Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 3/1 kur. 30-31
  • Yesu Anakaribishwa Akiwa Mesiya na Mfalme!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Anakaribishwa Akiwa Mesiya na Mfalme!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Unabii wa Kale Watimizwa
  • Ujumbe Kuhusu Umaliki
  • Somo Kwetu Sisi
  • Kuingia kwa Kristo Katika Yerusalemu kwa Shangwe ya Ushindi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kristo Aingia Katika Yerusalemu kwa Shangwe ya Ushindi
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mfalme Aingia Yerusalemu Akiwa Juu ya Mwanapunda
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yerusalemu wa Kidunia Watofautiana na Yerusalemu wa Mbinguni
    Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 3/1 kur. 30-31

Walifanya Mapenzi ya Yehova

Yesu Anakaribishwa Akiwa Mesiya na Mfalme!

ULE umati wenye makelele uliokuwa ukiingia Yerusalemu Nisani 9, 33 W.K., uliwashangaza Wayudea wengi. Ingawa lilikuwa jambo la kawaida kuona watu wakimiminikia hilo jiji kabla ya Sikukuu ya Kupitwa, watu hao wenye kuzuru walikuwa tofauti. Mtu maarufu miongoni mwao alikuwa mwanamume aliyekuwa amepanda mwana-punda. Huyo mwanamume alikuwa Yesu Kristo, na watu walikuwa wakitandaza mavazi na matawi ya mitende mbele yake huku wakipaaza sauti: “Okoa Mwana wa Daudi, twasihi! Mbarikiwa ni yeye ajaye katika jina la Yehova! Mwokoe, twasihi, katika mahali palipo juu!” Walipouona huo umati, wengi waliokuwamo Yerusalemu tayari walisukumwa kujiunga na huo mwandamano.—Mathayo 21:7-9; Yohana 12:12, 13.

Hata ingawa sasa alikuwa akikaribishwa, Yesu alijua kwamba majaribu yalimngoja. Kwani, katika siku tano tu, yeye angeuawa katika jiji hilohilo! Ndiyo, Yesu alijua kwamba Yerusalemu lilikuwa eneo lenye uhasama, na akiwa na wazo hilo akilini alipangia uingiaji wake wa kutazamisha katika hilo jiji.

Unabii wa Kale Watimizwa

Mwaka wa 518 K.W.K., Zekaria alitabiri uingiaji wa shangwe ya ushindi wa Yesu katika Yerusalemu. Aliandika hivi: “Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; tazama, mfalme wako anakuja kwako; ni mwenye haki, naye ana wokovu; ni mnyenyekevu, amepanda punda, naam, mwana-punda, mtoto wa punda. . . . Naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.”—Zekaria 9:9, 10.

Kwa hiyo uingiaji wa Yesu katika Yerusalemu Nisani 9 ulitimiza unabii wa Biblia. Halikuwa tukio la kivivi hivi tu bali lilipangwa kwa uangalifu. Mapema, akiwa nje tu ya Yerusalemu, Yesu alikuwa amewaagiza wawili wa wanafunzi wake hivi: “Shikeni njia mwende mwingie katika kijiji kilicho karibu yenu, nanyi mara moja mtakuta punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni na kuwaleta kwangu. Na ikiwa mtu fulani awaambia jambo lolote, lazima mseme, ‘Bwana awahitaji.’ Ndipo atawatuma mara.” (Mathayo 21:1-3) Lakini mbona Yesu alitaka kuingia Yerusalemu akiwa amepanda punda, na itikio la ule umati lilikuwa na umaana gani?

Ujumbe Kuhusu Umaliki

Mara nyingi mfano wa kuonekana ni wenye nguvu kuliko neno lisemwalo. Hivyo, nyakati nyingine Yehova aliwaagiza manabii wake waigize ujumbe wao ili kutia nguvu ujumbe wao wa kiunabii. (1 Wafalme 11:29-32; Yeremia 27:1-6; Ezekieli 4:1-17) Njia hiyo bora sana ya uwasiliano ya kutumia mifano ya kuonwa iliacha alama isiyofutika akilini mwa hata mtazamaji mwenye moyo mgumu kupita yote. Kwa njia hiyohiyo, Yesu aliigiza ujumbe wenye nguvu kwa kuingia jiji la Yerusalemu akiwa amepanda punda. Jinsi gani?

Katika nyakati za Biblia punda alitumiwa kwa makusudi ya kikabaila. Kwa kielelezo, Solomoni alikwenda kutiwa mafuta awe mfalme akiwa amepanda “nyumbu” wa babaye, mzao mvyauso wa punda-dume. (1 Wafalme 1:33-40) Kwa hiyo kuingia kwa Yesu Yerusalemu akiwa amepanda punda kulimaanisha kwamba alikuwa akijitoa kuwa mfalme.a Matendo ya ule umati yalitia nguvu ujumbe huo. Kile kikundi ambacho, bila shaka, kilitia ndani Wagalilaya hasa, walitandaza mavazi yao mbele ya Yesu—tendo lililokumbusha juu ya lile tangazo la hadharani la umaliki wa Yehu. (2 Wafalme 9:13) Kurejezea kwao Yesu kuwa “Mwana wa Daudi” kulikazia haki yake halali ya utawala. (Luka 1:31-33) Na kutumia kwao matawi ya mitende kulionyesha kwa wazi unyenyekeo wao kwa mamlaka yake ya kifalme.—Linganisha Ufunuo 7:9, 10.

Kwa hiyo huo mwandamano ulioingia Yerusalemu Nisani 9 ulionyesha kwa wazi kwamba Yesu alikuwa Mesiya na Mfalme aliyewekwa rasmi na Mungu. Bila shaka, si wote waliofurahi kumwona Yesu akiwa ametokezwa kwa njia hiyo. Mafarisayo hasa waliona kule kuonyeshwa kwa Yesu heshima nyingi hivyo ya kifalme kuwa jambo lisilofaa kabisa. Bila shaka wakiwa na hasira katika sauti zao, walidai hivi: “Mwalimu, kemea wanafunzi wako.” Yesu akajibu hivi: “Mimi nawaambia nyinyi, Kama hawa wangekaa kimya, mawe yangepaaza kilio.” (Luka 19:39, 40) Ndiyo, Ufalme wa Mungu ulikuwa ndio kichwa cha kuhubiri kwa Yesu. Angeupiga mbiu ujumbe huo kwa ujasiri iwe watu waukubali au la.

Somo Kwetu Sisi

Yesu alihitaji moyo mkuu sana ili kuingia Yerusalemu kwa njia iliyotabiriwa na nabii Zekaria. Alijua kwamba kwa kufanya hivyo alikuwa akichochea ghadhabu ya maadui wake. Kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, Yesu aliwapa wafuasi wake utume wa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na ‘kufanya wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote.’ (Mathayo 24:14; 28:19, 20) Moyo mkuu wahitajiwa pia ili kutimiza jambo hilo. Si wote wanaofurahi kuusikia huo ujumbe. Watu fulani ni wenye ubaridi kuuelekea, ilhali wengine huupinga. Serikali fulani zimewekea kazi ya kuhubiri vizuizi au zimeipiga marufuku kabisa.

Bado, Mashahidi wa Yehova wanang’amua kwamba habari njema ya Ufalme wa Mungu uliosimamishwa lazima ihubiriwe, iwe watu wasikiliza au wakataa kusikiliza. (Ezekieli 2:7) Waendeleapo kufanya kazi hiyo ya kuokoa uhai, wanatiwa moyo na ahadi hii ya Yesu: “Tazameni! mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi umalizio wa mfumo wa mambo.”—Mathayo 28:20.

[Maelezo ya Chini]

a Simulizi la Marko laongeza kwamba huyo mwana-punda alikuwa mmoja “ambaye hakuna yeyote wa wanadamu ameketi juu yake.” (Marko 11:2) Kwa wazi, mnyama ambaye hakuwa ametumiwa bado alifaa hasa kwa makusudi matakatifu.—Linganisha Hesabu 19:2; Kumbukumbu la Torati 21:3; 1 Samweli 6:7.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki