Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 2/15 kur. 8-9
  • “Hakika Huyu Alikuwa Mwana wa Mungu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Hakika Huyu Alikuwa Mwana wa Mungu”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Habari Zinazolingana
  • “Hakika Huyu Alikuwa Mwana wa Mungu”
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • “Hakika Mtu Huyu Alikuwa Mwana wa Mungu”
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Siku ya Mwisho ya Maisha ya Yesu ya Kibinadamu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Alikabiliana na Upanga wa Majonzi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 2/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

“Hakika Huyu Alikuwa Mwana wa Mungu”

YESU hajawa juu ya ule mti kwa muda mrefu wakati ambapo, katika mchana-kati, giza la kifumbo, lenye urefu wa saa tatu latukia. Halisababishwi na mpato wa jua, kwa kuwa mipato ya jua hutukia wakati wa mwezi mpya tu, na mwezi ni mpevu wakati wa Kupitwa. Zaidi ya hilo, mipato ya jua huwa ya dakika chache tu. Hivyo basi giza hili lina chanzo cha kimungu! Labda lawaachisha kidogo wale wanaomdhihaki Yesu, hata kusababisha dhihaka zao kali zikome.

Ikiwa ajabu hii yenye kutia woga yatukia kabla ya yule mtenda maovu mmoja kumtia adabu mwandamani wake na kumwomba Yesu amkumbuke, huenda hilo likawa ni jambo moja linaloleta toba yake. Labda ni wakati wa giza hilo kwamba wanawake wanne, yaani, mama ya Yesu na Salome dada yake, Mariamu Magdalene, na Mariamu mama ya mtume Yakobo Mdogo, wasogelea kuja karibu na mti wa mateso. Yohana, mtume mpendwa wa Yesu, yupo hapo pamoja nao.

Lo, jinsi moyo wa mama ya Yesu ‘wachomwa upande hadi upande’ atazamapo mwana aliyemlea na kumtunza kwa mapenzi akining’inia hapo kwa maumivu makali! Hata hivyo, Yesu afikiria, si maumivu yake mwenyewe, bali hali njema ya mama yake. Kwa jitihada kubwa, apunga kichwa chake kuelekea Yohana na kusema hivi kwa mama yake: “Mama [mwanamke, NW], tazama mwanao.” Halafu, akipunga kichwa kuelekea Mariamu, asema hivi kwa Yohana: “Tazama, mama yako.”

Kwa njia hiyo Yesu akabidhi utunzaji wa mama yake, ambaye ushuhuda waonyesha kwamba sasa yeye ni mjane, mikononi mwa mtume wake aliyependwa kipekee. Afanya hivi kwa sababu wana wengine wa Mariamu hawajadhihirisha bado imani katika yeye. Hivyo yeye aweka mfano mzuri wa kutoa riziki si kwa mahitaji ya kimwili tu ya mama yake bali pia kwa mahitaji yake ya kiroho.

Karibu saa tisa mchana, Yesu asema hivi: “Naona kiu.” Halafu, akihisi kwamba Baba yake ni kama ameondoa ulinzi kutoka kwake ili ukamilifu wake ujaribiwe kufikia kikomo, apaaza sauti hivi: “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Wasikiapo hivi, watu fulani waliosimama karibu wapaaza mshangao huu: “Tazama, anamwita Eliya.” Mara hiyo mmoja wao akimbia na, akitumia sifongo iliyofyonza divai chungu kwenye ncha ya kishina cha hisopo, ampa kinywaji. Lakini wengine wasema hivi: “Acheni; na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.”

Yesu apokeapo ile divai chungu, apaaza kilio hiki: “Imekwisha.” Ndiyo, amemaliza kila jambo ambalo Baba yake amemtuma duniani kulifanya. Mwisho, asema hivi: “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Kwa njia hiyo Yesu amkabidhi Mungu kani ya uhai wake kwa uhakika wa kwamba Mungu atamrudishia huo. Halafu ainama kichwa chake na kufa.

Yesu avutapo pumzi yake ya mwisho, tetemeko kali la dunia latukia, likipasua wazi matungamo-miamba. Tetemeko hilo lina nguvu sana hivi kwamba maziara ya ukumbusho nje ya Yerusalemu yaachwa wazi, na maiti zatupwa nje yayo. Wapita-njia, ambao waona miili mifu ambayo imefichuliwa wazi, waingia katika jiji na kuripoti jambo hilo.

Zaidi ya hilo, Yesu afapo, lile pazia kubwa sana ligawanyalo Patakatifu na Patakatifu Zaidi katika hekalu la Mungu lapasuliwa mara mbili, kutoka juu hadi chini. Kwa kuonekana pazia hili lililopambwa vizuri lina urefu wa kwenda juu wa meta 18 na ni zito sana! Mwujiza huo wa kushangaza sana si kwamba wadhihirisha hasira kali ya Mungu juu ya walioua Mwana Wake bali pia wamaanisha kwamba mwingilio wa kwenda Patakatifu Zaidi, mbinguni penyewe, sasa umewezeshwa na kifo cha Yesu.

Basi, watu hao wahisipo tetemeko hilo la dunia na kuona mambo yanayotendeka, wanaogopa sana. Ofisa wa jeshi mwenye kusimamia mambo kwenye ufishaji huo ampa Mungu utukufu. “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu,” atangaza. Yaelekea alikuwapo wakati dai la uana wa kimungu lilipozungumzwa kwenye jaribu la Yesu mbele ya Pilato. Na sasa yeye asadiki kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu, ndiyo, kwamba kweli yeye ndiye mwanamume mkubwa zaidi aliyepata kuishi.

Wengine pia washangazwa mno na matukio haya ya kimwujiza, nao wanaanza kurudi nyumbani wakijipiga vifua vyao, kama ishara ya kihoro na aibu yao nyingi sana. Wenye kutazama tamasha hii kwa mbali ni wanafunzi wa kike wa Yesu ambao waguswa kwa kina kirefu na matukio haya ya maana sana. Mtume Yohana yupo pia. Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49, UV; 2:34, 35, NW; Yohana 19:25-30, UV.

◆ Kwa nini mpato wa jua hauwezi kuwa ndio umesababisha zile saa tatu za giza?

◆ Muda mfupi kabla ya kifo chake, Yesu aweka mfano gani mzuri kwa ajili ya wale walio na wazazi wazee?

◆ Yesu asema nini mwishoni kabla hajafa?

◆ Tetemeko la dunia latimiza nini, na ni nini maana ya kupasuliwa kwa pazia la hekalu vipande viwili?

◆ Ofisa wa jeshi mwenye kusimamia mambo kwenye ufishaji huo aathiriwa jinsi gani na miujiza hiyo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki