Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 10/15 kur. 3-4
  • Woga wa Wafu Umeenea

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Woga wa Wafu Umeenea
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Wazazi Wetu wa Kale Wako Wapi?
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
  • Roho Zisizoonekana—Je! Zinatusaidia? Au Zinatuumiza?
    Roho Zisizoonekana—Je! Zinatusaidia? au Zinatuumiza?
  • Je, Uhofu Wafu?
    Amkeni!—1996
  • Kuna Sababu ya Kuwaogopa Wafu?
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 10/15 kur. 3-4

Woga wa Wafu Umeenea

Jua lilikwisha tua. Unarudi nyumbani kwa kuchelewa kidogo kuliko vile ungalipenda. Unapofika karibu na makaburi ya huko, moyo wako waanza kudunda haraka zaidi. Ukimya wa giza wakufanya usikie hata kelele ndogo zaidi. Kwa ghafula wasikia kwa mbali sauti nyembamba yenye kushtusha. Waongeza mwendo—moyo wako waongeza mwendo wake na kudunda-dunda haraka pia—unapoelekea kupata ulinzi nyumbani.

UMEWAHI kuwa na hisia za woga ulipokuwa karibu na makaburi? Ikiwa ndivyo, waweza kuwa uliongozwa na mawazo ya kidini yaliyo ya kawaida ulimwenguni pote—kwamba roho za wafu zaweza kusaidia au kudhuru walio hai.

Desturi nyingi za ushirikina zimesitawi kama tokeo la imani kwamba wafu wahitaji msaada wa walio hai au kwamba waweza kudhuru walio hai ikiwa hawatatulizwa. Kwa mfano, katika nchi fulani za Amerika ya Latini, wengi wana desturi ya kujenga makao madogo yakiwa na msalaba mahali ambapo mtu amekufa kutokana na aksidenti. Watu huwasha mishumaa na kuweka maua mahali hapo kwa jitihada ya kuonyesha kupendezwa au kwa kusaidia nafsi au roho ya mtu aliyekufa. Katika visa vingine, ripoti kuhusu majibu ya “kimwujiza” ya sala zimeenea, hivi kwamba watu waanza kwenda mara kwa mara mahali pa animita, lile kao dogo la nafsi au roho ya mtu aliyekufa. Hapo wao hufanya mandas, au ahadi, kwamba ikiwa mtu aliyekufa atawasaidia kutimiza au kupokea kitu—pengine ponyo la miujiza—wataonyesha shukrani zao kwa njia ya pekee. Kwa upande mwingine, yaweza kuripotiwa ya kwamba nafsi ya mtu huonekana kwenye giza la usiku, zikiwatisha sana wale waliopo. Husemwa kwa kawaida kwamba nafsi hizo ni penando, zikiwaudhi wanaoishi kwa sababu ya matukio yaliyopita.

Katika nchi nyingi watu huweka jitihada nyingi kutuliza “roho” za wafu. Karamu kubwa-kubwa hufanywa, dhabihu hutolewa, maneno ya kutuliza husemwa—yote kwa jitihada za kuzuia malipizo ya kisasi kutoka kwa roho za watu waliokufa. Yafikiriwa kwamba kuridhisha roho za wafu, kutaleta thawabu na baraka nyingi kwa waliobaki.

“Wengi huamini kuwa hakuna tukio hutokea ‘peke yalo au kama kawaida,’” yasema ripoti moja kutoka Afrika. “Tukio lolote—liwe ugonjwa, msiba, kutozaa, matatizo ya kifedha, mvua nyingi kupita kiasi au jua kali mno, aksidenti za barabarani, mgawanyiko katika familia, kifo—hufikiriwa kuwa laletwa na roho zisizoonekana zilizo na uwezo uzidio wa kibinadamu.” Ripoti nyingine yasema: “Watu huamini kwamba roho za wazazi wao wa kale ziko sehemu fulani mbinguni na daima zinawaangalia watu wao walio hai duniani. Wazazi wa kale wanaaminiwa kuwa na nguvu zisizo za kawaida, zinazoweza kutumiwa kubariki na kulinda watu wao wa ukoo walioko duniani au kuwaadhibu, ikitegemea staha au kuachiliwa kwa mfu na mtu wa ukoo.”

Lakini je, hayo huambatana na Neno la Mungu? Maoni yako ni nini?

[Picha katika ukurasa wa 4]

“Animita” katika Chile

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki