Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 9/15 kur. 8-9
  • Mtawala Mwenye Kiburi Apoteza Milki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtawala Mwenye Kiburi Apoteza Milki
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mtawala-Mwenzi au Mfalme?
  • Mtawala Mwenye Kujitumaini Mno na Mwenye Kiburi
  • Maneno Manne Yaliyoubadili Ulimwengu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2020
  • Biblia Inasema Nini Kumhusu Danieli?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 9/15 kur. 8-9

Mtawala Mwenye Kiburi Apoteza Milki

“BELSHAZA, mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao,” akaandika nabii Danieli. Hata hivyo karamu hiyo ilipokuwa ikiendelea, “uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.” Kabla ya usiku huo kwisha, “Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme.”—Danieli 5:1, 6, 30, 31.

Belshaza alikuwa nani? Alipataje kuitwa “mfalme wa Wakaldayo”? Alikuwa na wadhifa gani hasa katika Milki Mpya ya Babiloni? Alipotezaje milki hiyo?

Mtawala-Mwenzi au Mfalme?

Danieli humrejezea Nebukadneza kuwa baba ya Belshaza. (Danieli 5:2, 11, 18, 22) Hata hivyo, uhusiano huo si halisi. Kitabu Nabonidus and Belshazzar, cha Raymond P. Dougherty, chadokeza kwamba labda Nebukadneza alikuwa babu ya Belshaza kupitia Nitocris mama yake. Huenda pia ikawa kwamba Nebukadneza, akiwa mfalme aliyemtangulia, alikuwa tu “baba” ya Belshaza kuhusiana na ufalme. (Linganisha Mwanzo 28:10, 13.) Kwa vyovyote, miandiko ya kikabari kwenye silinda kadhaa za udongo ambazo ziligunduliwa katika karne ya 19 kusini mwa Iraki, zamtambulisha Belshaza kuwa mwana wa kwanza wa Nabonido, mfalme wa Babiloni.

Kwa kuwa simulizi la Danieli sura ya 5 lakazia matukio ya usiku wa kuanguka kwa Babiloni mwaka wa 539 K.W.K., halisimulii jinsi ambavyo Belshaza alikuja kupata mamlaka ya kifalme. Lakini vyanzo vya kiakiolojia vyatoa dhana fulani juu ya uhusiano kati ya Nabonido na Belshaza. “Maandishi ya Babiloni yafunua kwamba Nabonido alitawala akiwa mbali,” asema Alan Millard, mwakiolojia na stadi wa lugha za kale za Kisemiti. Millard aendelea kusema: “Ingawa hakupuuza miungu ya Babiloni, yeye . . . alitoa uangalifu mkubwa kwa mungu-mwezi wa majiji mengine mawili, Uru na Harani. Kwa miaka kadhaa ya utawala wake, Nabonido hata hakuishi Babiloni; badala yake aliishi mbali mahali penye oasisi (chemchemi katika jangwa) huko Teima [au, Tema], kaskazini mwa Arabia.” Ni wazi kwamba, kwa miaka mingi ya utawala wake, Nabonido alikuwa mbali na jiji kuu Babiloni. Wakati ambapo hakuwepo, Belshaza alipewa mamlaka ya utawala.

Ikifafanua zaidi juu ya cheo halisi cha Belshaza, hati ya kikabari ifafanuliwayo kuwa “Simulizi la Aya ya Nabonido” yasema: “Yeye [Nabonido] aliyakabidhi ‘Majeshi’ kwa (mwana) wake mkubwa, mzaliwa wa kwanza na kuviamuru vikosi kotekote katika nchi viwe chini ya (amri) yake. Yeye alimkabidhi (kila kitu), yeye akamkabidhi ufalme.” Hivyo, Belshaza alikuwa mtawala-mwenzi.

Ingawa hivyo, je, mtawala-mwenzi anaweza kuonwa kuwa mfalme? Sanamu moja ya mtawala fulani wa kale iliyopatikana huko kaskazini mwa Siria miaka ya 1970 yaonyesha kwamba, ilikuwa kawaida kwa mtawala kuitwa mfalme wakati ambapo, kihalisi, alikuwa na cheo cha chini kidogo. Sanamu hiyo ilikuwa ya mtawala wa Gozani na iliandikwa kwa Kiashuri na Kiaramu. Mwandiko wa Kiashuri ulimwita mwanamume huyo gavana wa Gozani, bali mwandiko wa Kiaramu unaolingana na huo ulimwita mfalme. Kwa hiyo, haingekuwa mara ya kwanza kwa Belshaza kuitwa mwana-mfalme mteule katika miandiko rasmi ya Babiloni na wakati uleule kuitwa mfalme katika maandishi ya Kiaramu ya Danieli.

Mpango wa kutawala kwa pamoja kati ya Nabonido na Belshaza uliendelea hadi siku za mwisho za Milki Mpya ya Babiloni. Kwa hiyo, usiku uleule Babiloni ilianguka, Belshaza alijitolea kumfanya Danieli mtawala wa tatu wa ufalme huo, wala si wa pili.—Danieli 5:16.

Mtawala Mwenye Kujitumaini Mno na Mwenye Kiburi

Matukio ya mwisho ya utawala wa Belshaza yaonyesha kwamba huyo mwana-mfalme mteule alikuwa mwenye kujitumaini mno na mwenye kiburi. Mwisho wa utawala wake ulipofika katika Oktoba 5, 539 K.W.K., Nabonido alikuwa amejificha huko Borsippa, akiwa ameshindwa na majeshi ya Umedi na Uajemi. Babiloni yenyewe ilikuwa imezingirwa. Lakini Belshaza alijihisi akiwa salama sana katika jiji hilo hivi kwamba, usiku huohuo aliwafanyia “wakuu wake elfu karamu kubwa.” Herodotus, mwanahistoria Mgiriki wa karne ya tano K.W.K., asema kwamba “wakati huo [watu] walikuwa wakicheza dansi na kujifurahisha” ndani ya jiji.

Ingawa hivyo, nje ya kuta za Babiloni, jeshi la Umedi na Uajemi lilikuwa chonjo. Chini ya mwelekezo wa Koreshi, walikuwa wameyaelekeza maji ya Mto Eufrati kwingineko, ambao ulipita katikati ya jiji hilo. Askari wake walikuwa tayari kuvuka bonde la mto huo mara tu kiwango cha maji kiliposhuka chini vya kutosha. Wangepanda ukingo ulioinama wa mto huo na kuingia jijini kupitia malango ya shaba yaliyokuwa wazi, ambayo yalikuwa kwenye ukuta kandokando ya mto.

Kama Belshaza angalijua yaliyokuwa yakitendeka nje ya jiji, angaliweza kufunga malango ya shaba, akawapandisha wanaume wake wenye nguvu kwenye kuta kandokando ya kingo za mto, na kunasa adui. Badala yake, akiwa amelewa divai, Belshaza mwenye kujigamba aliagiza vyombo kutoka katika hekalu la Yehova viletwe. Kisha yeye, wageni wake, wake zake, na masuria wake wakavinywea kwa ukaidi, huku wakiisifu miungu ya Babiloni. Kwa ghafula, mkono ukatokea kimuujiza, ukaanza kuandika kwenye ukuta wa jumba la mfalme. Akiwa ametiwa hofu, Belshaza aliwataka wanaume wake wenye hekima waeleze maana ya ujumbe huo. Lakini “hawakuweza kuyasoma maandishi hayo wala kumjulisha mfalme maana yake.” Hatimaye, Danieli “akaletwa mbele ya mfalme.” Chini ya upulizio wa Mungu, nabii wa Yehova mwenye ujasiri alifunua maana ya ujumbe huo wa kimuujiza, akitabiri anguko la Babiloni kwa Waamedi na Waajemi.—Danieli 5:2-28, Biblia Habari Njema.

Waamedi na Waajemi walitwaa jiji hilo kwa urahisi, naye Belshaza akafa usiku huo. Kwa kifo chake, na kule kuonekanao kuwa kujisalimisha kwa Nabonido kwa Koreshi, Milki Mpya ya Babiloni ilifikia kikomo.

[Picha katika ukurasa wa 8]

Danieli aeleza maana ya ujumbe wa kuangamizwa kwa Milki ya Babiloni

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki