Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 7/1 kur. 24-25
  • Beer-sheba Mahali Ambapo Kisima Kilimaanisha Uhai

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Beer-sheba Mahali Ambapo Kisima Kilimaanisha Uhai
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Jitihada Nyingi Zinahitajiwa Ili Kuendeleza Ibada ya Kweli
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Maji Yanayobubujika Ili Kutokeza Uzima wa Milele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Aliandalia Israeli Katika Sinai
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 7/1 kur. 24-25

Mandhari Kutoka Bara Lililoahidiwa

Beer-sheba Mahali Ambapo Kisima Kilimaanisha Uhai

“TOKEA Dani mpaka Beer-sheba.” Hilo ni fungu la maneno linalojulikana sana kwa wasomaji Biblia. Linasimulia Israeli yote, kutoka Dani, karibu na mpaka wa kaskazini, hadi Beer-sheba, kusini. Amani ya utawala wa Sulemani ilielezwa hivi: “Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.”—1 Wafalme 4:25; Waamuzi 20:1.

Lakini, tofauti kati ya Dani na Beer-sheba, zilihusisha zaidi ya umbali kati yao. Kwa kielelezo, Dani lilipata mvua ya kutosha; maji yalitiririka kutoka ardhini kufanyiza chanzo kimoja cha Mto Yordani, kama ionwavyo katika picha iliyo kulia. Beer-sheba lilikuwa tofauti kama nini, kwani lilikuwa katika eneo kavu, kati ya pwani ya bahari na sehemu ya kusini ya Bahari ya Chumvi.

Katika eneo la Beer-sheba, kiasi cha mvua cha kila mwaka kilikuwa kutoka sentimeta 15 hadi 20 tu. Ukijua hilo, angalia picha iliyo juu ya kilima, au mwinuko, wa Beer-sheba.a Rangi ya kijani kibichi unayoona inaonyesha kwamba picha hiyo ilichukuliwa baada ya mvua ya kiasi tu ya wakati wa kipupwe, wakati mashamba yanayozunguka Beer-sheba yanapokuwa mabichi kwa muda mfupi. Nyanda za karibu zilikuwa—na zingali—nzuri kwa mimea ya nafaka.

Kwa sababu eneo hilo lilikuwa kavu, masimulizi ya Biblia juu ya Beer-sheba yanakazia visima na haki za maji. Jiji hilo lilikuwa karibu na barabara au njia za misafara zilizovuka jangwa la kusini zaidi. Kama vile uwezavyo kuwazia, wasafiri waliopitia au kutua hapo wangehitaji maji kwa ajili yao na kwa ajili ya wanyama wao. Maji hayo hayakububujika kutoka ardhini, kama vile katika Dani, lakini yangeweza kupatikana kutoka visimani. Kwa kweli, neno la Kiebrania beʼerʹ lilirejezea shimo au tundu lililochimbwa ili kufikia ugavi wa maji wa chini ya ardhi. Beer-sheba lamaanisha “Kisima cha Kiapo” au, “Kisima cha Saba.”

Abrahamu na familia yake walikaa katika Beer-sheba na karibu na hapo kwa muda mrefu, na walijua umaana wa visima. Hagari mjakazi wa Sara alipokimbia hadi jangwani, huenda ikawa alipanga kupata maji kutoka katika visima au kutoka Wabeduini wanaovitumia—kama vile huyo mwanamke Mbeduini aliye kwenye ukurasa ufuatao, juu, anayechota maji kwenye kisima katika Peninsula ya Sinai. Baadaye Abrahamu alipolazimika kumfukuza Hagari pamoja na mwana wake mwenye matusi, yeye aliandaa kwa fadhili ugavi wa maji. Nini lilitukia mara maji hayo yalipoisha? “Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.”—Mwanzo 21:19.

Abrahamu alipata wapi maji ya kujaza kiriba cha Hagari? Labda kutoka katika kisima alichokuwa amechimba, ambacho alipanda mkwaju karibu nacho. (Mwanzo 21:25-33) Yaweza kusemwa kwamba wanasayansi sasa wanaona jinsi chaguo la Abrahamu la mkwaju lilivyofaa, kwani mti huo una majani madogo yanayopoteza kiasi kidogo cha unyevu, kwa hiyo unaweza kusitawi ijapokuwa ukavu wa eneo hilo.—Ona picha iliyo chini.

Kuchimba kisima kwa Abrahamu kulitajwa kuhusiana na bishano kati yake na mfalme mmoja Mfilisti. Kisima kilikuwa mali yenye thamani kwa sababu ya upungufu wa ujumla wa maji na kazi ngumu iliyohitajiwa ili kuchimba kisima kirefu. Kwa kweli, hapo nyuma, kutumia kisima bila ruhusa kulikuwa kuvamia haki za mali.—Linganisha Hesabu 20:17, 19.

Ukizuru Kilima cha Beer-sheba, waweza kutazama chini ya kisima kirefu kwenye mteremko wa kusini-mashariki. Hakuna ajuaye wakati kilipochimbwa mara ya kwanza kupitia mwamba thabiti na sehemu yacho ya juu (inayoonwa chini) ikaimarishwa kwa mawe. Wanaakiolojia wa kisasa walikichimba hadi meta 30 chini bila kufikia sehemu yacho ya chini. Mmoja wao alionelea hivi: “Inashawishi kukata maneno kwamba kisima hiki kilikuwa . . . ‘Kisima cha Kiapo’ ambapo Abrahamu na Abimeleki walifanya agano lao.”—Biblical Archaeology Review.

Kwa wazi Beer-sheba liliongezeka ukubwa baadaye katika kipindi cha Kibiblia, likija kuwa jiji lenye ngome na lenye lango kubwa. Lakini ufunguo wa kuwako na kufanikiwa kwalo ulikuwa yale maji muhimu kutoka katika kisima chalo kirefu.

[Maelezo ya Chini]

a Ili kuona kwa ukubwa zaidi Kilima cha Beer-sheba, ona 1993 Calendar of Jehovah’s Witnesses.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki