Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w10 11/1 uku. 3
  • Je, Inawezekana Kuwa na Uradhi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Inawezekana Kuwa na Uradhi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Je, ‘Umejifunza Siri’ ya Kuridhika?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
  • Pata Uradhi kwa Kutumia Kanuni za Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Unaweza Kuridhika na Fungu Lako Maishani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Unaweza Kudumishaje Maoni Yaliyosawazika Kuhusu Pesa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
w10 11/1 uku. 3

Je, Inawezekana Kuwa na Uradhi?

“Kuridhika kunawatajirisha maskini; kutoridhika kunawafanya matajiri wawe maskini.”—Benjamin Franklin.

KAMA msemo huo unavyoonyesha, watu wengi wamegundua kwamba uradhi hauwezi kununuliwa kama bidhaa. Si ajabu kwamba ni vigumu kuwa na uradhi—ile hali ya ndani ya kuhisi kuwa umeridhika au umetosheka—kwa kuwa tunaishi katika ulimwengu unaotuchochea kuwa na tamaa ya kupata mali nyingi, kutimiza mengi, au kufurahia maisha kama wengine wanavyofurahia! Je, umewahi kupatwa na hali yoyote kati ya hizi zifuatazo?

• Matangazo ya biashara yanayokuchochea uamini kwamba licha ya vitu vingi ambavyo tayari umenunua, unahitaji kununua vitu vingine zaidi ili uridhike.

• Mashindano kazini au shuleni yanayokuchochea ulinganishe uwezo wako na wa wengine.

• Kutothaminiwa kwa mambo unayowafanyia wengine.

• Kuchochewa na marafiki utamani vitu walivyo navyo.

• Kukosa majibu kwa maswali muhimu kuhusu maisha.

Ikiwa umepatwa na hali kama hizo, je, unaweza kuwa mwenye uradhi? Mtume Paulo alisema ‘nimejifunza jinsi ya kuridhika.’ Nyakati fulani alikuwa na vitu vingi na nyakati nyingine vitu vichache. Marafiki zake walimheshimu lakini wengine walimdharau. Hata hivyo, alisema “nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali.”—Italiki ni zetu; Wafilipi 4:11, 12, Biblia Habari Njema.

Kuridhika ni fumbo kwa wale ambao hawajawahi kuchukua hatua ya kusitawisha hali hiyo, lakini kama Paulo alivyosema, mtu anaweza kujizoeza kuwa mwenye uradhi. Tunakualika uchunguze njia tano zinazoweza kukusaidia kuwa mwenye kuridhika, ambazo zinapatikana katika Neno la Mungu, Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki