Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w02 9/15 uku. 3
  • Kwa Nini Watu Hupenda “Watakatifu” Siku Hizi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Watu Hupenda “Watakatifu” Siku Hizi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Habari Zinazolingana
  • Watakatifu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Watakatifu wa Kweli Wanaweza Kukusaidiaje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Je! Uchaji kwa Visalio vya Waonwao Kuwa Watakatifu Humpendeza Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Je, Tunapaswa Kusali kwa Watakatifu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
w02 9/15 uku. 3

Kwa Nini Watu Hupenda “Watakatifu” Siku Hizi?

“Wakumbuka wakati tulipokuwa tunachoka kusikia juu ya mashujaa? Waamerika milioni 4.2 hawakuchoka kusikia habari hizo walipokuwa wakitazama mazishi ya Mama Teresa hapo Septemba 13. Tangu alipokufa Septemba 5, watu wamekuwa wakisihi Vatikani wakitaka afanywe kuwa mtakatifu. Watu wengi wanaamini itakuwa hivyo.”—SUN-SENTINEL, MAREKANI, OKTOBA 3, 1997.

KAZI ya fadhila na ya hisani ambayo mishonari Mkatoliki Mama Teresa alifanya inaonwa na wengi kuwa sababu ya kumfanya awe mtakatifu wa kweli. Kuna watu mashujaa katika dini nyingine. Hata hivyo, labda hawatambuliwi rasmi kama wale wanaotangazwa kuwa watakatifu na Kanisa Katoliki la Roma.

Papa John Paul wa Pili amewatakasa karibu watu 300 wakati wa utawala wake wa kipapa, zaidi ya idadi ya wale waliotangazwa kuwa watakatifu na mapapa wengine wote wa karne ya 20 wakijumlishwa.a Kwa nini watu huwapenda sana “watakatifu,” ambao wengi wao hawajulikani miongoni mwa Wakatoliki kwa ujumla?

Mwanatheolojia wa Chuo Kikuu cha Notre Dame, Lawrence Cunningham aeleza hivi: “Wazo la kwamba kwaweza kuwa na utakatifu ulimwenguni lavutia watu. Kutambua kwamba kuna watakatifu kwaonyesha kwamba watu wanaweza kuwa mashujaa hata leo.” Kwa kuongezea, inadaiwa kwamba “watakatifu” wana njia ya pekee ya kumfikia Mungu, ikiwafanya wawe waombezi kwa niaba ya walio hai. Vitu fulani au masalio ya “watakatifu” huabudiwa yanapopatikana kwa sababu inaaminiwa kwamba yana nguvu fulani.

Baraza la Trent, lililofanywa mnamo karne ya 16 ili kuimarisha imani ya Kanisa Katoliki, liliamuru hivi: “Tuna haki ya kukata kauli kwamba kuwaheshimu watakatifu ‘ambao wamelala katika Bwana,’ kuwaomba watuombee, na kuheshimu sana vitu au masalio ya miili yao, huelekea kuuzidisha utukufu wa Mungu badala ya kuupunguza. Jambo hili ni kweli hivi kwamba tumaini la Mkristo linafanywa kuwa hai na kuimarishwa, na Mkristo anatiwa moyo kuiga sifa za watakatifu.” (The Catechism of the Council of Trent, 1905) Kwa kweli Wakristo wa kweli wanataka kuishi maisha yaliyo safi kiadili, kusali kwa Mungu kwa njia inayofaa, na kupokea msaada wa Mungu. (Yakobo 4:7, 8) Kwa hiyo, kulingana na Neno la Mungu, ni nani walio watakatifu wa kweli? Nao wanafanya kazi gani?

[Maelezo ya Chini]

a Mkatoliki aliyekufa ambaye ametangazwa rasmi kuwa mtakatifu anastahili kupewa heshima na Wakatoliki wengine wote.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki