Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 10/15 kur. 3-4
  • Kwa Nini Kuiba Kwaongezeka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Kuiba Kwaongezeka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Watu Huiba?
  • Usiibe
  • Kwa Nini Nisiibe?
    Amkeni!—1995
  • Je, Umaskini Ni Sababu Halali ya Kuiba?
    Amkeni!—1997
  • Kwa Nini Watu Huiba Vitu Dukani?
    Amkeni!—2005
  • Usiwe Mwizi Kamwe!
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 10/15 kur. 3-4

Kwa Nini Kuiba Kwaongezeka?

RIO DE JANEIRO—Jumapili, Oktoba 18, 1992. Fuko maarufu za Kopakabana na Ipanema zimejaa watu. Kwa ghafula, magenge ya vijana washambulia fuko hizo, wakipigana wao kwa wao na kuiba kitu chochote chenye thamani kutoka kwa watu walio ufukoni. Polisi walio wachache kuliko vijana hao wasimama kando—wasiweze kusaidia. Kwa Wakarioka (wakaaji wa hapo) na watalii, hilo ni jinamizi la mchana.

Kwa kweli, uhalifu unaohusisha mali umekuwa jambo la kawaida. Katika majiji makubwa, yajulikana kwamba wezi huwaibia vijana—na hata kuwaua nyakati nyingine—ili kupata viatu vyao vya mchezo. Wezi huingia nyumba za watu wawe wamo ndani, au la. Baada ya kujua mahali ambapo vitu huwekwa katika nyumba, watunza-nyumba wa kike wasiofuatia haki, huiba vito na fedha, halafu hutoroka. Misongamano ya watu hupora maduka. Vikundi vilivyopangwa vema huiba hata watu, kama inavyoonwa kutokana na idadi zilizoongezeka za watu walioibwa katika Brazili. Na labda ungeweza kutoa vielelezo vingine kutokana na mambo uliyojionea mwenyewe au kutokana na yale ambayo yametokea katika jumuiya yako. Lakini kwa nini kuna kuiba kwingi sana?

Kwa Nini Watu Huiba?

Ingawa umaskini wenye kuongezeka na matumizi ya dawa za kulevya ni sababu mbili kuu, jibu si dhahiri hivyo. The New Encyclopædia Britannica yaonelea hivi: “Utafutaji-tafutaji wa sababu moja tu ya uhalifu umeachwa hasa kwa sababu ya kukosa matokeo.” Hata hivyo, kitabu icho hicho chadokeza kwamba matatizo kama vile kuiba “huonwa kuwa tokeo la moja kwa moja la hali ya vijana ya kuhisi kutokufaa kitu na kuchukizwa kwa sababu ya kutohusishwa katika matimizo ya kimwili na thawabu za maisha ya kawaida.” Naam, kwa sababu ya ule msongo mwingi wa kupata vitu vya kimwili, wengi huona kwamba hawawezi kuvipata vitu wanavyotamani bila kuiba.

Lakini kwa kupendeza, The World Book Encyclopedia yaonyesha kwamba: “Kiwango cha uhalifu huwa thabiti kwa kulinganishwa katika jamii za kitamaduni ambazo katika hizo watu huamini kwamba njia yao ya maisha itaendelea. Viwango vya uhalifu huelekea kuongezeka katika jamii zilizo na mabadiliko ya upesi kuhusiana na mahali ambapo watu huishi na kazi wanayofanya ili kupata riziki—na kuhusiana na matumaini yao juu ya hali yao njema ya wakati ujao.” Ensaiklopedia hiyo yaongeza hivi: “Vijana wana fursa chache zaidi za kupata kazi. Kazi zinazopatikana ambazo hazihitaji ustadi zaonekana kuwa bila ladha zinapolinganishwa na zile faida za haraka na zenye kusisimua zinazotokana na wizi. Vijana wako tayari zaidi pia kukabili hatari ya kukamatwa kwa sababu hawana mengi ya kupoteza.”

Lakini, wengi wasio na kazi ya kuajiriwa au walio na kazi zenye mshahara wa chini hawaibi, ilihali idadi kubwa-kubwa za wafanyakazi wa ofisini na wafanyakazi wa mikono huiba kidogo-kidogo na mara kwa mara wakiwa kazini kana kwamba vitu wanavyoiba ni sehemu ya mshahara wao. Kwa kweli, cheo fulani cha kijamii chahitajiwa kwa mazoea fulani ya upunjaji. Je! hujapata kusikia kashfa zinazohusisha fedha nyingi sana ambazo katika hizo wale walioshtakiwa ni wanasiasa, wafanyakazi wa umma, na wanabiashara? Pasipo shaka, kuiba si tendo la walio maskini tu.

Kumbuka pia, mara nyingi sinema na programu za televisheni huonyesha kuiba kwa njia ya ucheshi (na huenda hata shujaa akawa ni mwizi), jambo linaloelekea kufanya wizi ukubalike zaidi. Ni kweli kwamba, kutazama hizo kwaweza kuitwa kitumbuizo, lakini wakati uleule, watazamaji huonyeshwa jinsi ya kuiba. Je! hilo haliwasilishi kwa hila lile wazo kwamba labda uhalifu wastahili? Bila shaka, pupa, uvivu, na wazo la kwamba kila mtu hufanya hivyo bila hofu ya kuadhibiwa, vyote huchangia ongezeko la kuiba. Kwa kweli, twaishi katika zile “nyakati za hatari” zilizotabiriwa ambazo katika hizo kujipendeza na kupenda fedha kwaenea.—2 Timotheo 3:1-5.

Usiibe

Zijapokuwa kanuni za ulimwengu zilizopotoka, ni muhimu kutii amri hii: “Mwibaji asiibe tena.” (Waefeso 4:28) Mtu anayependa mali au anasa kupita kiasi aweza kujidanganya mwenyewe aamini kwamba wizi wastahili chochote kiwezacho kumpata. Lakini kuiba ni jambo zito machoni pa Mungu na kwafunua kwamba mtu hampendi mwanadamu mwenzake. Isitoshe, hata kuiba vitu vidogo-vidogo kwaweza kumwongoza mtu awe na moyo sugu. Na namna gani kuonwa kuwa mtu asiyefuata haki? Ni nani anayeweza kumtumaini mwizi? Kwa hekima, Neno la Mungu husema hivi: “Mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya.”—1 Petro 4:15.

Bila shaka wewe wachukizwa na ongezeko la kuiba, lakini watu walio katika sehemu zenye uhalifu mwingi sana hukabilianaje? Wale waliokuwa wezi wamebadilije mtindo-maisha wao? Je! kuiba kutaisha wakati wowote ulimwenguni pote? Twakualika uisome makala ifuatayo, “Ulimwengu Bila Wezi.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki