Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 11/15 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Habari Zinazolingana
  • “Kuhani Milele kwa Mfano wa Melkizedeki”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
  • Je! Tunahitaji Ukuhani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Tamati Inayokuja ya “Kitabu cha Vita vya Yehova”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kitabu cha Biblia Namba 58—Waebrania
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 11/15 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Kwa kuwa yule kuhani wa kale aliyeitwa Melkizedeki alikuwa binadamu halisi, kwa nini Biblia husema kwamba alikuwa “hana wazazi [nasaba, ‘NW’]”?

Taarifa hiyo imetolewa kwenye Waebrania 7:3. Angalia mstari huo katika muktadha wao:

“Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu [Abrahamu, NW] alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake la kwanza ni mfalme wa haki [uadilifu, NW], tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi [nasaba, NW], hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.”—Waebrania 7:1-3.

Kama ilivyotajwa, Melkizedeki alikuwa binadamu halisi, kama vile Abrahamu, aliyeshughulika naye moja kwa moja, alivyokuwa halisi. (Mwanzo 14:17-20; Waebrania 7:4-10) Ikiwa hivyo, ni lazima iwe Melkizedeki alikuwa na wazazi, baba na mama, na huenda ikawa alikuwa na wazao. Kwa hiyo, akiwa binadamu alikuwa na nasaba, au ukoo. Alikufa pia. Kufikia wakati fulani Melkizedeki alikufa, kulingana na taarifa ya Paulo kwenye Warumi 5:12, 14. Lakini kwa kuwa hatujui wakati Melkizedeki alipokufa na hivyo akaacha kutumikia akiwa kuhani, kwa njia hiyo yeye alitumikia bila mwisho wowote unaojulikana.

Katika Waebrania, Paulo alieleza juu ya Melkizedeki alipokuwa akizungumza juu ya daraka la Yesu Kristo akiwa Kuhani Mkuu aliye bora zaidi. Akimrejezea Melkizedeki kuwa mfano, au kigezo, cha Yesu katika daraka hilo la kikuhani, Paulo alisema hivi: “Yesu . . . amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.” (Waebrania 6:20) Katika maana gani?

Ni lazima iwe Paulo aling’amua kwamba rekodi ya Biblia haitoi maelezo mengi juu ya nasaba ya familia ya Melkizedeki—wazazi wake wa kale au wowote wawezao kuwa wazao wake. Habari hiyo si sehemu hata kidogo ya rekodi ya Kibiblia. Kwa hiyo, kutokana na yale ambayo Paulo alijua au yale ambayo twajua, Melkizedeki angeweza kusemwa kwa usahihi kuwa “bila nasaba” (New World Translation of the Holy Scriptures; American Standard Version), “bila jedwali ya uzao” (W. J. Conybeare), au “bila ukoo.”—J. B. Phillips.

Yesu alikuwa hivyo kwa njia gani? Kwa kweli, twajua kwamba Baba ya Yesu alikuwa Yehova Mungu na kwamba mama yake wa kibinadamu alikuwa Mariamu wa kabila la Yuda. Bado, kulikuwa ufanano kati ya Melkizedeki na Yesu. Jinsi gani? Yesu hakuzaliwa katika kabila la Lawi, lile kabila la makuhani katika taifa la Israeli. La, Yesu hakuwa amekuwa kuhani kupitia nasaba ya kibinadamu. Wala Melkizedeki, ambaye hakuwa amekuwa kuhani “kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili,” yaani, kwa kuzaliwa katika kabila na familia ya kikuhani. (Waebrania 7:15, 16) Badala ya kuwa kuhani kupitia baba wa kibinadamu aliyekuwa amekuwa kuhani mwenyewe, Yesu alikuwa “ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.”—Waebrania 5:10.

Zaidi ya hayo, Yesu hakuwa na wazao wowote wala waandamizi kwa ukuhani wake. Kwa njia hiyo pia, alikuwa bila nasaba. Atatekeleza utumishi wake wa kikuhani kwa umilele akiwa mfunzi mwenye kusaidia. Paulo alieleza juu ya utumishi huo wenye kuendelea, akisema hivi:

“Kwa kuwa [Yesu] akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.”—Waebrania 7:24, 25.

Kwa hiyo, kufikiria kwetu maneno ya Paulo kwenye Waebrania 7:3 kwapasa kuwe zaidi ya kutia ujuzi kichwani mwetu. Kwapaswa kuimarisha uthamini wetu kuelekea ule uandalizi wenye upendo ambao Yehova Mungu ametufanyia ili tupate msamaha wa dhambi kwa umilele na kuelekea njia ambayo amepanga ili tupokee msaada na mwongozo daima.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki