Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w13 12/1 uku. 3
  • Kwa Nini Tujiulize Swali Hilo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Tujiulize Swali Hilo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Habari Zinazolingana
  • Utamwambia Nini Mtu Asiyeamini Mungu?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Kanisa—Mabadiliko na Mvurugo
    Amkeni!—1993
  • Je, Ni Lazima Uwe Mfuasi wa Kanisa Fulani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Kwa Nini Kanisa Linapoteza Uvutano?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
w13 12/1 uku. 3

HABARI KUU | JE, TUNAMHITAJI MUNGU?

Kwa Nini Tujiulize Swali Hilo?

“Je, wewe ni miongoni mwa watu wasioamini Mungu? Wengi hawaamini.” Maneno hayo yalikuwa kwenye bango lililotengenezwa na kikundi cha watu wasioamini Mungu. Wanahisi kwamba hawamhitaji Mungu.

Kwa upande mwingine, watu wengi wanaodai kumwamini Mungu hufanya maamuzi mabaya yanayoonyesha kwamba Mungu hayuko. Kasisi Mkatoliki, Salvatore Fisichella, alisema hivi kuhusu waumini wa kanisa lake: “Mtu akitazama mtindo wetu wa maisha hawezi kutambua kama sisi ni Wakristo, tunaishi kama watu wasioamini.”

Watu hawajali kwamba kuna Mungu. Wao hufikiri ni vigumu kumkaribia Mungu. Hata hivyo wao humtafuta Mungu wakati ambapo wanahitaji msaada—kana kwamba Mungu ni mtumishi wao.

Wengine hawaoni umuhimu wa kufuata mafundisho ya dini. Kwa mfano, asilimia 76 ya Wakatoliki nchini Ujerumani wanaamini kwamba ni sawa mwanamume na mwanamke kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa—maoni ambayo yanapingana na mafundisho ya Biblia na hata mafundisho ya kanisa. (1 Wakorintho 6:18; Waebrania 13:4) Bila shaka, mbali na Wakatoliki watu wa dini nyingine pia hawaishi kulingana na mafundisho ya dini zao. Viongozi wa dini mbalimbali husikitika kwa sababu waumini wao wanaishi sawa na watu wasioamini Mungu.

Mifano hiyo inatufanya tujiulize swali hili: Je, kweli tunamhitaji Mungu? Hilo si suala jipya. Linapatikana katika kurasa za mwanzo za Biblia. Ili tupate majibu, acheni tuchunguze baadhi ya mambo yanayotajwa kwenye kitabu cha Biblia cha Mwanzo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki