Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 2/15 kur. 3-4
  • Kuzipa Sanamu Heshima Kibishanio

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuzipa Sanamu Heshima Kibishanio
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Waikonoklasti (Wavunja Sanamu)
  • Je! Sanamu Zaweza Kukuleta Karibu Zaidi na Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Sanamu
    Amkeni!—2014
  • Maoni ya Kikristo Juu ya Mifano
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Je, Tumwabudu Mungu Kupitia Sanamu?
    Amkeni!—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 2/15 kur. 3-4

Kuzipa Sanamu Heshima Kibishanio

MAHALI fulani katika Polandi, mtu mmoja yu tayari kwa ajili ya safari yake. Hata hivyo, ni lazima bado ashughulikie jambo moja lenye maana. Apiga magoti mbele ya sanamu ya Yesu, afanya utoaji, na kusali apate ulinzi katika safari zake.

Umbali wa maelfu ya kilometa kutoka hapo, katika Bangkok, Thailandi, waweza kushuhudia sikukuu ya kwanza ya kawaida ya kila mwaka ya Kibuddha, wakati wa mwezi mpevu katika Mei. Katika sikukuu hiyo sanamu ya Buddha hubebwa katika mwandamano kotekote barabarani.

Bila shaka wafahamu kwamba kuzipa sanamu heshima, kama ilivyoelezwa, kumeenea kotekote. Kwa halisi mabilioni ya watu husujudu mbele ya sanamu. Kwa mileani kadha sanamu zimeonwa kuwa njia ya maana ya kumkaribia Mungu zaidi.

Wewe wafikirije kuhusu matumizi ya sanamu katika ibada? Je! kuzipa sanamu heshima kunafaa au hakufai? Mungu huhisije juu ya hilo? Je! kuna ushuhuda wowote kwamba yeye hukubali ibada ya jinsi hiyo? Labda hujapata kamwe kuyafikiria sana kibinafsi maswali kama hayo. Hata hivyo, ikiwa unathamini kuwa na uhusiano pamoja na Mungu, unahitaji kupata majibu kwayo.

Kwa kweli, hilo limekuwa jambo lisilo rahisi kusuluhisha kwa wengi. Kwa hakika, imekuwa habari ya kubishaniwa vikali na nyakati nyingine kwa jeuri kwa maelfu ya miaka. Kwa mfano, nyuma katika mwaka wa 1513 K.W.K., kiongozi Mwebrania Musa aliharibu sanamu ya dhahabu ya ndama na akaamuru watu 3,000 hivi waliokuwa wakiiheshimu wauawe kwa upanga.—Kutoka, sura 32.

Upinzani thabiti dhidi ya matumizi ya sanamu za kidini haujawa kwa Wayahudi tu. Wanahistoria wa kilimwengu wa kale wamehifadhi hekaya ya Takhmūrūp, mtawala Mwajemi anayesemwa kuwa alifanya kampeni nyingi dhidi ya kuzipa sanamu heshima mamia ya miaka kabla ya Musa. Katika China mfalme asemwaye kuwa aliishi zamani za kale aripotiwa kuwa alianzisha shambulio la kijeshi dhidi ya sanamu-umbo za miungu mbalimbali. Baada ya sanamu hizo kuharibiwa, alishutumu kuheshimu miungu waliofanyizwa kwa udongo kuwa upumbavu. Baadaye, Muhamadi alipokuwa yungali mtoto, kulikuwako Waarabu waliopinga matumizi ya sanamu katika ibada. Uvutano wao juu ya Muhamadi ulichangia msimamo wake kuhusu ibada ya sanamu katika miaka iliyofuata. Katika Kurani, Muhamadi afundisha kwamba ibada ya sanamu ni dhambi isiyoweza kusamehewa, kwamba waabudu sanamu hawapaswi kuombewa, na kwamba ndoa pamoja na waabudu sanamu yakataliwa.

Hata katika Jumuiya ya Wakristo watu mashuhuri wa dini wa karne za pili, tatu, nne, na tano W.K., kama vile Irenayo, Origeni, Eusebio wa Kaisaria, Epifanio, na Augustino, walipinga matumizi ya sanamu katika ibada. Karibu na mwanzo wa karne ya nne W.K., katika Elvira, Hispania, kikundi cha maaskofu kilitunga maazimio kadha ya maana dhidi ya kuzipa sanamu heshima. Hilo Baraza la Elvira lililokuwa maarufu lilitokeza kupigwa marufuku sanamu kutoka makanisa na kuwekwa kwa adhabu kali dhidi ya waabudu sanamu.

Waikonoklasti (Wavunja Sanamu)

Matukio hayo yalitayarishia njia kimojawapo vibishanio vikubwa sana vya historia: kibishanio cha kiikonoklasti cha karne za nane na tisa. Mwanahistoria mmoja ataarifu kwamba “kibishanio hicho kikali kilidumu kwa muda wa karne moja na nusu, na kikaleta kuteseka kwingi sana” na kwamba kilikuwa “mojawapo visababishi hasa vya mgawanyiko ulio kati ya milki za Mashariki na Magharibi.”

Neno “ikonoklasti” latokana na maneno ya Kigiriki eikon, likimaanisha “sanamu,” na klastes, likimaanisha “mvunja.” Kwa kupatana na jina yalo, harakati hiyo dhidi ya sanamu ilitia ndani kuondoa na kuharibu sanamu kotekote Ulaya. Sheria kadha za kupinga sanamu zilifanyizwa ili kuondolea mbali matumizi ya sanamu katika ibada. Kuzipa sanamu heshima kukawa suala motomoto la kisiasa lililovuta maliki, mapapa, majemadari, na maaskofu katika vita halisi ya kitheolojia.

Na hiyo haikuwa vita ya maneno tu. Cyclopedia of Biblical, Theological, na Ecclesiastical Literature, ya McClintock na Strong, yataarifu kwamba baada ya Maliki Leo wa 3 kutoa amri dhidi ya matumizi ya sanamu katika makanisa, “makutano ya watu walipinga amri hiyo, na misukosuko yenye jeuri, hasa katika Konstantinopo,” ikawa tukio la kila siku. Mapigano kati ya majeshi ya kifalme na watu yalitokeza mauaji na machinjo ya wengi. Watawa-waume walinyanyaswa kikatili. Mamia ya miaka baadaye, katika karne ya 16, majadiliano kadha ya peupe yalifanywa katika Zurich, Uswisi, kuhusu suala la sanamu katika makanisa. Tokeo likawa kwamba, amri iliyoshurutisha kuondolewa kwa sanamu zote kutoka kwa makanisa ikatolewa. Warekebishaji wengine wa kidini walikuwa maarufu kwa ajili ya malawama yao makali na mara nyingi ya jeuri dhidi ya ibada ya sanamu.

Hata leo kuna mtengano mkubwa miongoni mwa wanatheolojia wa ki-siku-hizi kuhusu matumizi ya sanamu katika ibada. Makala ifuatayo itakusaidia ukadirie kama sanamu zaweza kwa kweli kumsaidia mwanadamu amkaribie Mungu zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki