Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 8/15 kur. 3-4
  • Je! Imani Katika Ajali Hutawala Maisha Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Imani Katika Ajali Hutawala Maisha Yako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Fungu la Dini
  • Kurusha Sarafu na Kusoma Nyota
  • Je, Maisha Yako Yameamuliwa Kimbele au Wapatwa na Tukio Tu?
    Amkeni!—1999
  • Je, Biblia Hufundisha Itikadi Katika Ajali?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Je! Ajali Itawale Maisha Yako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutafuta Mambo Yaliyokusudiwa Kimbele ya Mwanadamu
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 8/15 kur. 3-4

Je! Imani Katika Ajali Hutawala Maisha Yako?

MNAMO Septemba 1988 afa lilitokea. Maji yasiyozuilika katika delta pana ya mito Ganje na Brahmaputra yalipanda meta 9 na kuzamisha robo tatu za Bangladeshi. Maelfu walikufa maji. Wapatao 37,000,000 waliachwa bila makao. Kilometa zaidi ya 60,000 za barabara zilitokomea.

Kwa kuwa mafuriko hayo yamezonga Bangladeshi wakati kwa wakati, gazeti moja liliita nchi hiyo “Delta ya Maangamizi.” Usemi huo waonyesha ambayo watu wengi huona kuwa kisababishi cha maafa makubwa kama hayo: maangamizi, au ajali.

Ingawa huenda wengine wakahisi kwamba ajali haitawali maisha, maoni ya imani katika ajali yameenea tufe lote. Ni kwa nini wengi huamini ajali, na imani katika ajali ni nini?

Fungu la Dini

Neno la Kiingereza “fate” (Kiswahili, “ajali”) latokana na fatum la Kilatini, maana yake “yale yaliyokwisha semwa.”a Waamini-ajali huamini kwamba matukio huandikwa kimbele na kwamba binadamu hawana nguvu za kubadili mambo. Maoni hayo yameenezwa na dini mbalimbali na yameongoza mtazamo wa mamilioni ya waamini. Mtupio-macho wa dini tatu kubwa zaidi za ulimwengu huonyesha kwamba ajali ina sura mbalimbali—kuanzia maumbo ya mahekalu ya Uhindu, misikiti ya Uislamu, na makanisa ya Jumuiya ya Wakristo.

Mathalani, Waislamu wa ulimwengu wapatao milioni 900 hushikilia kwamba ajali (Kismet) huamuriwa na mapenzi ya kimungu.b Kurani hujulisha rasmi hivi: “Hakuna uovu unaotokea duniani . . . , ila ule unaokuwa ndani ya kitabu kabla sisi hatujautokeza.” “Na nafsi haitakufa ila kwa ruhusa yake Mungu; usemi huo umeandikwa.”—Sura 57:22; 3:145.

Karma ni sheria ya kisababishi na matokeo—uso mwingine wa ajali—inayoathiri maisha ya Wahindu wa ulimwengu karibu milioni 700. Hushikiliwa kwamba matukio yanayotokea katika uhai wa wakati huu wa Mhindu huamriwa na vitendo vyake katika maisha ya wakati uliopita katika umbo jingine. Garuda Purana, maandishi ya kale ya Uhindu, husema: “Matendo ya nafsi hii katika maisha ya wakati uliopita ndiyo yanayoamua asili ya mwili wayo katika yatakayofuata, na pia namna ya maradhi, yawe ni ya kimwili au kiakili, yatakayompata . . . Mtu hupata maishani mwake aliyojaliwa kupata.”

Vipi juu ya washiriki wanaokadiriwa kuwa milioni 1,700 wa Jumuiya ya Wakristo? Yawezekana, baadhi katika Jumuiya ya Wakristo huenda wakadai wamemweka Mungu badala ya ajali, na kadari (yaliyokwisha amuliwa na Mungu) badala ya imani katika ajali. Lakini Encyclopædia of Religion and Ethics yakiri hivi: “Haiwezi kusemwa kwamba Ukristo uko . . . huru kabisa na imani katika Ajali.” Madhehebu fulani zingali zataja imani ya mrekebishaji-dini wa karne ya 16, Martin Lutheri, ambaye wakati mmoja alitaarifu kwamba binadamu “hayuko huru sawa tu na kipande cha ubao, mwamba, kidonge cha udongo, au nguzo ya chumvi.”

Kurusha Sarafu na Kusoma Nyota

Ingawa maoni hayo ya ushupavu sasa yamechukua sehemu ya nyuma ya imani nyingi za madhehebu makubwa ya Jumuiya ya Wakristo, mwanatheolojia mmoja akubali kwamba wengi wa washiriki wayo wangali wanakubali imani hiyo ikiwa “imefanyizwa kuwa ya namna ya kilimwengu.” Katika namna hiyo, ajali yaweza kuwa na upendezi wa muda na kupewa jina bahati. Yawezekana wewe wajua juu ya wengi ambao pindi kwa pindi hutupa sarafu wakiomba bahati, au ajali. Ingawa huenda wakatetea hilo kuwa desturi tu, wao huendelea kufanya hivyo, na, nyakati nyingine, kwao hilo huonekana lina matokeo. Kwa kielelezo, The New York Times hivi karibuni liliripoti kwamba mwanamume mmoja anayeishi katika United States alipata upande wa sarafu wenye kichwa baada ya kununua tiketi za bahati nasibu. Yeye alisema: “Kila mara ambayo nimepata sarafu ikiwa upande wa kichwa, sikuzote jambo fulani zuri limenipata.” Katika pindi hii, alishinda dola milioni 25.7. Je! wewe wafikiri kwamba imani yake katika bahati, au ajali, imepungua?

Watu fulani hucheka juu ya kutupa juu sarafu. Hata hivyo, huenda wao wakaamini kwamba wakati ujao wao umekadariwa (umeamuliwa) na miendo ya nyota—uso mwingine wa ajali. Katika Amerika ya Kaskazini pekee, magazeti yapatayo 1,200 huwa na safu za unajimu. Kura fulani ya kutafuta maoni ilionyesha kwamba asilimia 55 ya vijana katika United States pekee huamini kwamba unajimu una matokeo.

Ndiyo, iwe yaitwa Kismet, Karma, Mungu, bahati, au nyota, imani katika ajali imeenea tufe na imefanya hivyo kwa vizazi vingi. Kwa kielelezo, je! ulijua kwamba kati ya watu wote wa kihistoria walioorodheshwa hapa, ni mmoja tu ambaye hakuamini katika ajali? Ni nani ambaye hakuamini hivyo? Na maoni yake juu ya ajali yaweza kubadilije yako?

[Maelezo ya Chini]

a The Encyclopedia of Religion, Buku 5, ukurasa 290, hutaarifu hivi: “AJALI. Kutokana na fatum la Kilatini (jambo lililonenwa, julisho rasmi la kiunabii, uaguzi, azimio la kimungu).”

b “Kismet hutofautiana na Ajali katika kule kurejezewa kwayo tu kuwa Mapenzi yenye uwezo wote; rufani yote ya kibinadamu dhidi ya yoyote yazo ni bure.”—Encyclopædia of Religion and Ethics ya Hasting, Buku 5, ukurasa 774.

[Sanduku katika ukurasa wa 4]

NI NANI WALIOAMINI KATIKA AJALI?

Maskari̇̄putra Gośāla

Walii wa Kihindi,

Karne ya 6/5 K.W.K.

Zeno wa Sitio

Mwanafalsafa Mgiriki,

Karne 4/3 K.W.K.

Publio Vergilio Maro

Mshairi Mroma,

Karne ya 1 K.W.K.

Yesu Kristo

Mwanzilishi wa Ukristo,

Karne ya 1 W.K.

Jahm, mwana wa Safwān

Mwalimu Mwislamu,

Karne ya 8 W.K.

John Calvin,

Mwanatheolojia na mrekebishi-dini Mfaransa, karne ya 16 W.K.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki