Nyongeza ya Baraza Linaloongoza
KWA ajili ya kuongeza washiriki wa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova, kuanzia Julai 1, 1994, mshiriki mwingine mmoja ameongezwa kwa wale wazee 11 wanaotumika sasa. Mshiriki huyo mpya ni Gerrit Lösch.
Ndugu Lösch aliingia katika utumishi wa wakati wote katika Novemba 1, 1961, na kuhitimu katika darasa la 41 la Watchtower Bible School of Gilead. Alitumika katika kazi ya mzunguko na ya wilaya katika Austria kuanzia 1963 hadi 1976. Alioa katika 1967, naye pamoja na mkeye, Merete, baadaye walitumika kwa miaka 14 wakiwa washiriki wa familia ya Betheli ya Austria katika Vienna. Miaka minne iliyopita walihamishwa na kupelekwa katika makao makuu ya Sosaiti katika Brooklyn, New York, ambapo Ndugu Lösch ametumika katika Ofisi za Utekelezaji na akiwa msaidizi wa Halmashauri ya Utumishi. Akiwa na ujuzi mbalimbali katika eneo la Ulaya na kujua kwake Kijerumani, Kiingereza, Kirumania, na Kiitalia, atachangia sana kazi ya Baraza Linaloongoza.