Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w10 9/1 kur. 30-31
  • Mungu Hana Ubaguzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mungu Hana Ubaguzi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Uharibifu wa Sodoma na Gomora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Anawaponya Watu Kimuujiza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Awashangaza Wasikilizaji Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Ashinda Vishawishi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
w10 9/1 kur. 30-31

Kwa Ajili ya Vijana

Mungu Hana Ubaguzi

Maagizo: Fanya zoezi hili katika mazingira matulivu. Unaposoma maandiko, jiwazie ukiwa katika matukio yanayozungumziwa. Wazia kikao. Sikia sauti. Hisi kama wahusika wanavyohisi. Wazia kwamba masimulizi haya ni halisi kabisa.

Wahusika wakuu: Kornelio, Petro

Kwa ufupi: Petro anaiga sifa ya Mungu ya kutokuwa na ubaguzi kwa kumhubiria Kornelio ambaye si Myahudi.

1 CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA MATENDO 10:1-35, 44-48.

Wazia na ueleze jinsi Kornelio anavyoonekana.

․․․․․

Unafikiri Kornelio alihisi jinsi gani alipozungumza na malaika, kama mstari wa 3 hadi 6 unavyotaja?

․․․․․

Unafikiri Kornelio na watumishi wake walizungumzia nini kama inavyodokezwa katika mstari wa 7 na wa 8?

․․․․․

2 CHIMBA ZAIDI.

Kwa nini mfano ambao Petro alionyeshwa katika mstari wa 10 hadi 16 ulikuwa na matokeo? (Dokezo: Fikiria malezi ya Petro akiwa Myahudi, kama mstari wa 14 unavyodokeza.) _______

․․․․․

Unatambua sifa gani ya Kornelio katika mstari wa 25? Kwa nini si jambo la kawaida kwa mtu mwenye cheo kama chake kuwa na sifa hiyo? (Dokezo: Ona mstari wa 1.)

․․․․․

Kwa kutumia vifaa vya utafiti unavyoweza kupata, chunguza hesabu ya wanajeshi katika kikosi cha Italia ambacho Kornelio alisimamia.

․․․․․

Kwa nini kugeuzwa imani kwa Kornelio ni jambo la maana sana?

․․․․․

3 TUMIA MAMBO ULIYOJIFUNZA. ANDIKA MAMBO ULIYOJIFUNZA KUHUSU . . .

Kutumia mifano kwa njia yenye matokeo.

․․․․․

Sifa ya Mungu ya kutokuwa na ubaguzi.

․․․․․

Jinsi unavyoweza kuonyesha sifa hiyo ya kutokuwa na ubaguzi.

․․․․․

4 NI JAMBO GANI KATIKA SIMULIZI HILI AMBALO LIMEKUGUSA MOYO SANA, NA KWA NINI?

․․․․․

IKIWA HUNA BIBLIA, WAOMBE MASHAHIDI WA YEHOVA WAKUPE MOJA, AU SOMA HABARI ZAIDI KATIKA INTANETI www.watchtower.org

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki