Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 4/15 kur. 26-28
  • Mlima “Usongao”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mlima “Usongao”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mahali pa Kupilgrimu Palipoanzishwa Zamani
  • Sehemu za Pilgrimu
  • Kwa Nini Wanakwea?
  • Walisukumwa Kumthamini Muumba
  • Niliachwa na Wazazi Nikapendwa na Mungu
    Amkeni!—2001
  • Mimi Nilipanda Mlima Ulio Mzuri Kupita Yote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Wale Mapilgrimu na Kupigania Kwao Uhuru
    Amkeni!—1996
  • Ni Nani Atakayeiokoa Milima?
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 4/15 kur. 26-28

Mlima “Usongao”

ULE mlima wa kipekee uliochongoka mviringo wa Croagh Patrick magharibi mwa Ireland, ni mashuhuri kuliko milima inayouzunguka. Kila mwaka, Jumapili ya mwisho ya Julai, kilele cha mlima huonekana kama kinasonga wakati watu wengi karibu 30,000, wachanga na wazee vilevile, wakweapo hadi kwenye kilele (meta 765) kwa ajili ya kupilgrimu kila mwaka.

Siku hiyo, mapilgrimu hupanda na kushuka kwenye kijia chembamba, kibovu, na kwenye visehemu hatari. Kwa kweli, kuelekea kwenye kilele (karibu meta 300) kumeinuka zaidi na kuna miamba isiyo imara, hivyo ikifanya kupanda huko kuwe hatari na kwenye kuchosha sana.

Wengine hukwea bila viatu, na wachache hata watamalizia sehemu iliyobaki ya mkweo kwa magoti. Katika nyakati zilizopita, kupilgrimu kulianza usiku kukiwa na giza.

Kwa nini Croagh Patrick uwe wa maana jinsi hiyo kwa walio wengi?

Mahali pa Kupilgrimu Palipoanzishwa Zamani

Mapema katika karne ya tano W.K., Kanisa la Katoliki ya Kiroma lilimtuma Patrick Ireland akiwa askofu mishonari. Lengo lake lilikuwa kubadili Waireland wawe Wakristo, na wakati wa miaka yake ya kuhubiri na kufanya kazi miongoni mwa watu, Patrick anasemwa kuwa ndiye aliyeweka msingi wa Kanisa Katoliki huko.

Kazi yake ilimpeleka katika sehemu kadhaa kotekote nchi hiyo. Moja yayo ilikuwa magharibi mwa Ireland ambapo, kulingana na vyanzo fulani vya habari, alitumia siku 40 mchana na usiku juu ya mlima uliokuja kuitwa kwa jina lake—Croagh Patrick (maana yake “Kilima cha Patrick”). Huko alifunga na kuomba ili afanikiwe kwa kazi yake.

Kwa miaka mingi hekaya nyingi zimesemwa juu ya matendo yake ya ushujaa. Moja ya zijulikanazo sana ni kwamba akiwa juu ya mlima, Patrick alifukuza nyoka wote kutoka Ireland.

Mapokeo hudai kwamba alijenga kanisa dogo kwenye kilele. Ijapokuwa jengo hilo lilitoweka zamani, msingi wa kwanza bado upo, mahali hapo pamoja na mlima huo pamekuwa mahali pa kupilgrimu miaka yote.

Sehemu za Pilgrimu

Kwa mzee-mzee au kwa mtu asiyezoea kukwea milima, kumaliza kukwea kwa kilometa tano tu na kushuka salama ni utimizo mkubwa.

Kwenye visehemu vikuu kwenye kijia, watu wa kushughulikia mambo ya dharura husimama tayari kuhangaikia majeraha.

Kuna visehemu, au vituo vitatu njiani ambapo mapilgrimu hufanya maungamo. Hayo huandikwa waziwazi kwenye ubao wa matangazo penye mwanzo wa kupanda.—Ona sanduku.

Kwa Nini Wanakwea?

Kwa nini watu wengi hivyo hufanya upilgrimu huo hatari? Kwa nini wengine hufanya mambo kupita kiasi wakweapo?

Wengine huamini kwamba wakisali wakati wa kupilgrimu, dua zao za kibinafsi zaweza kusikilizwa. Wengine hufanya hivyo wakitafuta msamaha wa makosa fulani. Kwa wengine hii ni njia ya kushukuru. Bila shaka, wengi huenda kwa kusudi la sherehe. Mtu mmoja mwenye mamlaka alisema kwamba huo ‘ni wonyesho wa roho ya jumuiya na upendo wa kijamii.’ Pia alisema kwamba kukwea Croagh Patrick “kulikuwa njia yao ya kufuata nyayo za Mt[akatifu] Patrick na ya kutambua deni waliyomwia katika imani.” Aliendelea kusema kwamba jambo la maana zaidi, kukwea, ni “wonyesho wa toba kwa sababu uchovu wa mwili unaohusika ni tendo la toba kweli-kweli. Kukwea polepole kuelekea kilele ni tendo refu la toba.”

Mtu mmoja alisema kwa majivuno kwamba alikuwa amekwea mara 25! Alifanya hivyo, yeye akasema, “ili kufanya utubio mdogo!” Mtu mwingine alisema, “Bila maumivu, hakuna faida!”

Wengi hukwea mlima bila viatu, ingawa si lazima. Kwa nini? Kwanza, wanaona sehemu hiyo kuwa “takatifu” na hivyo wao hutoa viatu vyao. Pili, kwa kupatana na lengo lao la kuonyesha ‘utubio mdogo.’ Hili pia hueleza sababu inayofanya wengine kufanya matendo ya kuungama kwa magoti.

Walisukumwa Kumthamini Muumba

Lakini vipi ikiwa mtu fulani hakushiriki mambo ya kidini ya mapilgrimu waliokwea siku ya pekee? Mlima huo waweza kukwewa wakati wowote, hali ya hewa ikiwa nzuri na kuvalia viatu vizuri. Hatukukwea siku ambayo umati wa mapilgrimu walipokuwa wakikwea. Tulipotua kupumzika mara kwa mara, tuliweza kuwazia kukwea kwenyewe na matokeo ya kufanya hivyo kwa walio wengi. Tukiwazia maelfu ya mapilgrimu waliokuwa wakikwea kwa kutumia nguvu nyingi huku wakifanya vitubio kadha wa kadha, tulisukumwa kufikiri, ‘Je, hivyo ndivyo Mungu anavyotaka? Je, desturi ya ibada ya kukwea au ya kuzunguka majengo fulani huku sala zikirudiwa-rudiwa kweli humvuta mtu kwa Mungu?’ Vipi juu ya shauri la Yesu katika Mathayo 6:6, 7, juu ya sala za kurudia-rudia?

Kwa hakika, hatukukwea mlima huo kwa ajili ya mambo ya kidini. Na bado, tulihisi ukaribu zaidi kwa Muumba wetu kwa sababu tungeweza kuthamini uumbaji wake, milima iliyoko kokote ikiwa sehemu ya maajabu ya dunia. Kwenye kilele tuliweza kufurahia kuonekana wazi kwa uzuri wa nchi, hata kuona mahali ambapo nchi kavu imeungana na Bahari ya Atlantiki. Visiwa vidogo vyenye kung’aa katika ghuba iliyokuwa chini yetu katika upande mwingine vilitofautiana sana na sehemu ya milima-milima yenye mawe na iliyo tupu upande ule mwingine.

Tuliwazia juu ya vile vituo vitatu. Tukayakumbuka maneno ya Yesu, alipowaambia wafuasi wake wa kweli: “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke [“msiseme mambo yaleyale tena na tena,” NW], kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.”—Mathayo 6:7.

Tulitambua kwamba mlima huo ulikwisha kuwa sehemu ya mapokeo ambayo yamefunga maelfu ya watu katika desturi za ibada zenye kutumikisha. Tuliwazia jinsi hilo lilivyo tofauti na uhuru uliozungumzwa na mtume Yohana aliposema: “Tuzishike amri zake; [za Mungu] wala amri zake si nzito.”—1 Yohana 5:3.

Tulifurahia tafrija yetu, kutia ndani kukwea Croagh Patrick. Ilitusukuma kutazamia mbele wakati ambapo binadamu wote watawekwa huru kutokana na mapokeo yasiyo ya Kibiblia na kuweza kumwabudu Muumba wa dunia mwenye upendo “katika roho na kweli.”—Yohana 4:24.

[Sanduku katika ukurasa wa 27]

Sehemu Kubwa za Pilgrimu

Kila mpilgrimu akweaye mlima huo Siku ya Mtakatifu Patrick au katika siku ya nane, au wakati wowote wa miezi ya Juni, Julai, Agosti na Septemba, au katika juma hilo na KUSALI NDANI AU KARIBU NA KIKANISA HICHO kwa niaba ya makusudio ya Papa huenda atapata ondoleo la dhambi kwa msingi wa takwa la kwenda Kutubia Dhambi na Ushirika Mtakatifu kwenye Kilele au katika juma hilo.

VITUO VYA KIMAPOKEO

Kuna “vituo” vitatu (1) Kwenye mwanzo wa mlima au Leacht Benain, (2) Kwenye kilele, (3) Roilig Muire, mwendo fulani kuteremka chini upande wa Lecanvey [mji] wa mlima huo.

Kituo cha Kwanza - LEACHT BENAIN

Mpilgrimu huzunguka mviringo wa mawe mara saba akisema Baba Yetu mara 7, Maria Mtakatifu mara 7 na kurudia kanuni moja ya Imani

Kituo cha Pili - KILELE

(a) Mpilgrimu hupiga magoti na kusema Baba Yetu mara 7, Maria Mtakatifu mara 7 na kurudia kanuni moja ya Imani

(b) Mpilgrimu husali karibu na Kanisa kwa niaba ya makusudio ya Papa

(c) Mpilgrimu huzunguka Kanisa hilo mara 15 akisema Baba Yetu mara 15, Maria Mtakatifu 15 na kurudia kanuni moja ya Imani

(d) Mpilgrimu huzunguka Leaba Phadraig [Kitanda cha Patrick] mara 7 akisema Baba Yetu mara 7, Maria Mtakatifu 7 na kurudia kanuni moja ya Imani

Kituo cha Tatu - ROILIG MUIRE

Mpilgrimu huzunguka kila rundo la mawe mara 7 akisema Baba Yetu mara 7, Maria Mtakatifu 7 na kurudia kanuni moja ya Imani kwenye kila rundo la mawe [kuna marundo matatu ya mawe] na mwishowe huzunguka mahali pote pa Roilig Muire mara 7 akisali.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki