Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 3/1 kur. 2-5
  • Suala Kubwa Hilo Ni Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Suala Kubwa Hilo Ni Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Lile Suala Kubwa
  • Mwanzo wa Ulimwengu Wote Mzima
  • Mwanzo wa Uhai
  • Kujibu Lile Suala
  • Je, Ulimwengu Ulitokea Wenyewe Tu, Au Uliumbwa?
    Amkeni!—1999
  • Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
  • Muumba Aweza Kufanya Maisha Yako Yawe na Maana Zaidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Tisho la Nyuklia Halijaisha
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 3/1 kur. 2-5

Suala Kubwa Hilo Ni Gani?

SUALA kubwa linalokabili kila mmoja wetu ni gani? Je! hilo ni ongezeko la usawa wa bahari na halihewa isiyo ya kawaida yenye kusababishwa na kuongezeka kwa ujotojoto wa tufe? Je! ni hali ya kupungua kwa tabaka ya gesi ozoni, inayoelekeza kwenye hali yenye hatari ya kuachwa wazi kwa mionzi-urujuani ya jua inayopenya kupita kiasi ikileta madhara? Je! ni ongezeko kubwa mno la idadi ya watu, ambalo linatia ndani matatizo mengine ya tufe lote, kama umaskini na uhalifu? Au ni tazamio la kuangamizwa kwa mamilioni wasiohesabika katika vita vya nyukilia, hatimaye waokokaji wowote wa maangamizi hayo wakifa katika maumivu makuu kutokana na baridi, kuwa na njaa, au nuru yenye kudhuru?

Katika 1989 gazeti Scientific American baada ya kuzungumza juu ya masuala hayo na mengine, lilimalizia hivi: “Uwezekano wa vita ya nyukilia bila shaka ni onyesho la hatari nzito iwezayo kuharibu . . . uendelevu wa uhai.” Kwa hiyo, je! vita ya nyukilia ni suala kubwa linalotukabili?

Lile Suala Kubwa

Kukiwa na badiliko katika hali ya kisiasa tangu 1989, haionekani kuwa vita ya nyukilia itatokea. Hata hivyo, maadamu silaha za nyukilia zingali ziko, zitawekea ainabinadamu tisho zito. Walakini, habari katika 1990 Britannica Book of the Year inaelekeza kwenye jambo jingine la hatari. Kwa kupatana na kitabu hicho cha marejezeo, zaidi ya milioni 230 ya wakaaji wa dunia ni wasioamini kwamba Mungu yuko. Vyanzo vingine vyaonyesha kwamba mamilioni wa kuongezea wanavutwa na falsafa za Mashariki ambazo zakubali maoni ya kwamba hakuna Muumba. Tena, ingawa mamia ya mamilioni huamini kwamba Muumba yuko, mawazo yao juu yake hutofautiana sana. Na katika visa vingi, vitendo vyao huleta shutumu juu ya yule wanayedai kumwabudu.—2 Petro 2:1, 2.

Ikiwa Mungu yuko—na kwa hakika yeye yuko—basi kwa kweli lile suala kubwa leo lazima limhusu. Kwa nini yeye aliumba ainabinadamu? Daraka letu kumwelekea ni lipi? Yeye ataitikiaje kwa jinsi mwanadamu anavyoiharibu dunia? Na yeye ataitikiaje ule mwito wa ushindani unaodokezwa kwa mkatao wa walio wengi sana kumwamini au kujitiisha kwa mapenzi yake? Kwa hakika, suala kubwa linalokabili kila mmoja wetu ni kama sisi hukubali au hukataa enzi kuu ya Mungu, “ambaye jina lake peke yake ni YEHOVA.”—Zaburi 83:18, King James Version.

Mwanzo wa Ulimwengu Wote Mzima

Naam, kwa wale wasioamini Mungu, wajibu wetu kwake si suala kubwa. Lakini yeyote ambaye aangalia ubuni na uzuri wa makao yetu ya kidunia kwa unyofu yeye alazimika kukubali kwamba lazima kulikuwa na Mbuni mkuu. Ni kweli kwamba katika kujaribu kueleza juu ya maajabu ya kiasili yanayotuzunguka, wanasayansi wengi hukosa kutaja Mungu. Kwa mfano, wengi husema kwamba ulimwengu wote mzima ulikua kufikia ukubwa wake wa sasa kutoka kwa kitu kilicho kidogo sana kuliko kichwa cha pini, kwamba hilo lilitokea “kiasili,” lenyewe tu, bila kuhitaji Muumba. Hata hivyo, baada ya kueleza nadharia yenye kujulikana sana juu ya jinsi ulimwengu wote mzima ulitokea, mwanafizikia Hanbury Brown, katika kitabu chake The Wisdom of Science, alikiri hivi: “Nakisia kwamba, kwa watu walio wengi, hilo lingeonekana kuwa kiinimacho kuliko kuwa elezo.” Profesa Brown akata maneno kwamba “mwanzo na kusudi la ulimwengu” ni “mafumbo makubwa” ambayo sayansi yaonekana haiwezi kuyatatua.

Wanasayansi wameonyesha kwamba mata (asilivitu) na nishati (uwezo) zinalingana sana na kwamba mata inaweza kugeuzwa iwe nishati na nishati inaweza kugeuzwa iwe mata. Kama vile imeonekana katika milipuko ya kinyukilia, kiasi kidogo cha mata kinafananisha kiasi kingi cha nishati. Basi, je, chanzo cha nishati inayofananishwa na nyota milioni 100,000 katika galaksi yetu, na pia zile galaksi zaidi ya milioni 1,000 ambazo hufanyiza ulimwengu wote mzima unaoonekana, kiko wapi?

Biblia inasema hivi: “Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza [wingi wa nishati-msukumo, NW] wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.” Huyo ni nani? Biblia inarekodi jibu hivi: “Mimi ni BWANA [Yehova, NW]; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.”—Isaya 40:26; 42:5, 8.

Kisio kwamba dunia pamoja na ulimwengu wote mzima unaobaki zilitokea tu zenyewe linaondoa utukufu ambao ni wa Muumba, Yehova Mungu. (Ufunuo 4:11) Linaondoa pia kichocheo chenye nguvu kutenda kwa daraka kuelekea ulimwengu. Ikiwa wanadamu walifahamu kwamba wao wana wajibu kwa Mungu kwa yale wanayotendea uumbaji wake, ni yakini kwamba wangejali zaidi katika mambo kama uchafuzi wa hewa, uharibifu wa tabaka ya gesi ozoni, na kuongezeka kwa ujotojoto wa tufe.

Mwanzo wa Uhai

Fikiria pia swali hili: uhai ulianzaje? Watu wamefundishwa kwamba uhai ulianza bila Mungu kuhusika. Lakini hilo ni kinyume cha kanuni ya kisayansi ambayo ni thabiti. Wakati mmoja iliaminiwa kwamba mendemilia walitoka kwenye samadi ya ng’ombe, nyungunyungu walitoka kwenye nyama iliyooza, na panya wadogo walitoka kwenye matope. Hata katika pindi ya karne iliyopita, wanasayansi walifundisha kwamba vitu vidogo sana vyenye uhai vinatoka kwenye kitu kisicho na uhai. Lakini mawazo kama haya yalikanushwa na Redi, Pasteur, na wanasayansi wengine. The World Book Encyclopedia (chapa cha 1990) yataarifu hivi: “Baada ya majaribio ya Pasteur, wanabayolojia walio wengi walikubali wazo la kwamba uhai unatoka kwenye uhai ambao umekuwako.”

Hata hivyo, wanasayansi huwa na nadharia ya kwamba mambo yalikuwa tofauti zamani za kale. Wao husema kwamba viungohai vya kwanza vilitokea venyewe tu kutoka kwenye mchanganyiko usio hai wanaoita mchuzi wa zamani za kwanza (“primeval soup”), ambao ulikuwa na kemikali zenye kuhitajika kwa uhai. “Hiyo ilitokea yenyewe, yenyewe kabisa, kutoka mchuzi huo wa zamani za kwanza hadi kuwa binadamu,” ajulisha rasmi Christian de Duve katika A Guided Tour of the Living Cell.

Ikiongea juu ya Mungu, Biblia inasema hivi: “Kwako Wewe iko chemchemi ya uzima [uhai, NW].” (Zaburi 36:9) Taarifa hiyo inapatana kweli kweli na yale ambayo yameonwa—kwamba uhai unaweza kutoka kwenye uhai tu ambao ulikuwako hapo mbele. Hata hivyo, watu wengi hawaoni wajibu wowote kwa Mungu katika jinsi wanavyotumia maisha yao kwa kuwa mwelekeo wa sayansi ni wa kupendelea kuona uhai, ambao ni moja ya zawadi za Mungu yenye thamani nyingi, kuwa kitu ambacho kilitokea chenyewe tu. Hivyo, wao huvunja amri za Mungu, wakionea wenzao, wakiibia wenzao, wakiua wenzao, na wakitumia pesa, wakati, na ustadi mwingi katika kubuni silaha za ukatili ambazo zinaua na kuharibu kwa matokeo ya kuogopesha.

Kujibu Lile Suala

Zaidi ya wasioamini kwamba kuna Mungu na wenye kufuata desturi za siku hizi, kuna wengine wasiohesabika ambao hukana enzi kuu ya Mungu. Leo wengi sana hudai kuwa wanaamini juu ya Mungu, na zaidi ya milioni 1,700 hujiita Wakristo. Kwa karne nyingi makanisa ya Jumuiya ya Wakristo yamemtukuza Mungu waziwazi katika ibada zao. Lakini kwa kweli wengi wa hawa milioni 1,700 wanasimama upande gani wa jambo hili la enzi kuu ya Mungu?

Mtu mmoja mmoja na mataifa pia wameonyesha kutohusika na hilo kwa kwenda dhidi ya amri dhahiri za Mungu. Mataifa yanayodai kuwa Wakristo wamefanya vitendo vya kutomhofu Mungu vya jeuri, kutia ndani vile vita viwili vibaya zaidi katika historia ya binadamu—na makasisi “Wakristo” kutoka pande zote mbili walibariki vita hivyo! Wamemwakilisha vibaya sana Mungu kwa unafiki kama huo. Ni kama vile Biblia inataarifu: “Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana.”—Tito 1:16.

Ingawaje, Mungu “hawezi kujikana mwenyewe.” (2 Timotheo 2:13) Lazima wakati uje ambapo yeye atajibu sehemu zote za suala hili la enzi kuu kupatana na kusudi lake lililoarifiwa hivi: “Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA [Yehova, NW].” (Ezekieli 38:23) Lakini kwa nini yeye amechukua muda mrefu? Hatimaye suala litajibiwaje? Na wewe wawezaje kufanya maamuzi yanayofaa katika jambo hili lenye maana sana?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Mandhari-nyuma ya Jalada: U.S. Naval Observatory photo

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Mandhari-nyuma: Picha ya U.S. Naval Observatory

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki