Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 5/1 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Mvulana Mwenye Kupagawa na Shetani Aponywa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Mvulana Mwenye Kupagawa na Roho Mwovu Aponywa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 5/1 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Mkristo akisikia sauti fulani zisizoeleweka chanzo chake, je, hiyo inamaanisha kwamba anashambuliwa na roho waovu?

La. Ingawa imesemekana kwamba roho waovu hujidhihirisha kwa njia hiyo, watu wengi wanaosikia sauti, au kupatwa na hali fulani zenye kusumbua ambazo hazieleweki, wamegundua kwamba wana tatizo la kiafya baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Hata katika karne ya kwanza, yaonekana watu walitambua kwamba wakati mwingine hali kama hiyo ilisababishwa na roho waovu au magonjwa. Kwenye Mathayo 17:14-18, tunasoma kuhusu mvulana mmoja aliyeponywa na Yesu. Ingawa mvulana huyo alikuwa na dalili za kifafa, ugonjwa wake ulisababishwa na roho mwovu. Hata hivyo, pindi fulani kabla ya hapo, baadhi ya wagonjwa walioletwa kwa Yesu ili awaponye walikuwa “wenye kupagawa na roho waovu na wenye kifafa.” (Mathayo 4:24) Yaonekana ilijulikana kwamba watu fulani waliokuwa na kifafa hawakuwa wamepagawa na roho waovu. Walikuwa na matatizo ya kiafya tu.

Inasemekana kwamba watu fulani wanaougua schizophrenia (ugonjwa wa kuchanganyikiwa akili), ambao unaweza kutibiwa, husikia sauti au huonyesha dalili nyingine ambazo huenda hazieleweki.a Huenda magonjwa mengine ya kawaida yakafanya mtu achanganyikiwe akili na kufanya wengine wafikiri kimakosa kwamba yanasababishwa na roho waovu. Kwa hiyo, ingawa mtu anayesema kwamba anasikia sauti au anayepatwa na hali fulani zenye kusumbua ambazo hazieleweki huenda akafikiri kwamba anashambuliwa na roho waovu, anapaswa kutiwa moyo afikirie kufanyiwa uchunguzi ili kuona kama tatizo lake ni la kiafya au la.

[Maelezo ya Chini]

a Ona makala “Taking the Mystery out of Mental Illness,” katika gazeti la Kiingereza la Amkeni! la Septemba 8, 1986, linaloandamana na la Mnara wa Mlinzi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki