Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w09 9/1 uku. 24
  • Muujiza Siku ya Pentekoste!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muujiza Siku ya Pentekoste!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Habari Zinazolingana
  • Uharibifu wa Sodoma na Gomora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Anawaponya Watu Kimuujiza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Awashangaza Wasikilizaji Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Petro Amkana Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
w09 9/1 uku. 24

Kwa Ajili ya Vijana Wetu

Muujiza Siku ya Pentekoste!

Maagizo: Fanya zoezi hili katika mazingira matulivu. Unaposoma maandiko, jiwazie ukiwa katika matukio yanayozungumziwa. Wazia kikao. Sikia sauti. Hisi kama wahusika wakuu wanavyohisi. Wazia kwamba masimulizi haya ni halisi kabisa!

CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA MATENDO 2:1-21, 38-41.

Ni nini kinachokuja akilini unaposoma simulizi kuhusu ule “upepo wenye nguvu unaovuma” na zile “ndimi kama za moto”?

․․․․․

Unafikiri watu walisema nini waliposhangaa kuwasikia wanafunzi wakizungumza katika lugha za kigeni?

․․․․․

Unawazia nyuso za watu wenye shaka wanaozungumziwa kwenye mstari wa 13 zinaonyesha nini?

․․․․․

CHIMBA ZAIDI.

Pentekoste ilikuwa sherehe ya aina gani, na huenda hilo lilifanya umati uliokusanyika Yerusalemu uwe katika hali gani? (Kumbukumbu la Torati 16:10-12)

․․․․․

Petro aliwaonyesha wasikilizaji wake heshima jinsi gani alipokuwa akiongea nao, na alizungumza kuhusu jambo gani lililowapendeza wote? (Matendo 2:29)

․․․․․

Ujasiri alioonyesha Petro ulitofautiana jinsi gani na yale aliyotenda akiwa kwenye ua wa kuhani mkuu? (Mathayo 26:69-75)

․․․․․

TUMIA MAMBO ULIYOJIFUNZA. ANDIKA MAMBO ULIYOJIFUNZA KUHUSU . . .

Uhitaji wa kutafuta mambo yanayowapendeza wasikilizaji wetu na kuzungumza kwa heshima tunapowaambia kuhusu imani yetu inayotegemezwa na Biblia.

․․․․․

Unaweza kuwa Shahidi wa Yehova mwenye ujasiri hata ingawa sasa una haya au woga.

․․․․․

NI MAMBO GANI KATIKA SIMULIZI HILI AMBAYO YAMEKUGUSA MOYO SANA, NA KWA NINI?

․․․․․

Ukitaka kufanya utafiti zaidi, ona gazeti Mnara wa Mlinzi la Septemba 15, 1996 (15/9/1996), ukurasa wa 8-9.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki