Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 3/15 uku. 7
  • Wategemezwa na Rafiki Yao Mkubwa Kupita Wote

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wategemezwa na Rafiki Yao Mkubwa Kupita Wote
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Divai, Mbao, na Utengenezaji wa Mapipa
    Amkeni!—2005
  • Nilikuwa Mwanasiasa Lakini Sasa Mimi Ni Mkristo
    Amkeni!—2002
  • Zaidi ya Miaka 40 Chini ya Marufuku ya Ukomunisti
    Amkeni!—1995
  • “Wana Nguvu Nyingi Ajabu za Kiadili”
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 3/15 uku. 7

Wategemezwa na Rafiki Yao Mkubwa Kupita Wote

KUNA urafiki mmoja ambao hasa huwategemeza Mashahidi wa Yehova. Ni uhusiano wao wenye thamani pamoja na Rafiki yao mkubwa kupita wote, Yehova Mungu. (Linganisha Yakobo 2:23.) Yeye huwategemeza wakati wa mitihani mikubwa ya imani.

Rekodi ya Mashahidi ya uaminifu-maadili chini ya utawala wa kimabavu imesifiwa na watazamaji wengi. Mmoja wao ni Jiří Krupička, daktari wa falsafa na sayansi za asili ambaye alihama kutoka Chekoslovakia katika 1968 baada ya kuwa katika kambi za mateso za Kikomunisti. Katika kitabu chake Renesance rozumu (Mvuvumko wa Welekevu), anatoa maelezo kuhusu mateseko na uimara wa Mashahidi waliofungwa gerezani kwa sababu ya kutokuwamo kwao.

Wakiwa chini ya serikali ya Kikomunisti, Mashahidi wengi walitiwa gerezani kwa sababu ya imani yao. Ijapokuwa walikuwa wamefungwa gerezani, walikataa kuchimba urani za kutumiwa vitani. (Isaya 2:4) Krupička afafanua jambo aliloona kwenye mojawapo machimbo hayo katika 1952. Aliona maumbo mawili yakisimama kama vinyago vilivyofunikwa na barafu katika halihewa ya kipupwe kikali. Mapipa ya chuma yalifunika vichwa vyao na sehemu za juu za miili yao.

Krupička aandika: “Walikuwa wamesimama hapo wakiwa wamevalia matambaa ya gereza tangu asubuhi mapema. Wangewezaje kusimama kwa muda mrefu hivyo miguu yao ikiwa imegandamana kwa barafu? Kwa nguvu za imani. Hayo mapipa yalikuwa ya zamani na yenye kutu. Mtu mkatili aliwapiga kwa nguvu vichwani na mabegani hivi kwamba ukingo wa pipa wenye vichonge ulikata koti hadi kwenye ngozi ya mmojawapo wanaume hao, na damu ilikuwa ikitiririka kupitia mkono wa vazi lake.

“Mlinzi alisimamisha safu yetu mbele yao, naye kamanda akatutolea hotuba fupi. Yeye alisema, kukataa kufanya kazi ni uasi na adhabu hutolewa vilivyo. Hakuna mateto ya upuzi dhidi ya vita na uuaji yatakayosaidia hawa wapinzani, hawa adui wa Usoshalisti.”

Kamanda huyo akachukua chuma na kupiga mojawapo yale mapipa. Mwanamume aliyekuwa ndani yalo alizirai, pipa likiwa lingali linamfunika kichwani. Lililofuata kutukia linabaki sana katika kumbukumbu la Krupička.

Yeye asema: “Kuimba kulisikika kukitoka ndani ya hayo mapipa. Sauti nyororo, sala ya kunong’oneza kwa Mungu, awezaye kusikia kitu chochote kutoka mahali popote—hata kuimbwa kulikojaribiwa kutoka ndani ya mapipa ya zamani ya urani, yaliyo na kutu. Yeye husikia zaidi ya uimbaji uimbwao kwa sauti ya juu katika kanisa kuu.”

Mnamo Septemba 1, 1993, kazi ya Mashahidi wa Yehova katika Jamhuri ya Cheki ilitambuliwa kisheria. Mashahidi wa Cheki sasa huonea shangwe kuendeleza kazi yao ya Kikristo ya uelimishaji wakiwa huru. Naam, wao hufurahia kuambia wengine kuhusu Yehova, Rafiki yao mkubwa kupita wote.

[Picha katika ukurasa wa 7]

Wahudhuriaji wa mkusanyiko katika Jamhuri ya Cheki

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki