Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w01 5/1 uku. 19
  • Jina la Mungu Laondolewa Lawama

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jina la Mungu Laondolewa Lawama
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Ninawezaje Kuwa na Uhusiano Mzuri na Mwalimu Wangu?
    Vijana Huuliza
  • Ninaweza Kufanya Nini ili Nielewane na Mwalimu Wangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Alifanikiwa Kuliko Alivyotarajia
    Amkeni!—2003
  • Watoto wa Shule wa Naijeria Wabarikiwa kwa Ajili ya Uaminifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
w01 5/1 uku. 19

Ripoti ya Watangazaji wa Ufalme

Jina la Mungu Laondolewa Lawama

NENO la Mungu Biblia lasema: “Dumisheni mwenendo wenu ukiwa bora miongoni mwa mataifa, ili, katika jambo ambalo katika hilo wao wanasema dhidi yenu kuwa watenda-maovu, likiwa tokeo la kazi zenu bora ambazo wamekuwa mashahidi wa kujionea wapate kumtukuza Mungu katika siku ya ukaguzi wake.” (1 Petro 2:12) Kwa hiyo Wakristo wa kweli hujitahidi kudumisha mwenendo bora ili kuepuka kulitia jina la Yehova lawama.

Katika eneo la mashambani la Zambia liitwalo Senanga, redio ya mwalimu mmoja iliibwa kutoka nyumbani mwake. Kwa kuwa Mashahidi wa Yehova walikuwa wakihubiri katika eneo hilo, mwalimu huyo alisema kwamba wao ndio walioiba redio hiyo. Aliripoti jambo hilo kwa polisi, akadai kwamba Mashahidi waliiba redio yake. Ili kuthibitisha kwamba Mashahidi walikuwa wameingia nyumbani mwake, alionyesha trakti ambayo aliipata kwenye sakafu. Hata hivyo, polisi hao hawakumwamini. Walimshauri aende akafanye uchunguzi kwa makini zaidi.

Mashahidi waliokuwa wamehubiri eneo hilo siku hiyo walitiwa moyo na baraza la wazee wa kutaniko waende wakazungumze na mwalimu huyo kuhusu jambo hilo. Baadhi ya ndugu hao walienda na kuzungumza naye, wakamweleza kwamba walitaka kuliondolea jina la Yehova lawama. Wakati wa mazungumzo hayo, ndugu hao walimwambia kwamba walikuwa wamekuta mwanamume kijana nyumbani mwake na kumpa trakti. Mwalimu alimtambua mwanamume huyo walipomweleza sura yake. Hata walikuwa washiriki wa kanisa lilelile. Mwalimu huyo aliongea na mwanamume huyo kijana, lakini akakana mashtaka hayo. Ndipo mwalimu huyo akazungumzia jambo hilo na wazazi wa mwanamume huyo kisha akarudi nyumbani. Baada ya muda wa saa moja, mama ya mwanamume huyo akarudisha redio iliyokuwa imeibwa.

Mwalimu huyo alienda kwa baraza la wazee wa kutaniko akiwa amesikitika na kuomba msamaha kwa mashtaka yasiyo ya kweli aliyotoa. Wazee walikubali ombi lake la kutaka msamaha lakini wakaomba kwamba matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili kila mtu ajue kwamba Mashahidi hawakuwa na hatia. Tangazo lilifanywa kwenye shule, hivyo jina la Yehova likaondolewa lawama. Mashahidi wa Yehova wanaweza kuendelea kuhubiri katika eneo hilo bila vizuizi.

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 19]

AFRIKA

Zambia

[Hisani]

Mountain High Maps® Copyright © 1997 Digital Wisdom, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki