Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 9/1 uku. 24
  • ‘Wao Husema Juu ya Wema na Upendo’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Wao Husema Juu ya Wema na Upendo’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Habari Zinazolingana
  • Mashahidi Wafikia Watu Wote Ufaransa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • “Wema Wake, Jinsi Ulivyo Mwingi!”
    Mkaribie Yehova
  • Mweneo Mkubwa Ajabu wa Wema wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Wema Mwingi wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 9/1 uku. 24

‘Wao Husema Juu ya Wema na Upendo’

KATIKA miaka ya hivi karibuni, Mashahidi wa Yehova nchini Ufaransa wamekuwa shabaha ya kampeni kali ya kuwaharibia jina. Kweli zilizopotoshwa na udanganyifu umetumiwa na wapinzani wao kuwasema vibaya mbele za umma. Mwanzoni mwa mwaka wa 1999, Mashahidi wa Yehova kotekote Ufaransa waligawanya trakti milioni 12 yenye kichwa People of France, You Are Being Deceived! Katika trakti hiyo, walishutumu taarifa zinazotolewa ambazo zinawaharibia jina.

Siku chache baada ya kampeni hiyo, Bw. Jean Bonhomme, daktari aliyewahi kuwa mbunge, alituma barua kwa gazeti moja la huko. Aliandika hivi: “Mara kwa mara Mashahidi wa Yehova huja nyumbani kwangu. Wao huja kusema nami juu ya wema na upendo wa ulimwenguni kote. . . . Hawanilazimishi kuwasikiliza. Wao husema kwa upole na kusikiliza kwa fadhili shaka zangu.”

Akizungumzia maoni ya kiroho ya Mashahidi wa Yehova, Bw. Bonhomme alisema hivi: “Kutojua kwao mambo ya kilimwengu hakuwezi kamwe kudhuru yeyote. Kwa upande mwingine, wanasiasa wasiojua mambo ya ulimwengu wanaweza kuwa tisho zaidi kwa amani ya raia na utangamano wa jamii.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki