Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 9/1 kur. 3-4
  • Je, Kweli Kuna Matazamio Mazuri Kule Mbele?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kweli Kuna Matazamio Mazuri Kule Mbele?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuongeza Eneo Jipya
  • Utegemezo wa Kimungu?
  • ‘Na Ukuta Ukaanguka kwa Kishindo’
    Amkeni!—1992
  • Ulaya Iliyoungana—Kwa Nini Ni Jambo Linalopasa Kufikiriwa?
    Amkeni!—2000
  • Berlin—Wonyesho wa Jinsi Ulimwengu Wetu Ulivyo?
    Amkeni!—1991
  • Mashahidi wa Yehova Katika Ulaya Mashariki
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 9/1 kur. 3-4

Je, Kweli Kuna Matazamio Mazuri Kule Mbele?

“Huenda ukuta [wa Berlin] ukawa wenye kupisha mambo zaidi na zaidi wakati mahusiano ya Mashariki na Magharibi yaongezekapo. Lakini miaka, hata vizazi, vitapita, kabla haujabomolewa. Ujerumani zote mbili hazitaunganika tena kamwe.”

Ndivyo lilivyoandika gazeti moja la habari la Amerika katika Machi 1989. Siku zisizozidi 250—si miaka wala vizazi—baadaye, ukuta ulianza kuporomoka. Haipati majuma, maelfu ya sehemu za ukuta huo, sasa zikiwa zimepunguziwa umaana zikiwa makumbusho tu, zilikuwa zikitumiwa kuwa mapambo ulimwenguni pote.

PAZIA la Chuma lenye kutu nyingi lilikuwa limegawanyika hatimaye, likichochea matumaini kwamba hatimaye amani na usalama wa ulimwenguni pote ulikuwa karibu. Hata Vita ya Ghuba katika Mashariki ya Kati haikufifisha tumaini kwamba ushindani wa muda mrefu kati ya Mashariki na Magharibi ulikuwa umeisha, na utengemano mpya wa ulimwengu ulikuwa karibu.

Kuongeza Eneo Jipya

Tangu vita ya ulimwengu ya pili, mwendo kuelekea Ulaya iliyounganika umekuwa dhahiri. Katika 1951, nchi za Ulaya ya Magharibi zilianzisha Jumuiya ya Ulaya ya Makaa-Mawe na Chuma cha Pua. Katika 1957 hiyo ilifuatwa na Soko la Kishirika la Ulaya. Katika 1987 nchi 12 za jumuiya hiyo ya kimataifa (sasa yenye idadi ya watu milioni 342) inaweka mradi wa kupata umoja kamili wa kiuchumi kufikia 1992. Hata umoja kamili wa kisiasa waonekana sasa kuwa uwezekano thabiti. Hilo ni badiliko lenye kuburudisha kama nini kutoka historia ya Ulaya yenye hatia ya kumwaga damu ya miaka iliyopita!

Hata hivyo, kwa sababu ya mabadiliko ya kisiasa ya hivi karibuni, mwaka 1992 unazidi kuwa na maana. Kisio limeongezeka kwamba nchi zilizokuwa za Kikomunisti za Ulaya Mashariki huenda pia zikatiwa hatimaye katika Ulaya iliyounganika.

Utegemezo wa Kimungu?

Baadhi ya vikundi vya kidini, vikipuuza kanuni ya kutokuwamo kwa Kikristo, viliruhusu kushindwa kwa dini kwa miongo mirefu katika Ulaya Mashariki kuvisukume katika kujihusisha sana na siasa. Likieleza juu ya hilo, gazeti la habari la Kijerumani Frankfurter Allgemeine Zeitung linaonyesha kwamba “hakuna ubishi kwamba Wakristo wamesaidia kuleta mabadiliko katika Mashariki,” likiongeza kwamba “hakika sehemu waliyoshiriki haipasi kupunguziwa thamani.” Linazidi kueleza hivi: “Kwa mfano, katika Polandi dini ilijiunga yenyewe na taifa, na kanisa likawa adui mkaidi wa chama kilichokuwa kikitawala; katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani (GDR) [iliyokuwa Ujerumani Mashariki] kanisa liliandaa mahali pa utendaji kwa watu wenye maoni ya ukaidi likawaruhusu kutumia majengo ya kanisa kwa shughuli za kitengenezo; katika Chekoslovakia, Wakristo na Wademokrasi walikutana gerezani, wakaja kuthaminiana, na hatimaye wakaungana.” Hata katika Romania ambako “makanisa yalithibitika kuwa wafuasi waaminifu wa utawala wa Ceauşescu,” uwezekano wa kukamatwa kwa kasisi Laszlo Tökes (Lazlou Toukesi) ndio uliosababisha mapinduzi.

Vatikani ilihusika pia. Gazeti Time lilieleza hivi katika Desemba 1989: “Ingawa sera ya Gorbachev ya kuondoa mamlaka yake ilikuwa ndicho kisababishi cha mara moja cha mfululizo wa uhuru uliokuja ghafula kotekote Ulaya Mashariki katika miezi michache iliyopita, John Paul anastahili kusifiwa sana kwa jitihada ya wakati mrefu zaidi. . . . Katika miaka ya 1980 hotuba zake zilikazia sana wazo la Ulaya iliyounganika kutoka Atlantiki hadi milima Urali ikiwa imepuliziwa roho na imani ya Kikristo.” Hivyo, kwa mfano, alipokuwa akizuru Chekoslovakia katika Aprili 1990, papa alionyesha tumaini la kwamba ziara yake ingefungua milango mipya kati ya Mashariki na Magharibi. Alitangaza mkutano uliopangwa wa maaskofu wa Ulaya ili kutafuta maarifa ya kutimiza njozi yake ya “Ulaya iliyounganika juu ya msingi wa asili zayo za Kikristo.”

Je! inawezekana kwamba Ujerumani iliyounganika iliyo ndani ya mfumo wa Ulaya iliyounganika yaweza kuthibitika kuwa mwanzo wa Ulaya iliyounganika kikamili, na kisha hata wa ulimwengu uliounganika? Je! kuhusika kwa dini hakuonyeshi kwamba Biblia inaahidi hilo? Kwa uhakika, makasisi katika Mashariki na Magharibi pia wakiwa wanatenda sasa katika mfumo wa kisiasa kwa ajili ya amani na usalama, je, tusingeweza kutazamia hilo kuwa jambo halisi karibuni? Ebu tuone.

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 4]

Kanisa la Kiprotestanti la Nikolai katika Leipzig—ishara ya mabadiliko ya kisiasa katika Ujerumani

Mataifa yanayoshiriki katika Soko la Kishirika la Ulaya

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki