko likiwa katika njia ya mruko wa kuhama kati ya Ulaya na Afrika. (Kumbukumbu 14:18; Zaburi 102:6; Yeremia 8:7) Viumbe wengine wa eneo hilo wangalikuwa wasioonekana sana, lakini kuwapo kwao kulifanya Bonde la Hula liwe lisilopendeza kwa ziara. Yaelekea kwamba hao walikuwa ni kutia ndani simba, kiboko, jibwa-mwitu, na nguruwe-mwitu. (Ayubu 40:15-24; Yeremia 49:19; 50:44; Habakuki 1:8) Katika vipindi fulani malaria yenye kuletwa na mbu ilikuwako kwa wingi, kwa wazi hiyo ikiwa ni moja ya homa ambazo hutajwa katika Biblia.

Yaeleweka kwamba wasafiri mmoja mmoja na pia misafara mikubwa ingepita karibu na eneo hili lenye majimaji. Kwa hiyo wangeuvukia wapi Mto Yordani katika bonde hilo kaskazini ya Bahari ya Galilaya?

Karibu zaidi na Bahari ya Galilaya kulikuwako mchomozo wa miamba ya jiwe-basalti; kufanyika huko kwa hilo lililo kama bwawa la maji ndiko kulifanya maji yarudi nyuma na kufanyiza Ziwa Hula. Waweza kuona sehemu ya mchomozo huo katika ukurasa wa 16. Yordani utumbukiapo humu kusini ili kwenda kwenye Bahari ya Galilaya (yenye kuonekana kule mbali), husogea kwa haraka sana hivi kwamba matokeo huwa ni maji kuwa meupe. Kwa wazi, wasafiri wa kale wangaliona ikiwa hatari kushuka ndani ya kibonde hicho chenye kina kirefu na kuyavuka maji ya Yordani yenye kwenda haraka sana.

Kati ya lile eneo lenye majimaji la Bonde la Hula na kibonde hicho ulikuwako mwendo fulani wa eneo lenye usawa ambapo maji yalitiririka kwa utulivu. Hapo wasafiri wa kale wangeweza kwa usalama kuuvuka mto kwa miguu, napo pakawa sehemu ya njia kuu ya usafiri kupita katika Bara Lililoahidiwa. Sasa mahali hapo pana daraja, ambalo lingali mahali pakuu pa kuuvuka Yordani.

Leo Bonde la Hula ni eneo la ukulima lenye rutuba; hata kuna vidimbwi vya samaki. Yote hayo yamewezekana kwa sababu ya maji tele ambayo hutiririka kuteremkia sehemu hii ya Mto Yordani.

[Maelezo ya Chini]

a Linganisha ramani na picha kubwa zaidi katika 1990 Calendar of Jehovah’s Witnesses.

[Ramani katika ukurasa wa 17]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Hula

Bahari ya Galilaya

[Hisani]

Yategemea ramani ambayo haki ya unakili imetolewa na Pictorial Archive (Near Eastern History) Est. na Survey of Israel

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 17]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

Foto za Wanyama: Safari-Zoo of Ramat-Gan, Tel Aviv7

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki